Taarifa nilizopata juu ya chaguzi za CCM; ni hatari kwa nchi hii

Taarifa nilizopata juu ya chaguzi za CCM; ni hatari kwa nchi hii

Hili la rushwa ni nchi nzima na majimbo yote, kule kilwa wajumbe Wana kauli moja tu "anaetoa pesa nyingi ndiye anayepewa kura nyingi"
 
Ccm hawafai kabisa mim nimeshiriki hizi mambo za kura za maoni mwaka huu 2020..sijui kwa miaka mingine ila kwa mwaka huu nauhakika rushwa nimeshuhudia mwenyewe 100% kwakweli pesa imetembea na tusitegemee viongozi waadilifu lazima watarudisha chao..hapo ndio deals zitatembea
Kwa maana hiyo habari za kuwa Magufuli amepambana kupiga vita rushwa ni UONGO MKUU.
Magufuli amelea rushwa na kuigeuza kuwa mfumo ndani ya CCM kuliko kiongozi mwingine yeyote katika historia ya CCM.
 
Nawaomba mnisome hapa:
Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao. Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.

Hakuna kitu umeandika, ccm na rushwa ni sawa na ngozi na mtu, Hawaachani
 
Bahati mbaya Ni kwamba hata Mwenyekiti wa chama ameotia huko huko, anajuwa kuwa alikuwa anatumia njia gani ili kupita kwenye Kura za maoni. Kwa hiyo msitegemee jipya. Aliyepata Kura nyingi ndo anayeensa kuwa mgombea.
Huyu alinunua hadi wagombea wa upinzani ili apite bila kupingwa
 
Mh Raisi akemee hii kwa vitendo, atume TISS wafanye uchunguzi kwa wale wote waliotoa rushwa iliyokithili

Watuondolee watoa Rushwa tubaki na wazalendo ambao hawataenda bungeni kufanya biashara hili pesa zao ziludi
Huko ccm wote wametoa rushwa,ila wamezidi ana tu.
Magu akitumia hiyo taasisi hayupo atakayepona,sasa unataka CHADEMA wachukue nchi?

Au wewe unaonaje? Mi nadhani hii hali siyo mbaya sana kwa vile ccm tumewanunua wapinzani kwa hela tuendelee hivi hivi.

Kwani hujui dawa za maumivu wakati mwingine huwa zinaahirisha homa?
 
Mh Raisi akemee hii kwa vitendo, atume TISS wafanye uchunguzi kwa wale wote waliotoa rushwa iliyokithili

Watuondolee watoa Rushwa tubaki na wazalendo ambao hawataenda bungeni kufanya biashara hili pesa zao ziludi
Hili likifanyika vyema, kuna majimbo yatapaswa kurudia kura za maoni.
Shida ni kubwa kuliko inavyodhaniwa.
Moshi ulikolea, moto umeanza.
 
Umeitaja Ukerewe na wakati huu niko huku. Hapa Ukerewe siyo siri. Mambo yako wazi kabisa. Kilichofanyika na kinachoeleweka kwa watu wa hapa ni kwamba. Mbunge aliyehamia CCM hakubaliki. Kura za maoni amepita na haijulikani jina litarudi au hapana. Lakini kupita kwake ni rushwa kwa kusaidiwa na viongopzi wa CCM wa Wilaya; Mkiti, Katibu, PCCB na usalama wa Wilaya, wote walipigwa milioni 5 kila mtu.

Siku ya uchaguzi kila mjumbe akarushiwa 70 kwenye simu yake. Niambie mtu wa aina hiyo au mfumo wa aina hiyo utatuletea nini. Yaonekana ni nchi nzima ndo mfumo uliotumika.
Rushwa na ccm ni sawa na uji kwa mgonjwa,wao kuanzia nambari uno ni rushwa tu
 
Kweli ccm imeoza na inazidi kuoza. Rushwa ya mwaka huu haijapata kutokea tangu ccm ianzishwe. Watanzania tutafute mbadala wa hawa walafi.
Mwaka huu rushwa zimezidi kuliko miaka yote licha ya mkaripio wa Raisi
 
Mwaka huu rushwa zimezidi kuliko miaka yote licha ya mkaripio wa Raisi
Kabla ya kura za maoni CCM kupitia Polepole walitangaza utaratibu wa kura za maoni kuwa ni ule wa watia nia wote kuchujwa na vikao kuanzia wilaya, mkoa na hatimae kamati kuu kurudisha majina 3 ya watia nia ili yapigiwe kura ya maoni, tena yanasomwa ndani ya mkutano na kura zinapigwa.. Utaratibu huu ndio ulikuwa umefunga mlango wa rushwa..baada ya kikao cha mafunzo kwa wenyeviti wa CCM wilaya na mkoa kilichoitishwa mwezi juni, walilalamikia utaratibu huu kwamba utaleta lawama na eti si wa kidemokrasia, kukata majina ya watia nia na kurudisha majina 3... hadi sasa ni vigumu kuelewa sekretariat ya CCM taifa ilishindwa kuona na kugundua lengo ovu la wenyeviti kutaka utaratibu wa zamani huu waliotumia ndio utumike.. huu ndio uliifikisha CCM shimoni mwaka 2015, kiasi cha kuchukiwa na kila mtu sababu ya rushwa ndani ya chama..sasa wamejionea kile wenyeviti wao walikitaka..ni ujinga kuwa na demokrasia inayowaletea janga halafu mnaanza kuhangaika nalo wakati mgeweza kulizuia..huwezi kupambana na rushwa kwa kutaja namba ya simu au kutegemea taarifa kutoka kwa watu..SAHAU! hata kama TAKUKURU wangekuwa na ofisi kila kijiji. Tupambane na rushwa kwa kuweka taratibu zinazozuia rushwa kufanyika! Utaratibu wa majina 3 ulikuwa unazuia rushwa kufanyika..ngoja tusikilize najua Mwenyekiti wa CCM Taifa angeweza kufuta wenyeviti wote wilaya na mikoa kwa ushauri mbovu kabisa waliotoa kwa sekretariat hadi katiba ikabadilishwa..lkn kwa vile wanapigiwa kura nadhani 2022 chama kiwaondoe wote wasigombee tena ili kung'oa mizizi ya rushwa ndani ya chama hicho ndicho wanastahili.
 
Mh Raisi akemee hii kwa vitendo, atume TISS wafanye uchunguzi kwa wale wote waliotoa rushwa iliyokithili

Watuondolee watoa Rushwa tubaki na wazalendo ambao hawataenda bungeni kufanya biashara hili pesa zao ziludi
Tissini gani hao watumwe ambao hawapokei rushwa? Hawa hawa wa mshahara laki 9? Nchi hii rushwa itaisha siku keki ya taifa ikigawanwa kwa usawa hakuna muujiza mwingine.

Keki ya taifa ikiendelea kubaki huko bungeni tu tutayashuhudia haya kila uchwao.

Kama suala la rushwa linajulikana mafaili yapo mezani kabla na baada ya uchaguzi lakini nani atayafanyia kazi? Nani atamgusa nani atamuacha nani? Na huyo anayegusa wenzio mikono yake ni misafi? Akijitahidi sana atafanya double standards.
 
Kabla ya kura za maoni CCM kupitia Polepole walitangaza utaratibu wa kura za maoni kuwa ni ule wa watia nia wote kuchujwa na vikao kuanzia wilaya, mkoa na hatimae kamati kuu kurudisha majina 3 ya watia nia ili yapigiwe kura ya maoni, tena yanasomwa ndani ya mkutano na kura zinapigwa.. Utaratibu huu ndio ulikuwa umefunga mlango wa rushwa..baada ya kikao cha mafunzo kwa wenyeviti wa CCM wilaya na mkoa kilichoitishwa mwezi juni, walilalamikia utaratibu huu kwamba utaleta lawama na eti si wa kidemokrasia, kukata majina ya watia nia na kurudisha majina 3... hadi sasa ni vigumu kuelewa sekretariat ya CCM taifa ilishindwa kuona na kugundua lengo ovu la wenyeviti kutaka utaratibu wa zamani huu waliotumia ndio utumike.. huu ndio uliifikisha CCM shimoni mwaka 2015, kiasi cha kuchukiwa na kila mtu sababu ya rushwa ndani ya chama..sasa wamejionea kile wenyeviti wao walikitaka..ni ujinga kuwa na demokrasia inayowaletea janga halafu mnaanza kuhangaika nalo wakati mgeweza kulizuia..huwezi kupambana na rushwa kwa kutaja namba ya simu au kutegemea taarifa kutoka kwa watu..SAHAU! hata kama TAKUKURU wangekuwa na ofisi kila kijiji. Tupambane na rushwa kwa kuweka taratibu zinazozuia rushwa kufanyika! Utaratibu wa majina 3 ulikuwa unazuia rushwa kufanyika..ngoja tusikilize najua Mwenyekiti wa CCM Taifa angeweza kufuta wenyeviti wote wilaya na mikoa kwa ushauri mbovu kabisa waliotoa kwa sekretariat hadi katiba ikabadilishwa..lkn kwa vile wanapigiwa kura nadhani 2022 chama kiwaondoe wote wasigombee tena ili kung'oa mizizi ya rushwa ndani ya chama hicho ndicho wanastahili.
Huo utaratibu ambao ulikuwa mwanzo na haukufatwa ulikuwa mzuri na ungepunguza rushwa na zoezi lingekuwa vyema maana wagombea CV zao zingepitiwa na kuchunjwa na kurudishwa hayo matatu na hapo mwanya wa rushwa ungepungua Sana, maana hao wajumbe kwanza ni rahisi kuwahonga maana unakuta hawafiki 400 na wabunge waliochukua kiinua mgongo hawaoni shida kuhonga hata laki mbili na wabunge wengi wameshinda.
Nadhani huu utaratibu uchunguzwe sio mzuri na majina yachunjwe Kama inavokuwaga kwenye application ccm wakiacha hivi huu mfumo wa rushwa aisee kwanza huko chamani watu watagawanyika na 2025 ccm itapata upinzani mkali kuliko wa 2015.
Pia chakushangaza hata viti maalumu, uvccm Napo rushwa kwa kwenda mbele kipindi hichi. I think kamati kuu iwakate wale watoa rushwa wote na iwe agenda maana image kwa jamii wote wameshinda kwa kuhonga
 
Wengi waliopata kura chache ni wale ambao hawakuhonga I wish hii tabia ikomeshwe Mara moja bila hivo maskini watabaki watawaliwa tu
Unataka atawale masikini ili iweje sema mfumo ubadirike namna ya kuwapata hao wajumbe au idadi iongezeke, mashart ya wagombea yaongezeke sio kila mtu anaweza kugombea.
 
Nimeona clip ikisemekana ni waziri wetu wa elimu akiwa ndani ya gauni la kitenge akiwezesha wajumbe nje ya geti.
Natafuta habari za mzee wetu aliyezaliwa Kilosa, tuone umahiri wa sheria ulimuongozaje.
 
Back
Top Bottom