Taarifa: waandamana kupinga ujio waBUSH


Sasa unachouliza ni nini au hoja yako ni nini?, usijitetee kijinga. Mie nakushangaa sana, nilikuwa nafikiri kuwa u-mtu mwenye mawazo mapana kumbe ndio wale wale, mbumbumbu mzungu wa reli. Na hili lilijisadikisha kule ulipoanza umatonya, nakuuliza, honestly, una asili ya ugogoni wewe?
 
ndipo ulipolenga hapo ? pole mkuu mkuki umepiga sipo.

tofautisha baina ya maziwa na tuwi.

au utaula na chuwa kwa uvivu wa kuchagua

Mtu wa pwani kiswahili chako nimekipenda ur trying to make a point
 

NAOMBA MSAMAHA
 
Wandugu nimeomba msamaha kwa maeno yaliyonitoka. Yamenitoka kwa sababu niliwahi kupata mateso makubwa kwa ajili ya imani hiyo. Mlipuko wa bomu pale ubalozi wa marekani dar ulinipotezea mpendwa wangu..waliohusishwa nao ni ile ile imani! Wakati fulani nilikuwa Qatar kikazi..nilipata sana matatizo na unyanyasaji kwa sababu sikuwa na hiyo dini..nilipoteza haki zangu zote kwa kuwa ni kafiri..kwa kifupi utu wangu haukuonekana kwa kuwa sikuwa na imani hiyo.
Kama wachangiaji wengi walivyojiuliza ni kwa nini matukio yote ya ugaidi yahusishwe na imani hiyo?
Huwa najizuia kuchangia chochote kama imani hii ikijadiliwa kwa sababu nimesha i-brand vibaya(si kusudi langu, circumstances). In the first place nisingetakiwa kuchangia chochote...lakini ndo hivyo ukiwa na fundo juu ya kitu fulani na kikatajwa unaweza shusha lolote bila kufikiri.

NAOMBA MSAMAH TENA SITACHANGIA KATIKA HILI..WALE WANAOTAKA SHINGO YANGU MNISAMEHE PIA.
 
TzPride,

Bila samahani mkuu kufiwa na ndugu ama rafiki yako haiwezi kuwa sababu ya kuchukia dini nzima maana hata sisi wengine tumezipata taabu hizo ktk nchi za ugenini iwe Arabuni ama Ulaya na hata siku moja siku judge matukio hayo kutokana na dini ama zangi zao ila yangu mimi..next time nakuwa makini zaidi napo approach vitu hivyo.
Maadam upo hai hii yote ni mitihani kwetu sote, utakutana na mengi na sii ajabu mengine hapahapa nyumbani ukachujwa kwa sababu ya maumbile, kabila au Utaifa.
Kwa taarifa yako Mwarabu hana udini isipokuwa ana ubaguzi kama wanavyobagua watu wengine, hata mimi yameisha nikuta pengine mazito kuliko yalokukuta wewe pamoja na kwamba nina imani sawa na yao, na wapo wenye imani tofauti wamekuwa treated vizuri. Kifupi sikwenda nchi hizo tafuta maisha kwa sababu ya imani yangu..na hata siku moja usije tegemea kupima mazuri ya binadamu kutokana na dini, jinsia ama rangi yako, utashangaa..
Kumbuka tu ktk Mauaji ya Ubalozi wa Marekani walikufa pia waislaam marafiki zetu...Kichaa ni cha mtu mmoja hakiwezi kubeba dhamana ya ukoo ama dini nzima. AS a fact Ujio wa Bush kwa hao waislaam wenye siasa kali nadhani wasingeandamana... wangekaa kimya wakamtafuta mjinga mwenzao wakambebesha bomu kumwondoa Bush na huyo mwenyeji wake JK kwa sababu kafanya kufuru kumleta shetani...Je, Umewahi ona maandamano Iraq, Afghanstan ya kumpinga Bush?...Hapana! na hiyo ndio tofauti yetu, mwenye chuki binafsi hasemi mkuu... hufanyiza!
Mkuu, kweli yawezekana sisi wajinga lakini sio wajinga hivyo!
 

Uwongo mtupu.
 

Huo ni upuuzi, na wale waoandama UDSM nao wametumwa na waarabu pia, mie nakushangaa wewe mtanzania gani huheshimu wajomba na shemeji zako?
 
Zomba,

Huyo Bakari Muhogo wala asikusumbue, message yake nzima imejaa sifa za umalaya!..Haelewi kinachoambatana na ujenzi wa barabara hizo na kwa nini basi wanaweka sahihi za Mkataba..
Ukimuuliza huo mkataba unahitaji malipo gani toka upande wetu haelewi kitu!.....
 
Uwongo mtupu.

Zomba,

Hata kama huamini hizo circumstances, basi amini kwamba nimeomba msamaha kwa dhati. Peace mkuu..nitajitahidi kutofanya makosa kama hayo tena.
 
Sawa kama unataka mtazamo wangu ktk swali lako nadhani tutarejea tena katika mjadala kama huu uliofanyika mwaka 2006..Niliwahi toa mfano wa karibu vile vile na kuuliza watu kama sisi weusi tungeshindwa kuondoa Ukoloni Africa kama tusingetumia jina la rangi yetu..weusi!.. [/QUOTE said:
Hivi hao hawana rangi? Waafrica waliunganashwa na rangi yao "weusi" kama ulivyosema ingawa walikuwa na Dini tayari. Hawa kwa nini wasiungane kwa Rangi yao au maeneo wanayotoka badala ya kutumia dini!!
 
Nyangumi,
Hivi hao hawana rangi? Waafrica waliunganashwa na rangi yao "weusi" kama ulivyosema ingawa walikuwa na Dini tayari. Hawa kwa nini wasiungane kwa Rangi yao au maeneo wanayotoka badala ya kutumia dini!!

Mkuu usinichekeshe.... sasa rangi gani tena hiyo, hivi walioandamana Dar -es-Salaam walikuwa na rangi gani..na kama wewe hukubaliani nao wataweza vipi kutambua sababu zilizokufanya usikubaliane nao. Bila shaka hukubaliani na maandamano hayo kwa sababu wewe sio Muislaam, lakini wapo wakritsu wanaokubaliana (support) na maandamano kama ya jana.

Ubaguzi una vipengele vingi ikiwa ni pamoja na rangi, kabila dini ama jinsia kwa hiyo usifikirie ubaguzi huja kwa watu weusi tu.
 
Zomba,

Hata kama huamini hizo circumstances, basi amini kwamba nimeomba msamaha kwa dhati. Peace mkuu..nitajitahidi kutofanya makosa kama hayo tena.

Peace, amani iwe juu yetu na si hisia zetu.
 
hawa ndugu zangu wana haki ya kuandamana.ndio demokrasia, however, agenda iko zaidi kwenye uislamu kwani naamini wanafikiri bush ni anti-islam! i dont know about that for facts but what i know bush amesaini mkataba mkubwa sana utakaosaidia miundombinu ya nchi na msaada wa afya(malaria/hiv-aids) ambao unaendelea kusaidia wananchi utaongezwa congress ikimaliza ku-debate.msaada ambao utadouble.for two facts nampongeza bush.na hii misaada haijasemwa kuwa ni ya wakristu au waislamu!! ni ya watanzania wote.hivi watu wamesahau kwamba osama aliua almost 300 kenyans na tanzanians wasiokua na hatia!! kisa anachukia sera za marekani! watu wengi wanalaumu sera za bush katika hiki kipindi chake cha miaka 7 ilopita, ambacho kimekua dictated na sept 11 attacks, now, kama osama asinge-facilitate zile attacks, marekani ingeingia afghanistan na iraq!!!!???98 osama(through agents) alilipua mabomu huko east-africa, clinton hakua serios na threat ya osama, zikatupwa tomahawks 3(long-range missiles) kutoka kwenye meli ilokua gulf, zikamkosa in a matter of 30mins, he then went on to plan and execute 9/11 ambayo marekani under bush ikaona lazma ifanye something because history ilish-judge kuwa huyu mtu akiachiwa anafanya something bigger and more lethal!! sasa wanaompinga bush kuwa ni katili, they should go back to his first year in white house, just before 9/11, did bush have plans to invede afghanistan and iraq before 9/11?? nobody knows for sure, but what i know if you are a president, and 3000+ of your civilians die in a single attack,lets be frank, how would react??
 
Kuna jambo moja rahisi sana!

Nina hakika asilimia kubwa sio wote walikuwa hata hawajui Bush amekuja Tanzania kufanya nini?

Tanzania watu wengi wanafanya mambo ki-imla imla tu, unaburuza unavyotaka!!!
 
Moshe Dayan,
Sawa mkuu....Je, ukiambiwa Ahmadinajad huyafanya hayo bado utampokea kwa moyo mweupe?...
jaribu kutuelewa tunapotenganisha Politics zao na maendeleo yetu...mkuu wangu.
 
mi ntampongeza tena sana tu.tunachotakiwa ni kujali anayetujali tukiwa kwenye shida bila kununuliwa kwa misaada.a friend in need is a friend..........., najua una jibu.we dont have to believe siasa zao za sisi wazuri wao wabaya.what we should do ni kuwaogopa ambao walishatuumiza, kama ahmad hajawahi kutuumiza na anatusaidia kwanini tusimpongeze?
 
 
mhh,interesting, i respect sana maoni yako, ila mi sidhani ka nipo bias.kama unaamini kwenye mlengo flani wa siasa utaona mi nipo bias.sasa tukianza kuleta habari za kina george sr. na wolfwitz tutaenda mbali.kwa sababu unatafuta facts za ambazo huzifahamu.tubishane kwa facts sio vitu vinavyoelea angani.hivi wajua mission ya gulf war ilikua nini!! haikua regime change, ilikua kuitoa iraq kuwait, kama wangetaka regime change wasingeshindwa, kwa sababu by then states ilikua na more international support kuliko sasa.thats fact! kuhusu powell UN, all intel gathered by that time ilionesha kua saddam alikua na WMD's, hata MI6 waliamini hivyo.thats a fact!swali, kwanini WMD's hazikukutwa? kwa kukuhabarisha, kuna investigation inafanyika saivi ambayo inaangalia if the WMD's were moved to Syria before invasion.Lakini at the same time, nataka niwe fair, its very possible hakukua na WMD's, now, were did they get it wrong, kwanza it depends on ASSETS(foreign agents) ambao walikua wanaipa data marekani.yawezekana walikua wanawaambia wamarekani kile ambacho wamarekani walikua wanataka kukiskia kwa sababu these cooks are well paid na ntu anataka aendelee kuwa kwenye paycheck ya wamarekani,hizi mistakes zishatokea sana na ndo mana watu sasa wanabase zaidi kwenye technology, pili, kutokana na picha za satellites, inaonekana kabisa kulikua na programmes za WMD's zinaendelea, lakini, hii inaweza ilikua strategy ya saddam kuonesha wako militarly strong.kwa sababu for sure alikua anajua big brother was watching everything, therefore its very possible alikua anafanya bogus activities as if anatengeneza WMD's ili ku-create fear.hiyo imo kwenye ulimwengu wa vita.
 
one more thing, kuhusu usemi ulosema kua clinton hakuwaskiliza kina wolfwitz, ngoja nikupe fact, marekani vyama vya siasa vina sera tofauti, kama republicans wao kihistoria ni watu wanaopenda vita, very aggressive, ambao hawazingatii sana diplomacy, am sure unajua bwana hivi vitu.democrats ni opposite and thats why clinton alikua na mtazamo tofauti kabisa na g sr.
 
Kuna watu wanapinga ujio wa Bush kwa msingi kuwa anapinga vita uislamu. Kwa hiyo watu hao wanaunganisha wengine wote wanaokosoa kitendo cha wasilamu kuandamana kupinga ujio wa Bush kwa madai kuwa wote hao ni maadui wa uislamu. Hiyo siyo kweli na huenda inavuruiga kabisa thamani ya mjadala huu.

Ukweli ni kuwa maandamano haya na namna yalivyofanyika (kuanzia msikitini na uchomaji wa bendera ya Marekani) ni kazi ya viongozi wachache sana wa dini ya kiislamu ambao wamekuwa mbele sana kutumia waislamu ili wao binafsi wajipatie ujiko fulani. Siamini kabisa kuwa huo ndio msimamo wa waislamu wote nchini kwa vile mtu aliyemkaribisha Bush ni mwislamu. Mwaka juzi tulishuhudia ufisadi uliofanywa na baadhi ya viongozi hao hao wa kiislamu kujipatia mali kwa kuuza kiwanja cha chuo cha Bakwata wakidai kuwa mtu aliyeuziwa ni mwislamu safi na atawasaidia waislamu; hivyo wakawa wanawasukumiza waislamu wamtetee kwa nguvu sana mtu huyo hadi ikafikia waislamu kuichukia IPP kutokana na mgongano uliokuwapo kati ya Mengi na mwislamu huyo.

Mwishoni mshindi anakuwa na yule kiongozi binafsi aliyewasukumiza waislamu na wala siyo waislamu wenyewe wanoafaidika na juhudi za kiongozi huyo.

Ni kweli kabisa kuwa ujio wa Bush siyo ujiko kwa Tanzania, bali ni kwa ajili ya maslahi ya Marekani. Hata hivyo, ni lazima tukubali kuwa kwa vile tumejijenga kama taifa linalotegemea misaada kutoka nje, basi hatuwezi kuwazuia wao wasitupatie dola milioni 700 halafu wakavuna kitu chenye thamani mara mia ya kiasi hicho. Tulichotakiwa ni kuwakumbusha viongozi wetu kuwa wana dhamana ya kulinda maslahi ya nchi katika mikataba yoyote wanayofanya.

Binafsi sikubaliani kabisa na sera za Bush kwa nchi za nje na hata kwa hapa ndani ya Marekani. Sera za Bush hazikubaliki karibu duniani kote. Tuna haki ya kuungana na wenzetu duniani kuonyesha kuwa hatukubalini na sera hizo kwa njia ya maandamano kama watanzania; hiyo ni sawa kabisa. Tungeaandamana kwa ustaarabu kabisa tukiwa na mabango makubwa sana yanayoonyesha wazi kabisa kuwa hatukubalinai na sera za kibeberu za Bush. Hakuna haja ya grupu moja la waislamu kuandamana kuwa sera hizo ni dhidi ya uislamu tu kama vile zinatetea dini nyinine. Labda niwakumbushe wale wote wanaomuangalia Bush kwa msingi wa Uislamu kuwa:

  1. Huko Iraq walioathirika ni wairaq wote,, waislamu na wakristo wote kwa pamoja. Ikumbukwe kuwa yule Tariq Aziz aliyekuwa Deputy Prime Minister na Waziri wa mambo ya nje alikuwa ni mkatoloki (jina lake halisi Mikhail Yuhanna). Yeye vile vile mpaka sasa bado yuko kifungoni kutokana na uvamizi wa Bush. Baada ya Uvamizi huo watu wote walioko madarakani huko Iraq sasa hivi ni waislamu, hakuna hata mkristo hata mmoja. Kwa hiyo kudai kuwa uvamizi huo ni kupinga uislamu ni makosa makubwa sana. Ukweli ni kuwa amewasadia zaidi waislamu wa shiite dhidi ya wale wa Sunni na Wakristo.
  2. Uvamizi wa Afghanstani ulitokana na Bin Laden alieongoza mashambulizi ya 9/11 kujificha huko na serikali ile ikamhifadhi. Inajulikana kabisa kuwa marekani haikuwa na mpango wowote na Afghanstani kabla ya hapo. Uvamizi ule uliondowa Waislamu wa Taliban kutoka madarakani na kusimika waislamu wengine madarakani. Sioni kama kitendo hicho ni kupiga vita uislamu.
  3. Swala la Palestine ni la muda mrefu sana na linajulikana kabisa dunian kote. Mara ya mwisho wakati Clinton anataka kugawanya eneo lile kuwa na nchi mbili huru za Israel na Palestine, ni wapalestine wenyewe waliokataa mpango ule. Bush aliingia madarakani mara tu baada ya juhudi hizo za Clinton kushindwa. Kosa lake ni kuwa aliweka kiburi kutolishughulikia tena swala hilo mpaka baada ya muda mrefu sana wakati watu wengi wameshpoteza maisha yao. Hata hivyo, kuna makosa sana kudhani kuwa mgogoro huo unawaathiri waislamu tu. Ni mgogoro unaotahiri watu wa dini zote katika eneo lile.
  4. Nadhani kuwa kwa population ya Marekani, rais Bush kawaweka waislamu wengi sana serikalini kwake; hivyo sidhani kama anawachukia waislamu. Tatizo lake ni ubeberu, ubabe na labda tamaa ya kutawala visima vya mafuta.
Baada ya kuelezea hapo, ndiyo maana nasema kuwa msimamo wa waislamu kuandamana kupinga ujio wa Bush ati kwa sababu anapiga vita uislamu ni makosa makubwa sana. Ukweli kilichotakiwa na maandamano ya watanzania kulaani sera sera za Bush kwa kusisitiza kuwa ni mbaya kwa watu wote siyo waislamu tu; hakukuwa na maana ya kupinga ujio wake wakati tayari ameshafika nchini. Kutumia uislamu kunapunguza kabisa uzito wa ujumbe ambao ungefika kwa Bush kutokana na maandamano yale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…