Mwafrika wa Kike,
Mkuu katika hili angalia kuwa hata wanaotetea maandamano hapa wamesema wenyewe kuwa haya ni maandamano ya waislam na wanatetea issue za waislam. Hapa ndipo nilipoingia katika debate hii ili kuondoa dhana kuwa hii ni issue ya dini fulani pekee (kumbuka mfano wangu wa wanafunzi wa mlimani
Shukran, Kwanza soma sentesi yako ya kwanza inayohusu wenye nguvu, umesema hata Marekani hu - lebel watu hasa minority lakini sio sivyo inapokuwa ni Wazungu... Yet, umeshindwa kuelewa kuwa hawa minority wa Marekani watakapo andamana wataandamana kwa rangi zao na kijieleza hata kama watakuwemo Wazungu kati yao. Huwezi kupigania equal right Marekani bila kujieleza una represent kundi gani?.. hivyo basi hata Blacks Marekani hujitambulisha/hutambulishwa wao kama blacks pamoja na kwamba wanaoandamana sio wote blacks.
Ndivyo ilivyokuwa Dar, walioandamana hawakuwa wote waislaam, pili nilishasema kuwa neno Waarabu linakuwa lina limit mipaka ya malalamiko ya hawa waislaam kwani swala sio Iraq tu..lakini kinachowaunganisha wote hawa ni dini yao.
Mkuu, ebu jiulize hivi, pamoja na yote haya inakuwaje Obama anashangiliwa zaidi nchi za Kiislaam na ni hope ya wengi ikiwa Obama sio Muislaam na pia ni Mmarekani kama alivyo Bush.... Why mnashindwa kuelewa hilo ama kwa sababu Mnamtazama Bush kama ni mkristu, hivyo waislaam wana mpinga kwa sababu ana represent Wakristu!... Najua ndivyo walivyokuwa wakifikiria wazungu wengi enzi za Mkoloni - Ukipinga Ukoloni basi bila shaka unawachukia wazungu..Je, ni hiki mnachokiogopa?...kama ndivyo how come nchi hizo hizo zina mahusiano mazuri na nchi kama Italy, France, Germany na hata Vatican?
Unajua Mwafrika wa Kike nadhani kuna maswala mengine ni vigumu kwako kuelewa ikiwa wewe sio Muislaam kama vile tunavyoshindwa kuelewa mambo mengine ya wanawake!..
Mimi nilitegemea itakuwa rahisi kwenu kuelewa kwa sababu yamekwisha kufikeni, kwani Ubaguzi wa South Afrika na Zimbawe hatukuusema kwa makabila yaliyohusika (Wazuru, Nkosa, Washona ama Wandebele) wala hatukuwaita Wa south au Wazimbabwe wanaonewa! bali tulitumia kile kinachotuunganisha sisi sote nacho ni weusi wao kutokana na Apartheid yenyewe ilivyowatenga. Na hakika waliotengwa walikuwa weusi sii kwa makabila yao ama Itaifa wao. Huu ni ukweli ambao haupendezi masikioni but the fact remains kuwa weusi ndio waliopata matatizo ya Ubaguzi South, bila kujali kabila zao ama Utaifa wao. Na kama ingelikuwa kwa dini zao ni lazima tungetumia dini. Zipo nchi tunalalamika kuhusu uhuru wa Wakristu sehemu hizo na hatuwaiti ati Waarabu, bali ile sababu iliyofanya kutengwa.
Leo ktk swala la Iraq au Afghanstan mnataka tuseme Waarabu hali ubaguzi wa mzungu unasema wazi kuwa Magaidi (terrorists) ni Waislaam hawasemi Waarabu, hivyo wameidhinisha miswada ya kuwafuata huko huko kwao - Nchi za Kiislaam, regarless of their nationality.