Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa ya yanayoendelea Pemba, taarifa hiyo imeandaliwa na Maalim Seif na kutolewa kwa Umma

=======
Taarifa zilizothibitishwa kutoka Pemba zinasema wananchi watatu wameuawa kwa silaha za moto na Jeshi la Polisi kuelekea mwanzo wa upigaji kura siku ya kesho, wengine tisa wamejeruhiwa.

Usiku huu Jeshi limekuwa likigawa masanduku ya kupigia kura kwenye vituo kwa ajili ya upigaji kura wa awali. Wananchi wanaozunguka maeneo hayo wamedai kwamba masunduku hayo tayari yana kura zenye alama. Wananchi hao walizuia masunduku hayo kwenda kwenye vituo vya kupigia kura, polisi walianza kurusha mabumu ya machozi kwenye jaribio la kutawanya mkusanyiko. Baada ya kushindikana, wakatumia silaha za moto. Bahati mbaya, imepelekea vifo vya Wazanzibari watatu na tisa kujeruhiwa.

Waliofariki katika kijiji cha Kangani
  1. Asha Haji Hassan(33)
  2. Yussuf Shaame Muhiddin(27)
  3. Kombo Hamad Salum(30)
Waliojeruhiwa kwa sialaha za moto
  1. Abbas Haji Nyange(27)
  2. Bakari Khamis Bakari(50)
  3. Mukhtar Yahya Hassan(16)
  4. Khamis Mohammed Mmanga(40)
  5. Hassan Kombo Ali(13)
  6. Abbas Mgau(22)
  7. Mgau Omar Mgau(35)
  8. Hamad Omar Hamad(20)
  9. Ali Hamad Seif(16)
Kulingana na vyanzo eneo hilo, imekuwa kuwachukua waliojeruhiwa kwenda hospitali kutoka Kangani kwa sababu barabara zote kuelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete zinasimamiwa na vyombo vya usalama.

UPDATE:

Screen Shot 2020-10-27 at 08.41.33.png
Screen Shot 2020-10-27 at 08.41.48.png



Zanzibar 1.jpg


Zanzibar 2.jpg
 
ZANZIBAR: MAALIM SEIF ALAANI MAUAJI YA WATU WATATU YALIYOFANYWA NA VIKOSI VYA USALAMA

Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo Maalim Seifa Sharrif Hamad amelaani vikali mauaji ya watu watatu yaliyotokea kijiji cha Kangagani, Pemba

Kwa mujibu wa Maalim Seif, polisi walikuwa wanasambaza karatasi za kupigia kura katika vituo, wananchi walidai baadhi ya karatasi hizo zilikuwa zimeshatiliwa tiki kwa baaadhi ya wagombea

Kutokana na hilo ilizuka ghasia iliyolazimisha Polisi kutumia nguvu iliyopelekea mauaji ya watu watatu na wengine tisa kujeruhiwa

Taarifa inasema majeruhi wamepata ugumu wa kufika hospitali kwa kuwa njia zinazoelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete zimedhibitiwa na maafisa usalama



1603755768083.png



1603755777785.png
 
Back
Top Bottom