Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Zanzibar 2020 Taarifa ya ACT Wazalendo yasema watu watatu wamefariki kwa kupigwa risasi na Polisi huku tisa wakijeruhiwa Zanzibar

Cha ajabu jana kulikuwa na clip inazunguka mitandaoni raia wanawarushia polisi mawe lakini Maalimu Seif hakutoka wala kutweet kulaani hilo tukio.
 
Sawa ngoja tuendelee mpaka hapo tutapofikia siku zote nazi haivunji jiwe.
Tatizo askari hutafuta chanzo cha kuwafanyia uharamia wapinzani,sasa Hawaii vijana wadogo ndio wanakuwa victims,tumepata habari ya kuwa askari Pemba wamekuwa wakipita na magari,bila ya kushuka,na wamefyatua risasi kwa raia,waliokaa mabarazani,na kuuwa watu wasio na hatia,nakubali nazi haivunji jiwe,jee itakapofika jiwe likavunja jiwe,wewe hili utalichukulia vipi?,sababu mwenye nazi na yeye anal uwezo wa kulimiliki jiwe vilevile.
 
Cha ajabu jana kulikuwa na clip inazunguka mitandaoni raia wanawarushia polisi mawe lakini maalimu seif hakutoka wala kutweet kulaani hilo tukio.
mawe haijibiwi kwa Risasi ya moto. Angalia Afrika kusini au nchi zingine jinsi polisi wanavyopambana na waandamanaji wanaorusha mawe. kwa sheria za ICC hilo ni kosa tena kubwa sana.

Ni Israel pekee wanaojibu kwa risasi nao wanasababu huwa wanasema walijichanganya na watu wenye bunduki ndio maana wanfayatua risasi kwa lengo la kumpiga mtu aliyeshika bunduki na sio aliyeshika jiwe. Kwa walichofanya jana Polisi ni Kosa tena kubwa sana

Tunaendelea kuangalia
 
Mkoloni kaharibu akili ya Mwafrika, tazama tunavyouwana wenyewe kwa wenyewe, mambo haya wazungu hawana, hawauwani kwasababu ya madalaka..
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa ya yanayoendelea Pemba, taarifa hiyo imeandaliwa na Maalim Seif na kutolewa kwa Umma

=======
Taarifa zilizothibitishwa kutoka Pemba zinasema wananchi watatu wameuawa kwa silaha za moto na Jeshi la Polisi kuelekea mwanzo wa upigaji kura siku ya kesho, wengine tisa wamejeruhiwa.

Usiku huu Jeshi limekuwa likigawa masanduku ya kupigia kura kwenye vituo kwa ajili ya upigaji kura wa awali. Wananchi wanaozunguka maeneo hayo wamedai kwamba masunduku hayo tayari yana kura zenye alama. Wananchi hao walizuia masunduku hayo kwenda kwenye vituo vya kupigia kura, polisi walianza kurusha mabumu ya machozi kwenye jaribio la kutawanya mkusanyiko. Baada ya kushindikana, wakatumia silaha za moto. Bahati mbaya, imepelekea vifo vya Wazanzibari watatu na tisa kujeruhiwa.

Waliofariki katika kijiji cha Kangani
  1. Asha Haji Hassan(33)
  2. Yussuf Shaame Muhiddin(27)
  3. Kombo Hamad Salum(30)
Waliojeruhiwa kwa sialaha za moto
  1. Abbas Haji Nyange(27)
  2. Bakari Khamis Bakari(50)
  3. Mukhtar Yahya Hassan(16)
  4. Khamis Mohammed Mmanga(40)
  5. Hassan Kombo Ali(13)
  6. Abbas Mgau(22)
  7. Mgau Omar Mgau(35)
  8. Hamad Omar Hamad(20)
  9. Ali Hamad Seif(16)
Kulingana na vyanzo eneo hilo, imekuwa kuwachukua waliojeruhiwa kwenda hospitali kutoka Kangani kwa sababu barabara zote kuelekea Chake Chake, Vitongoji na Wete zinasimamiwa na vyombo vya usalama.

UPDATE:

View attachment 1613359View attachment 1613360


View attachment 1613146

View attachment 1613147
Ccm wanadhulumu uhai wa watu sana siku hizi mauaji yamekuwa mengi tuwakatae ccm kesho.
 
Back
Top Bottom