Huyu ni Padri wa Kanisa Katoliki. Hawaruhusiwi kuoa. Ana familia kubwa, ana wajukuu, hapa anahaha kuwatafutia kula yao. Alikuwa Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu. Ndiye aliyempokea Papa alipokuja. Kidogo awe Askofu, ingekuwaje?Mungu wa mbinguni ampe maisha marefu ndugu Dr. Wilbroad Peter Slaa. Mbulu akiwa na akili anakuwa akili kubwa kupita wote na huwezi kuiga akili yake.
Jiulize: hawa ni wajukuu, aliwapataje bila kuwa na mke au wake? Kwa lugha yake, mikataba ya bandari ni ya gizani. Basi na Familja yake ni ya giza. Aliwezaje kulidaganya Kanisa muda wote huo? Tangu Sekondari, Seminari Ndogo, Seminari Kuu, Shemasi, Padri, PhD. Wangapi wamejaribu kulidanganya Kanisa wakashindwa? He must be very clever.
Je, tuzidi kumwamini sasa anatenda ya Mungu kumbe anajitafutia hela kwa mabeberu kulisha familia yake ya maasi?
Alilishinda Kanisa kwa muda mrefu lakini baadaye likagundua likamfukuza. Sisi tuendelee kumwamini mpaka lini? Amkeni.