Taarifa ya daktari wa rais

Taarifa ya daktari wa rais

Wakati fulani katika umri wangu wa ujana Bibi mzaa Mama yangu aliniita na kuniasa kuwa nipunguze mahusiano yangu ya ngono na mabinti ambao nilikuwa nao wengi. Aliniambia wazi kuwa endapo nitabahatika kufika uzeeni shughuli hiyo ingeniathiri sana kiafya ikiwemo kuishiwa nguvu sio tu kwa ngono bali hata kupumua.
JK naye tumekuwa tukisikia "ushujaa" wake kwa mabibi. Huenda hili aliloniasa bibi yangu lina ukweli?
 
Past history ya afya ya raisi, signs na symptoms zinazotajwa ktk incidence ya Mwanza na matokeo ya uchunguzi na vipimo vilivyofanywa haviendani na diagnosisi iliyotolewa na daktari

kuishiwa nguvu, kulazimika kwenda kupumzika ni kawaida...sio sawa na kupata blackout na kubebwa kupelekwa ndani,

taarifa ya daktari inaleta maswali zaidi kuliko majibu,
kuzidi kwa damu mwilini ni nini tena? au ana maanisha kuzidi kwa red blood cells (polycythemia), kama ndio hivyo, basi hiyo sio habari nzuri maana complications zake zinazidi hiyo faida ya kuchangia damu
 
Wakuu, heshima mbele,
Kadri tunavyozidi kwenda mbele tunadafua mengini. Ukweli ni kuwa mkuu wetu wa nchi anaumwa. Waombe Mungu, hii kuficha ficha isije waumbua mbeleni "even before the 2010" Mola apishie mbali.
 
itakuwa njaa tu maana anaonekana anapenda sana kulakula..wawe wanamuwekea karanga na visheti mfukoni awe anatafuna tafuna akiwa kwenye mikutano

kama ivo si waweke tu mezani kwenye sahani...yasije kuwa yale ya Mr.Bean na peremende kanisani..
 
Mkuu hapo umechemka nani kasema colonoscopy ukifanyiwa unakuwa sedated, ni kitendo cha dakika kadhaa na unakuwa macho. kama unataka unajiona utombo wako kwenye screen.....bring facts mkuu!

YE wewe hujui hiki kipimo cha colonoscopy kinafanywaje; utauonaje utumbo wako wakati uchunguzi unafanywa kupitia matakoni? You have to be sedated.
 
YE wewe hujui hiki kipimo cha colonoscopy kinafanywaje; utauonaje utumbo wako wakati uchunguzi unafanywa kupitia matakoni? You have to be sedated.
Magonjwa mengine jamani hayajali hata wadhifa, anyaway mkuu, can u expln a bit, unanitisha kuna vipimo kama hivi?
 
ni vizurii kuwa na uhakika na afya ya Raisi wetu. Asante Daktari kwa ufafanuzi yakinifuuuuu...ila ni gharama kweli kutambua vyotee hivyooo!!

Kwani isingetosha kutwambia kwamba afya ya Rais ni nzuri. Daktari ameweka details nyingi ambazo zitaibua maswali kwa nini wameenda mbali mno kuelezea afya ya Rais. Kulikoni? Kuna msemo wa Kihaya unasema hivi: "Banshabile ekanyisibwa nyinayo" Tafisri ni kwamba "mwanamke akibakwa ni yeye wa kwanza kueneza habari ya kubakwa kwake! Akinyamaza hakuna hatakayejua maana mbakaji hawezi kusema.
 
Halafu tena mwezi ujao anaenda Jamaica, kwanini hizi safari asimpunguzie makamu wake Shein!!! Anasafiri mno huyu mzee!!
 
Kwani isingetosha kutwambia kwamba afya ya Rais ni nzuri. Daktari ameweka details nyingi ambazo zitaibua maswali kwa nini wameenda mbali mno kuelezea afya ya Rais. Kulikoni? Kuna msemo wa Kihaya unasema hivi: "Banshabile ekanyisibwa nyinayo" Tafisri ni kwamba "mwanamke akibakwa ni yeye wa kwanza kueneza habari ya kubakwa kwake! Akinyamaza hakuna hatakayejua maana mbakaji hawezi kusema.

si alijidai kuonyesha ufundo wa kujieleza ooh mimi ni daktari wa rais mara tummpima ulimi,bandama ,na maini yako safi ..sasa kachokoza nyuki..unajua ikulu imejaa watu wanaokosa umakini sana.unakumbuka wakati bunge linataiti issue ya RICHMOND,akatokeza katibu mkuu kiongozi akasema oooh rais alikataza hela zisilipwe lakini hawakusikia..sasa mkuu kaanguka afya mgogoro haya tena wamekuja na bonge la ripoti lililojaa contradiction.this time hatuwaachii ngo watatueleza tu anaumwa nini au watukabithi tumpeleke hospital binafsi tumpime.haiwezekani asiwe anaumwa kitu..teeeh eti aliumia mgongo wakati mdogo hapo ndo nimechoka sasa na mikiki mikiki ya kule jeshini aliiwezaje kama disc za mgongo zimesogea
 
Sasa kama masaa 24 ya safari yanamchosha hiyo kampeni ya urais 2010 ya miiezi karibu mitatu ataiweza kweli???

Kuna mtu alisema huko nyuma, Shein akae mkao wa kula..................
 
Vipimo afya ya Kikwete vyatolewa hadharani kuwa ana afya njema
brotherjk.jpg
Rais Kikwete, taarifa kuhusu afya yake imethibitika kuwa ni njema, atasafiri kwenda Jamaica mwezi ujao.
broken-heart.jpg
* Kwenda Jamaica Novemba kwa safari ya kikazi

Na Ramadhan Semtawa

RAIS Jakaya Kikwete aliweka hadharani matokeo ya uchunguzi wa vipimo vya afya yake, yanayoonyesha kuwa kiongozi huyo wa nchi ana afya njema baada ya tatizo la kuishiwa nguvu akiwa jukwaani mjini Mwanza Oktoba 4, kuibua mjadala.

Lakini vipimo hivyo vinaonyesha kuwa tatizo pekee linalomsumbua Rais Kikwete ni maumivu ya shingo ambayo yanatokana na kuumia nyakati za ujana au utoto.

Afya ya Rais Kikwete ilizuia mjadala baada ya kuishiwa nguvu akihutubia kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza na kulazimika kubebwa na wasaidizi wake hadi chumba kidogo cha uwanjani hapo na ilielezwa baada ya rais kuzinduka kuwa tatizo hilo lilitokana na uchovu baada ya safari ndefu kati ya New York, Marekani na Dar es salaam na baadaye Arusha na Mwanza.

Pamoja na uchovu huo kuhusishwa na safari ndefu ya Rais Kikwete taarifa iliyopokelewa kutoka Radio Jamaica jana jioni zinasema kuwa rais atakwenda nchini Jamaica kwa ziara ya kikazi itakayoanza Novemba 24 na kumalizika Novemba 26.

Na jana daktari wa rais, Peter Mfisi alirejea tena kauli hiyo akisema uchovu, hasa wa safari, ndio uliosababisha kiongozi huyo wa nchi kuishiwa nguvu jukwaani, huku kukiwa na habari kuwa ataenda Jamaica mwezi ujao kwa safari ya kikazi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ikulu kuweka hadharani vipimo vya uchunguzi wa afya ya Rais Kikwete, ambaye pia aliwahi kuishiwa nguvu siku ya mwisho ya kampeni zilizomuingiza Ikulu, na kuanguka akiwa jukwaani.

Daktari wa rais, Peter Mfisi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa vipimo hivyo ni pamoja na cha damu kwa ajili ya kuangalia virusi vya Ukimwi ambacho huchukuliwa kila baada ya miezi sita.

"Nimekuja kufafanua afya ya mheshimiwa rais kutokana na tukio la Oktoba 4, 2009 (la kuishiwa nguvu jukwaani) pale Mwanza. Tukio hilo limesababisha mshtuko kwa watu wengi na kuendelea kuwa jambo linalozua mjadala kuhusu hali ya afya ya mheshimiwa," alisema daktari huyo.

"Naelewa sababu ya wananchi kuwa na hofu na kuwepo kwa mjadala miongoni mwao. Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia utotoni na wakati wa ujana.

"Baadhi ya pingili za uti wa mgongo sehemu ya shingoni ziliathirika kutokana na kuumia huko na humsababishia maumivu. Mara nyingi matatizo hayo huwapata wanamichezo na wanajeshi."

Dk Mfisi aliongeza kusema: "Tumekuwa tunamfanyia mheshimiwa rais uchunguzi wa damu yake kwa vipimo mbalimbali vinavyotumika kutambua maradhi mbalimbali yanayohusu damu yenyewe na mwili mzima wa mwanadamu. Tumekuwa tunafanya hivyo hapa nchini na hata nje kwa nia ya kulinganisha matokeo yetu na kwa vipimo ambavyo sisi tunavyo.

"Matokeo ya uchunguzi wetu yameonyesha mheshimiwa rais yuko salama, hana maradhi ya damu au kisukari, wala Ukimwi au wingi wa mafuta (Cholestrol), kiwango cha madini, tezi la kibofu wala shingo, au ya ini, au ya homoni mbalimbali zilizoko mwilini na mengine."

Dk Mfisi alifafanua kwamba, uamuzi huo wa kutoa vipimo hivyo umetokana na ridhaa ya rais mwenyewe.

"Ni ridhaa ya mheshimiwa rais mwenyewe... kutokana na kiapo changu cha udaktari na maadili yangu ya kazi, siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake," alisema Dk Mfisi.

Kwa mujibu wa daktari huyo, baada ya Rais Kikwete kuishiwa nguvu jukwaani, alichukua vipimo muhimu wakati akiwa kwenye chumba maalumu uwanjani hapo kama ilivyo kawaida na kwamba vipimo hivyo vimeshafanyiwa uchunguzi.

Alifafanua kwamba matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa siku ya tukio la Mwanza yalionyesha shinikizo la damu (BP) lilikuwa kati ya 130 kwa 85 (vipimo vya kitaalamu), kitu ambacho ni cha kawaida kwa mtu mwenye umri kama wa Rais Kikwete.

"Mapigo ya moyo wake yalikuwa ni 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida; sukari kwenye damu ilikuwa 5.5 ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida; joto la mwili lilikuwa nyuzi 37.5 ambalo ni la kawaida," alifafanua Dk Mfisi.

"Mheshimiwa Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi. Mheshimiwa Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile (la Mwanza)."

Hata hivyo, Dk Mfisi alisema baada ya kurejea Dar es Salaam alijaribu kuwasiliana na madaktari wenzake wa ndani na nje ya nchi ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kuchunguza na kufuatilia afya ya Rais Kikwete.

"Wote hao baada ya kuwasimulia kilichotokea na matokeo ya vipimo nilivyomfanyia mheshimiwa rais, kwa tafakuri zao hawakuwa na wasiwasi wowote kuwa tukio hilo lilisababishwa na jambo jingine lolote isipokuwa uchovu," alisisitiza daktari huyo wa rais.

Aliongeza kwamba mmoja wao alimuona rais siku moja kabla ya kuondoka New York ambako alipata nafasi ya kumchunguza afya ya mkuu huyo wa nchi.

Dk Mfisi, akitoa mtiririko huo wa vipimo mbalimbali na matokeo alisema: " Blood Pressure (shinikizo la damu), tunafuatilia kwa karibu sana msukumo wa damu, mwenyewe tunampa mashine ya kujipima kila siku na anafanya hivyo, kwa jumla presha yake iko kwenye viwango vya kawaida.

"Aidha, uzito wake wa mwili unaendana ipasavyo na urefu wake, mheshimiwa Rais ni mtu mwenye mazoea ya kufanya mazoezi na yuko makini katika chakula anachokula."

Daktari huyo wa rais aliweka bayana kwamba, wanahusika kwa ukamilifu na kuelekeza kuhusu chakula anachokula na kuongeza kwamba "ana nidhamu ya kujipima pamoja na mazoezi na chakula."

Kuhusu moyo, Dk Mfisi alisema tayari walishamfanyia rais vipimo vya kitaalamu vinavyofahamika kama ECHO na ECG na vingine, na kwamba matokeo yameonyesha hakuna tatizo lolote.

Akizungumzia ubongo, alisema mwaka jana Rais Kikwete alifanyiwa uchunguzi wa afya ya ubongo wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutumia kipimo cha CT-Scan na matokeo yake yalionyesha kwamba, hakuwa na tatizo pia.

Dk Mfisi alisema Rais Kikwete aliwahi kufanyiwa uchunguzi wa ini, figo, bandama na kongosho kwa kutumia kipimo cha mionzi (ultra sound), uchunguzi ambao ulibaini viungo vyote hivyo viko salama.

"Kila mwaka tunapomfanyia uchunguzi wa afya ya mheshimiwa rais, tumekuwa tunafanyia uchunguzi wa viungo vyake muhimu vya tumboni kama vile ini, figo, bandama na kongosho na kwa kupima damu yake kwa vipimo vyote muhimu," aliongeza Dk Mfisi.

Kuhusu mfumo wa njia ya chakula, ambayo huhusisha koromeo la chakula, tumbo, utumbo mdogo, Dk Mfisi aliweka bayana kwamba matokeo ya uchunguzi yameonyesha hakuna tatizo lolote.

Alisema mwaka 2007 walimfanyia kipimo cha kitaalamu cha colonoscopy mjini Paris, Ufaransa, kuchunguza hali ya afya ya utumbo mkubwa na kwamba matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa hana matatizo yoyote.

Alisema daktari aliyemfanyia rais kipimo hicho aliwaambia kuwa mkuu huyo wa nchi hahitaji kufanyiwa kipimo kama hicho tena mpaka baada ya miaka saba na kwamba daktari huyo alimtania rais kwa kusema kuwa "angefurahi kuazima utumbo" wake.

Kuhusu tezi la shingo, Dk Mfisi alisema kuwa akiwa mjini New York katika safari yake ya juzi, Rais Kikwete alifanyiwa uchunguzi wa afya ya tezi la shingo pamoja na kiwango chake cha utoaji wa homoni, matokeo yaliyoonyesha hakuna tatizo, hali kadhalika uchunguzi wa tezi la kibofu ulionyesha hana tatizo.

Dk Mfisi alisema rais hana tatizo la macho, masikio na pua na kwamba uvaaji miwani wa Kikwete haumaanishi kuwa ni maradhi. "Tunapofanya uchunguzi wa macho ukiacha ile ya kuchunguza uwezo wa kuona, tunaangalia presha ya macho na hali ya viungo vya nje na ndani, mheshimiwa Rais hana matatizo yoyote," alisema.

SOURCE: MWANANCHI TAREHE 09 OCTOBER,2009


Sina shaka na majibu yavipimo vyake ila kwa madaktari hiyo ni sawa kwa kututangazia majibu hayo. Je kwanini watumie magazeti kufanya hivyo, si itatufanya tuwe na maswali mengi ya kujiuliza. Kinachoshangaza zaidi kutuambia kila baada ya miezi sita wanampima kama ana virusi vya UKIMWI. Why all this
 
[Malaise and brief losses of consciousness after 65 years of age. Clinical diagnosis and value of complementary studies in 512 patients]

[Article in French]


Guillevin L, Sereni D, Girard JF, Galanaud P, Veyssier P, Labram C.
A retrospective study of the diagnosis and causes of malaise and loss of consciousness has been conducted under the aegis of the French National Society of Internal Medicine. This multicentric and retrospective enquiry, which involved 512 patients, revealed that up to 44% of the malaise had no diagnostic label and that those of known aetiology were frequently due to cardiovascular disorders, such as postural hypotension (11.7%) or arrhythmia (9.5%). The study also demonstrated that the clinical enquiry was more important than complementary examinations which yielded few useful data

Dr Mfisi hajaiona hii article, hebu mtumie labda itamsaidia
 
TOO MUCH POLITICS.kwanini kila baada ya miezi sita wampime Virus vya UKIMWI. Depite of this something is wrong kwani hii ni second time
 
hata asafiri masaa mangapi haijalishi.huyu afya yake ina mgogoro and he is not fit to lead the nation.simple

hii post ni ya kibaguzi tu. Ni ubaguzi wa kidhalimu kabisa, yaani mtu hata akiwa kweli na tatizo lolote la kiafya (kama ambayo wengi tunayo) hafai kuongoza kwa kigezo tu cha afya? Kwani huyu boss JK ni kitu gani ama ni kazi gani ameshindwa hadi sasa kutokana na afya yake?
 
is this not dublication of threads?
newspaper release and not press release naona unafananisha jangoo na tandu. Hapa kuna watu wana makengeza sasa huwezi hata kukisia wanatazama ,kusoma na kuandika wapi 😀
 
Halafu tena mwezi ujao anaenda Jamaica, kwanini hizi safari asimpunguzie makamu wake Shein!!! Anasafiri mno huyu mzee!!

mbali na hiyo shughuli ya kikazi inawezekana ameshauriwa kujipatia ka holiday kidogo (alisema hatapinga tena ushauri)...unajua tena akienda beach za kwetu hataweza kujirestisha kwa uhuru kamili...
 
Jamani kuumwa ni kitu cha kawaida kwa binadamu, mbona kelele nyingI? acheni kuwa hivyo, wangapi ambao hawajawahi kuumwa hapa? sometimes muwe reasonable, he is a human being just like any other.
Halaffu kuongoza nchi ambayo system zote zimecollapse kama hii si kazi ndogo jamani, muoneeni huruma mwenzenu, mpeni support na pole badala ya speculation hizi.
Kwa mtu yeyote kwenye position ya kikwete lazima uwe stressed especially because nguvu zinazomzunguka zinamzidi kwenye maamuzi, the guy is confused au kwa ufupi kazidiwa, hawezi kuongoza hii nchi so lazima tu acollapse.

Wewe hujaelewa somo, kwanza hata kama kuumwa ni kitu cha kawaida hutaki rais wako awe mgonjwa, na ukijua rais wako ana ugonjwa wa kuanguka anguka kila mara unaweza kutotaka aendelee urais kipindi kijacho.Ndio maana Kikwete na madaktari wake wanaficha ukweli.

Lakini zaidi ya hilo, kuna swala zima la kutokuwa waadilifu.Hapa ukiacha swala la kuumwa kuna swala la uongo wa wazi unaoletwa na Ikulu ya Kikwete kwa watanzania.Kwa hiyo huyu Kikwete si mgonjwa tu, bali ni mgonjwa na muongo.

Najua wengine mnamuona kama baba yenu na upuuzi mwingine wa figurehead symbol of a nation and all.Wengine hatuambiwi hivyo. Tunataka ukweli tu, hata kama "mungu" anaumwa tutasema tu. Ilmradi ni kweli.
 
Kwani isingetosha kutwambia kwamba afya ya Rais ni nzuri. Daktari ameweka details nyingi ambazo zitaibua maswali kwa nini wameenda mbali mno kuelezea afya ya Rais. Kulikoni? Kuna msemo wa Kihaya unasema hivi: "Banshabile ekanyisibwa nyinayo" Tafisri ni kwamba "mwanamke akibakwa ni yeye wa kwanza kueneza habari ya kubakwa kwake! Akinyamaza hakuna hatakayejua maana mbakaji hawezi kusema.

Shakespeare katika Hamlet, through Queen Getrude alisema

"The lady doth protest too much, methinks."

Similarly

"The doctor doth protest too much, methinks"
 
hii post ni ya kibaguzi tu. Ni ubaguzi wa kidhalimu kabisa, yaani mtu hata akiwa kweli na tatizo lolote la kiafya (kama ambayo wengi tunayo) hafai kuongoza kwa kigezo tu cha afya? Kwani huyu boss JK ni kitu gani ama ni kazi gani ameshindwa hadi sasa kutokana na afya yake?

Kwanza afya ya mtu inaweza kum limit kiutendaji, hivyo katika position nyeti kama urais, afya inaweza kuwa kigezo cha kum disqualify.

Pili hapa kuna issue nyingine tofauti na fya.Kama unakubali JK anaumwa lazima ukubali kwamba Ikulu pamoja na yeye mwenyewe JK ni wadanganyifu.Hatutaki rais mdanganyifu. Maana akitudanganya kwenye afya yake atashindwa vipi kutudanganya kwenye ma Richmond huko?
 
Back
Top Bottom