Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Status
Not open for further replies.
Tatizo letu Tanzania ni ukosefu wa elimu. mitandao ya kijamii kimsingi ni kama vijiwe tu, hakuna kitu kinaongelewa hapa hakiongelewi katika vijiwe vya kahawa utakamata wangapi?
 
Badala waendelee na Mazoezi ya kijeshi wanataka kuhamia Jf haya ngoja tusubili lakini wakumbuke na watu wao wako humu wakilisoma ilo badiko watajua.

Baadhi ya habar hazipaswi kuwa posted. Mtu unakaa unatafuta habari za jeshi na kuzipost humu....Z not good at all
 
Ningependa jwtz,,,waseme na yale mazuri yanayotoka na jf,,mfano jwtz walificha majina ya askari walio uwawa sudan lakini jf tulikuwa nayo na ilitusaidia kupunguza wasisi kwa sisi ambao wazazi wetu wapo huko wakifanya kazi yakurudisha amani iliyopotea,,kwanini wasingekanusha na ilo au kilipongeza jf kwa juudi zakuwaondolea wananchi wasiwasi
 
(Kama yaliyoandikwa ni ya Kweli) basi this is Another none in our Millitary sense.
Hebu mtafuteni huyo Kanali wenu mliyempa kitengo nyeti bila kujua kuwa ni adui halafu baadaye akawatorokeni.
Tumewaungeni mkono kipindi chote shida mlivyokuwa mkituhitaji na sasa mnapanga kusimama kujipima dhidi JF?
JF ni sisi, hivyo mmechagua kusimama dhidi yetu na yenu wenyewe. Habari ni za uhakika sijui shida yenu nini, au jamaa wa kile chama wameona ndiyo muda muafaka wa kuitumia JWTZ kuzorotesha JFkabla ya uchaguzi mkuu?
JF siyo Mtwara, wala siyo M23.

Tumewaunga mkonooooo, sasa vita Kongo inaisha wanatugeuka sio !, POA haina noma.
Ila na sisi tuangalie habari za kupost humu, zile za siri kubwa kwa upande wetu, Tumezee, sio kila taarifa ni habari.
 
Na hiyo tovuti mbona haifanya kazi?usd 12000 zishaliwa tayari,mwee tz bana raha sana ukiwa upo kwenye loop!
 
alafu wanashindwa elewa kua habari siku izi zinapatikana kirahisi kwa mfano kwenye website ya monusco kuna kina kila detail ya operation zinazoendelea hata bbc so hatuitaji habari zao za kupikwa kama wanataka kusiwe na msuguano wawe wanatoa habari sahihi kwani wasipozitoa wao zinapatikana kiurahisi tu kwenye vyanzo vyengine na JF ni sehem ya kupeana habari sahihi sio hapa sio kwenye TBC au magazeti ya uhuru na mzalendo zama izo zimeisha kitambo sana!!!
 
Nahitaji updates za muendelezo wa matukio huko Congo kila siku na sitaki ujanjaunjanja wa kuiedit habari, JWTZ inataka hizo habari wazifanyie Editing ndo watuletee wkt watu tunanunua na kulipishwa ving'amuzi ili kupata habari moto kabla hazijapoa
 
Nilidhani ni Mzee Msekwa na Mukama pekee ndiyo watu wenye nyadhifa katika nchi hii wasiojua jinsi Mitandao ya Kijamii inavyofanya kazi lakini kumbe sikuwa sahihi. Karibu mwezi mzima kabla ya tukio, kulikuwa na tweeter handle JW_TZ ikiripoti taarifa za Jeshi na maendeleo yake kwenye vita dhidi ya M23. Kipindi chote hicho Jeshi lilikuwa kimya likifurahia kutukuzwa kupitia mabandiko ya hiyo handle. Mara tu baada ya kubandika kuhusu kupandishwa kwa hali ya utayari na kufutwa kwa likizo, Jeshi ndo likajitokeza kuyakana mabandiko! Mambo ya chanzo chenye dhamana ndani ya taasisi kukana matokeo ya habari kiliyoitangaza tumeyazoea kwa wanasiasa. Sikutegemea kuyasoma kutoka kwenye chombo nyeti kama Jeshi.

Tangu watu na taasisi waanze kutumia makanusho ya maandiko na matamshi yao wenyewe, mie nimejifunza kuhifadhi kila kinivutiacho!
1170779_10151823911248069_1228467406_n.jpg

Yale yale tunaweza kuyategemee kutokea kwenye handle ya PolisiTz. Tena hii ndo yenye vituko zaidi. Inatumia Picha ya IGP kama Logo!
attachment.php

POLISI TZ.jpg
 
Watu kama nyie ndo mnaiongezea heshima JF tunashukuru kwa kuwabandikia hiyo twit hapo juu waseme sasa kama hiyo akaunti ni yao au sio yao na kama sio yao inakuwaje wanaiachia muda wote huo? na wakuchukuliwa hatua ni mwenye hiyo akaunti sio JF,Jw walinde mipaka ya nchi kazi ya siasa za majitaka wawaachie Nape na Mwigulu
CHUKUA Hii itakusaidia pia..wanasema hawana FB wala TWITER
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.
JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote. Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.
Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/ JWTZ).
Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi. Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.
Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
 
Emu walinde mipaka yetu uko haya mambo ya BLOG wamuachie SAID MWEMA au na wao hawaliamini jeshi la polise.
Said mwema hata panga la dhahabu ofisini kwake wanamuibia ndio itakuwa haya mambo ya digitali?
 
Wadau nawasalimu woote,,
Leo asbh kupitia vpindi vya MAGAZETI redioni zimeskika habari kuwa Jeshi la Wanachi Tz limetangaza mgogoro usiokoma kati yake na mitandao ya kijamii ikiwemo JF kwa kile kibachodaiwa kuwa Wamepakaza habari za uwongo kuwa Likizo zoote kwa Wanajeshi zimefutwa na wanajesh walokuwa likizo kurejeshwa makazini mara moja kufuatia hali ya hatari iliyokuwa imetanda nchini, JWTZ imedai kuwa habari hizo ni za kipotoshaji na uongo mkubwa na serikali haitasita kuwachukulia hayua wahusila.

Anaejua undani wa hili afunguke hapa

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata habari kupitia mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga mbele.
JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote. Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.
Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/ JWTZ).
Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi. Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa siyo za JWTZ.
Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu utoaji wa taarifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
 
Kwani wahamiaji haramu waliojaa Tanzania sio hali ya hatari?
 
[h=1]Makunga, Kibanda wana kesi ya kujibu[/h]
Dar es Salaam. Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Theophil Makunga na wenzake wawili, wamepatikana na kesi ya kujibu katika kesi ya makala ya uchochezi inayowakabili.

Makunga na wenzake Absalom Kibanda na Samson Mwigamba wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima yenye maneno yaliyolenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.

Makala hayo ya Novemba 30, 2012 yaliyokuwa na kichwa cha habari `Waraka maalumu kwa askari wote’ yaliandikwa na mshtakiwa wa kwanza, Mwigamba ambaye ni mwandishi wa makala katika safu yake ya `Kalamu ya Mwigamba’ katika gazeti hilo.
 
CHUKUA Hii itakusaidia pia..wanasema hawana FB wala TWITER
Kaka Ben Mugashe hivi ungekuwa ordinary System Administrator wa JWTZ na ni kweli hii TWITER handle siyo ya Taasisi unayofanyia kazi, kwa elimu ya nafasi yako na kwa nguvu ya kimamlaka ya Taasisi unayoifanyia kazi, unadhani ingekuchukua sekunde ngapi kui-pin hii handle? Kwa nini JWTZ wanalalama tu huku handle ikiendelea kubandika habari zinazowahusu? Hawajui kazi ya TCRA tuwasaidie na kuwaelekeza ofisi zao zilizpo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom