Mazingira ya sakata la dereva wa gari la serikali, landcruiser mkonga, kumtishia dereva wa basi la SATCO mjini Dodoma , liemegubikwa na sintofahamu nyingi.
Ni hivi:
1. Gari hilo ni dark tinted kama kawaida ya magari ya wasiojulikana.
2. Hiyo bastola ambayo inasemekana feki haijulikani kama ilikamatwa hapo hapo.
3. "Kiongozi" aliyebebwa ndani ya gari, ni kibonge mweupe hajatambuliwa
4. Nyuma ya gari, tyre cover ina nembo ya vyombo vya ulinzi na usalama.
5. Inasemekana dereva aliyetishia bastola alimpigia mwenziwe ambaye alikuja eneo la tukio, hatuambiwi aliko tokomea.
6. Polisi wanasema namba ya serikali ilikiwa imefungwa namba plate fake ya gari jingine lakini hawajamtaja huyo mwenye namba feki. Na zaidi ya hapo ilikuwepo namba nyingine ya chombo cha ulinzi na usalama ndani ya gari.
CONCLUSION:
a) Wasiojulikana sasa wanaanza kujitokeza hadharani bila woga.
b) Haiwezekani kabisa dereva wa taasisi ya ujenzi kuwa na munkari wa kutaka kumteka mtu ili ampeleke kusikojulikana. Ni vyombo tu vina uthubutu huo.
C)Kwa nini gari la serikali kwa Taasisi ya kawaida kama TARURA wakawa na gari za tint nzito na kuficha identity zao?
d) Maelezo ya polisi hayakidhi mazingira ya tukio. Maelezo ni kama wanafunika kombe wanaharamu wapite.
Soma Pia:
HITIMISHO
Kwa muda mrefu wananchi wengi wana wasiwasi kuwa kuna genge ndani ya serikali, genge hili linatambuliwa na hata polisi, lakini genge hili hata polisi hawana uwezo kulielezea hadharani.
Na ndio hao wasiojulikana.
Genge hilo ni la wakubwa.