Taarifa ya polisi mlipuko Arusha; Victor Ambros kufikishwa mahakamani

Taarifa ya polisi mlipuko Arusha; Victor Ambros kufikishwa mahakamani

hizo mil 50 amezitoa wapi mpaka agawe kwa m2 atakayemsema mhalifu wakati inafahamika kuwa mwananchi ni polisi jamii na mlinzi wa mwenzake.
Niliona hoja juu ya mishahara ya watumishi serikalini, sasa kakusanya miezi mingapi au atakusanya miezi mingapi ifike 50mil? Mmojawapo huyo jueni anapata kiasi gani!

Wewe nawe sijui unafikiria kwa kutumia nini? hizo pesa zinatoka kwenye mfuko wa jeshi sio mfukoni mwake.
 
Kwa nini wageni hao walikamatwa na kuhusishwa na kadhia hiyo? Serikali iko tayari kuwalipa fidia kwa kuwachafua kwa tuhuma zisizowahusu? Kwa nini walikamatwa wao badala ya wengine waliokuwa eneo la tukio? Watz tuna maswali mengi juu ya jambo hili na tunaelekea kuamini maneno ya Card Pengo

Unaposoma taarifa za serikali usisome kama kitabu cha Willy Gamba. Jifunze kuelewa ujumbe unaotolewea.

Kukusaidia tu ni kwamba raia hawa wameingia nchini kimagumashi. Kwa vile tarehe walizoingia zimeingiliana na tukio hili kumekuwa na ulazima wa kuwascreen kuwa hawahusiki.

Hawajaachiwa huru. Jeshi la polisi halijasema kuwa wameingia nchini kimagumashi, ila limesema kuwa wamekabidhiwa kwa mamlaka husika juu ya jinsi walivyoingia nchini.

Mara nyingi wafanyabiashara huingia nchini na visa za kitalii. Jambo ambalo ni kinyume cha kisheria.
 
Huyo Victor wamemuonea tu!kama wamekosa watu wa kuwashika,wangesema upepelezi unaendelea,huyo Ambrose hana kosa!kumpa kesi mauaji ni kumuonea!
mtaje ni nani sasa anahusika, mil.50 hiyo hapo.
 
Kwa maelezo hayo ya Jeshi la Polisi, bado sijaona kama huyo Victor ndiye mshukiwa nambari moja.
Jeshi la Polisi lieleze kwa undani namna bomu hilo linavyohusishwa na huyo bwana mdogo, sio kutueleza tu kuwa lilirushwa.
Ni jambo gani lililowashawishi hata kuamini kweli mtu huyo ndiye mhusika mkuu.
Ni nini motive ya yeye kufanya hivyo?
Kwa nini iwe ni kwa kanisa katoliki?
 
kazi kwelikweli...............................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!??????????????
 
Nimepitia taarifa sijaelewa kisa cha Ambros kufikishwa mahakamani, hebu waliohudhuria mtupashe taarifa zaidi. Huyo kijana wameeleza ni mwendasha boda boda, Je yeye alikuwa na bomu na kulirusha au kosa lake ni nini? Au walikuwa na nia moja na mrusha bomu?.
 
nafasi ni yako sasa kumtaja mtuhumiwa kuna mil 50 zinakungoja mkuu
sidhani kama ambrose anajua chochote maana yeye inadaiwa kampeleka mteja mahali alipoelekezwa na mteja,so si rahisi kumjua mteja aliyembeba,nadhani mashahidi wapo waliomwona ambrose akimbeba ??mtuhumiwa aliyechapa mwendo baada ya tukio sababu tukio lilitokea mchana,ambros anatakiwa apate mawakili akina tundu lisu,abdhala safari ili wamtetee apate haki yake,chadema si lazima wawatetee wanachama wao tuu pia na hata raia kama huyo tena yatima,nafikiri hili litawajenga zaidi kisiasa
 
MAJINA YA WATUHUMIWA WALIOACHIWA HURU PAMOJA NA RIPOTI YA POLISI KUHUSU BOMU LA ARUSHA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013


Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.

Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)

Raia hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa Tanzania wenye asili ya Yemen. Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo.

Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.

Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.

Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.

viongozi wote walisema kua ule ulikua ni ugaidi. Mbona huyo mtuhumiwa hakushitakiwa kwa kosa la ugaidi?. Au kwa sababu si muislamu.
 
Back
Top Bottom