- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Kumekuwa na Taarifa kwa umma ya kuanzia Tarehe 23 mwezi wa pili ikiwa na utambulisho wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa ikiwataka watu wanaotaka kubadili majina wawasiliane na namba zilizowekwa.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa Taarifa hiyo haijatolewa wala kuchapiswa katika kurasa rasmi za mitandao ya na OWM-TAMISEMI kama inavyodaiwa, hivyo ina lengo la kufanya ulaghai.
Taarifa hiyo licha ya kuwa haijatolewa na TAMISEMI lakini pia ina baadhi ya mapungufu ikiwemo makosa ya kiuandishi mathalani rejelea maneno kama "taarifaau", "chagbamoto", "sekodnari", "kuwatangazi"
Mbali na hayo Taarifa hiyo imetumia mawasiliano binafsi na si namba za ofisi, pia inawataka watu wawasiliane kupitia Whatsapp.