Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi

Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu (THBUB): Mauaji ya Mwangosi

Wakuu, nimeipenda taarifa hii ya THBUB. Imechukua siku chache na watu wachache (naamini haikutumia gharama kubwa).
Imefafanua kila kitu kwa marejeo ya sheria mama na mikataba ya kimataifa ambayo TZ imeridhia.
Imeandaliwa kisomi na si kama riwaya ya ile kamati ya Mhe. Waziri.

Kwa kweli nawapongeza, ni kazi ya serikali sasa kuifanyia kazi kama kweli inajali.
 
Hii ni ripoti ya akili hata kwa ufupisho wake. Kwani imejibu maswali ya msingi ambayo Ripoti ya Uchimvi imeshindwa hata kugusia. Kinachoshangaza ni kuwa wote waliangalia kitu kile kile!!!

Mzee tofauti ni mtazamo na lengo la kuandaa report. Hawa wameiandaa katika mtazamo wa "haki za binadamu na (angalau) usawa meble ya sheria". Wale wengine ni watawala. Ila katika yote kinachonishangaza bado ni hao kina Makunga na Mtambalike kushiriki kuleta upuuzi huo!
 
Hii sasa ndio angalau unaweza kuita report sio ule uchafu wa Nchimbi.ila tutafika tu.....
 
kweli uwongo na ukweli ni kama maji na mafuta,huwezi kuchakachua ukweli wakati wote.DrNchimbi na wenzio mneona eeeeeh?
 
Ritz naona umekuwa unatoa maoni kwa kutumia mawazo ya mtu anayetafakari. Nakugongea senks sasa

Tundu Lissu alishawaambia kuwa hizi tume hazina manufaa. la muhimu ilikuwa kuunda tume huru yenye kuunganisha kada zote
 
Inawezekana kabisa Raisi wa Nchi hii akawa hata hajui kama mauaji ya Mwangosi yalitokea nchini kwake na yalifanywa na vijana wake kwa amri yake akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi a ulinzi na usalama.

Ngoja kwanza aende kuzima mwenge labda atachukua hatua hata kama hazitakuwa na manufaa tena kwa taifa
 
Report ya Ihemi haina uchambuzi halafu imejaa maneno hollow kama amani, utulivu, amri halali, utii wa sheria bila shuruti, maadili, utawala wa sheria, elimu ya uraia n.k. Halafu yeye alikuwa ansikiliza wakina Mukama (magamba) kisha anatoa mapendekezo ya Mukama kama ndo mapendekezo ya kamati. Anashauri eti baada ya uchaguzi ipitishwe sheria kusiwe na shughuli za kisiasa nje ya bunge. Anachekesha kweli tena amekuwa kioja. Maana yake huyu mh. wala hajui siasa ni nini. Hiyo sheria inalenga M4C shame upon him. Anadai eti watu wanashindwa kufanya kazi za maendeleo sababu ya siasa. Mbona yeye ameenda Iringa kufanya siasa badala ya kuchunguza kifo cha Mwangosi? Ahaa ahaa ahaa huyu mh. ananikumbusha wakati Mrema yupo kwenye chati kila siku anabebwa. Magamba wakapendekeza itungwe sheria kuzuia watu kubebwa. Mwalimu aliwashushua kwa kuwaambia kama kuna apendaye kubebwa na wabebaji wapo, nyie chawawasha nini. Waacheni wabebane kwani hamna sheria iliyovunjwa. Sijui walijisikiaje, na wamesahau ndio maana hiyo sheria ya Ihemi itaenda bungeni haraka sana.
 
Ukweli upo palepale Amri ya kuua alitoa Kamuhanda, alipewa maagizo toka kwa Nchimbi,Nchimbi alipewa maagizo toka kwa CCM. Je kesi ya Mbuzi hakimu Fisi haki itatendeka
 
Ukweli upo palepale Amri ya kuua alitoa Kamuhanda, alipewa maagizo toka kwa Nchimbi,Nchimbi alipewa maagizo toka kwa CCM. Je kesi ya Mbuzi hakimu Fisi haki itatendeka

Uwezekano wa wauaji wote kuanzia kwa wale askari wengine sita pamoja na rpc kamuhanda na igp mwema kushitakiwa ni kama haupo kwa sasa lakini kwa taarifa hii watanzania wameweza kuujua ukweli.
Tangu awali jeshi la polisi pamoja na wizara ya mambo ya ndani walikuwa wamejiandaa kuuhadaa umma na kuupotosha lakini sasa ukweli umebainika na wauaji wamefahamika.

Lakini pia hii ripoti itabaki kwenye kumbukumbu huko mbeleni tukipata serikali makini wauaji wote watatendewa haki yao kadri ya ushiriki wao katika mauaji ya Mwangosi.
 
Back
Top Bottom