Report ya Ihemi haina uchambuzi halafu imejaa maneno hollow kama amani, utulivu, amri halali, utii wa sheria bila shuruti, maadili, utawala wa sheria, elimu ya uraia n.k. Halafu yeye alikuwa ansikiliza wakina Mukama (magamba) kisha anatoa mapendekezo ya Mukama kama ndo mapendekezo ya kamati. Anashauri eti baada ya uchaguzi ipitishwe sheria kusiwe na shughuli za kisiasa nje ya bunge. Anachekesha kweli tena amekuwa kioja. Maana yake huyu mh. wala hajui siasa ni nini. Hiyo sheria inalenga M4C shame upon him. Anadai eti watu wanashindwa kufanya kazi za maendeleo sababu ya siasa. Mbona yeye ameenda Iringa kufanya siasa badala ya kuchunguza kifo cha Mwangosi? Ahaa ahaa ahaa huyu mh. ananikumbusha wakati Mrema yupo kwenye chati kila siku anabebwa. Magamba wakapendekeza itungwe sheria kuzuia watu kubebwa. Mwalimu aliwashushua kwa kuwaambia kama kuna apendaye kubebwa na wabebaji wapo, nyie chawawasha nini. Waacheni wabebane kwani hamna sheria iliyovunjwa. Sijui walijisikiaje, na wamesahau ndio maana hiyo sheria ya Ihemi itaenda bungeni haraka sana.