Taarifa ya utekelezaji miradi ya maendeleo kupitia fedha ya kuchochea maendeleo ya jimbo la Bukoba Mjini

Taarifa ya utekelezaji miradi ya maendeleo kupitia fedha ya kuchochea maendeleo ya jimbo la Bukoba Mjini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kuelekea kumaliza kipindi chake cha utumishi katika jimbo la Bukoba mjini na katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. WILFRED M. LWAKATARE (Mb) na Waziri kivuri wa wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi anayo furaha kuwashirikisha mafanikio makubwa ya usimamizi wake juu ya matumizi bora ya fedha za mfuko wa jimbo la Bukoba mjini ambayo yamepelekea kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo, mikubwa na midogo ndani ya jimbo la Bukoba mjini kwenye kata zake zote 14.

Mh. Lwakatare kupitia ofisi yake ya Mbunge atatoa taarifa ya kila mwaka wa fedha kuanzia 2015/2016 mpaka 2019/2020 na kisha kutoa taarifa ya jumla ya miaka yote mitano.

Kwa pamoja tuijenge Bukoba yetu kwa kila mmoja wetu kuwajibika kikamilifu katika eneo lake.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO KUPITIA FEDHA YA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO LA BUKOBA MJINI

Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ilipata kiasi cha Tsh. 30,294,000/= ikiwa ni fedha ya kuchochea miradi ya maendeleo katika jimbo la Bukoba mjini.Kulingana na utaratibu na mwongozo wa matumizi wa fedha hizi kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo ndiyo inayopitisha na kugawa fedha hizi kulingana na uhitaji ulioibuliwa kutoka katika kata, taasisi na vikundi mbalimbali vya kijasiliamali.

Kamati ilipita katika kata zote za Halmashauri ya Manispaa na kupata mahitaji ya kila kata kama yalivyoainishwa hapa chini;

KATA YA BAKOBA

Katika kata ya Bakoba; upo mtaa ambao haukuwa na huduma ya barabara kwa muda mrefu japo kuna wananchi wanaoishi. Kukosekana kwa barabara katika eneo husika kulisababisha changamoto nyingi kwa jamii ya watu waishio pale; mfano:-
  • Eneo si rafiki kabisa kwa huduma muhimu kama usafiri.
  • Wakazi wa eneo husika wanapata changamoto kubwa pale kunapotokeadharula mfano:- Wagonjwa mahututi na Mama wajawazito
  • Hapa; wananchi wanalazimika kutumia usafiri wa mitumbwi mpaka maeneo ya kastam mwaloni; Eneo ambalo kunapatikana usafiri wa magari na Boda boda. Jambo ambalo linakuwa ni mzunguko mrefu ukilinganisha na hali halisi
1587972241000.png

Mhe. Diwani wa kata kwa kushirikiana na wananchi wakiwa katika harakati za upasuaji wa miamba na mawe kwa ajili ya kufungua baraba ya Kalobera.


Hivyo ilimlazimu Mh. Diwani pamoja na wakazi wa mtaa husika kufanya jitihada za makusudi kuanzisha barabara yenye urefu wa takribani Kilometa 3.Eneo linaloandaliwa kwa barabara lilikuwa limejaa miamba mingi sana, Ambayo ilikuwa ni lazima iondolewe kwanza kabla ya kuendelea na zoezi la kutengeneza barabara hiyo.

Ili kufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi; Mh. Diwani wa kata husika aliomba vifaa vifuatavyo:-

v Nyundo za Kupiga Mawe za Kg.2Idadi:
15​
v Nyundo za Kupiga Mawe za Kg.3Idadi:
10​
v SululuIdadi:
02​
v KoleoIdadi:
05​
v Tape MeasureIdadi:
02​
v TororiIdadi:
02​
v TindoIdadi:
10​
v MitalimboIdadi: 04

Kupitia kamati ya mfuko wa jimbo kata ya Bakoba iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. 787,000/= kwa ajili ya kufanya manunuzi ya vifaa na kuhakikisha mawe na miamba vinapasuliwa na kuifanya barabara hiyo kuweza kupitika na ununuzi wa madawati. Jumla ya fedha zilizoelekezwa kata Bakoba zilikuwa ni Tshs. 787,000/= kiasi cha fedha Tshs. 200,000/= kilielekezwa katika utengenezaji wa madawati na Tsh. 587,000/= kununua vifaa vya kupasulia miamba.
1587972463771.png

M/kiti wa kamati ya mfuko wa jimbo Mh. Wilfred M. Lwakatare (MB) pamoja na Mstahiki Meya wakionyesha mfano katika zoezi la kupasua mawe kupisha barabara
1587972516505.png

Mh. diwani kata Bakoba, M/kiti wa mtaa, wajumbe wa kamati ya mfuko wa jimbo wakiongozana na M/kiti wa kamati hiyo Mh. W.M.Lwakatare (MB) kukagua eneo la barabara lililokamilika
1587972557195.png

Eneo kubwa la barabara limekwisha anza kuruhusu magari kuingia na kutoka hasa yale yanayokwenda kuchukua mawe na kokoto hivyo hata huduma za usafili wa umma zimekwisha anza.
II.KATA YA IJUGANYONDO

Kumalizia ujenzi wa Jengo la chumba cha darasa la awali.

Mradi huu ulianza mwaka 2013/2014 kwa ufadhili wa fedha za LGCDG toka Serikali kuu, fedha iliyopokelewa ilikuwa ni sh.14,573,000/= ambayo haikukidhi kukamilisha ujenzi wa jengo hilo na miaka iliyofuata Halmashauri haikupata fedha za LGCDG hivyo kubaki na kiporo cha ukamilishaji wa mradi huu wa chumba cha darasa la awali katika kata ya Ijuganyondo.kazi zilizozosalia ni kama:
Kuweka vioo katika madirisha

Kuweka “ceiling board”

Kujenga vyoo (Matundu-04) kwa ajili ya wanafunzi na mwalimu

Kupitia kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo kata ya Ijuganyondo iliidhinishiwa kiasi cha Tsh. 1,200,000/= Kiasi cha tshs. 858,500/= kilitumika kwa ajili ya kumalizia uwekaji wa vioo, ceiling board pamoja na kuanzisha ujenzi wa matundu manne ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu. kiasi cha fedha tshs. 200,000/= kilielekezwa katika matengenezo ya madawati kama ilivyokuwa kwa kata zingine zilizopata ufadhili wa mfuko wa jimbo. Baada ya matumizi ya awali kiasi cha fedha ths. 141,500/= kilisalia na kimepangwa kuanzisha ujenzi wa matundu ya choo kwa ajili wanafunzi na walimu katika shule hiyo ya awali.
1587972613816.png

Wajumbe wakilikagua ukamilishaji ujenzi wa chumba cha darasa la awali lililokamilishwa na fedha ya mfuko wa maendeleo ya jimbo.
1587972656435.png

Wajumbe wakilikagua eneo yatakapojengwa matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu, wakipokea pia maelezo toka kwa mwakilishi wa wenyeji wa eneo hilo.

III.KATA YA KIBETA


Kumalizia ujenzi wa Vyumba Viwili (2) vya Madarasa Kibeta sekondari

Mradi huu ulianza kwa juhudi za wananchi wa kata ya Kibeta, wazazi wa wanafunzi wanaosomea hapo, na mapato yatokanayo na miradi/ kodi ya pango katika vibanda vinavyomilikiwa na ofisi ya mtendaji wa kata.Michango yote ilifanikisha ukamilishaji wa ujenzi wa msingi wa vyumba viwili vya madarasa.Kata inahitaji uwezesho wa kuinua /kujenga kuta.

Kupitia mfuko wa kuchochea maendeleo katika jimbo, uongozi wa kata kibeta ulipokea kiasi cha fedha taslimu tshs. 3,180,000/=

Ambapo kiasi cha tshs. 200,000/= kilitumika kununulia madawati yaliyokuwa yakihitajika katika shule ya msingi kibeta na shule ya sekondari ya kibeta hivyo kusaidia kuondoa tatizo la madawati lililokuwa likizikabili shule hizo.

Kiasi cha tshs. 2,980,000/= zilitumika kuinua vyumba viwili vya madarasa vilivyopo katika shule ya sekondari ya kibeta.
1587972717866.png

Wajumbe wa mfuko wa jimbo walipokuwa wakiwasili katika shule ya sekondari ya Kibeta wakiongozana na m/kiti wa kamati Mh. Wilfred Lwakatare (MB) kukagua maendeleo ya miradi iliyofadhiliwa na mfuko wa jimbo
1587972748088.png

Wajumbe wakipokea ripoti ya utekelezaji ndani ya chumba kimojawapo cha darasa kilichochengwa kwa ufadhili wa mfuko wa jimbo
1587972781940.png

Mwonekano wa vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kwa ufadhili wa mfuko wa jimbo katika shule ya sekondari ya kibeta

NB:
Kata kibeta iliomba kuongezewa kiasi cha pesa tshs. 5,600,000/= kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa.
1587972814737.png

Wajumbe wakiongozana na viongozi wa kata Kibeta pamoja na wenyeji wao uongozi wa shule ya sekondari ya Kibeta kuwasalimia wanafunzi waliokalia madawati yaliyotengenezwa kwa ufadhili wa fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo.
IV. KATA YA RWAMISHENYE

Kamati ya maendeleo ya kata ya Rwamishenye iliomba kukarabatiwa vyumba 4 vya madarasa na kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu.Miradi inayopaswa kukamilishwa ni pamoja na:-

Kumalizia ujenzi wa nyumba ya mwalimu

Kufanya ukarabati katika vyumba (4) vya madarasa.

Kuezua na kuweka mabati mapya kwa madarasa mawili (2) yanayovuja.

Kupiga sakafu kwa upya katika madarasa manne (4).

Uongozi wa kata Rwamishenye ulipokea fedha taslimu tshs. 874,375/= kwa malengo ya kutekeleza ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Rwamishenye, paa lililokuwa linavuja na sakafu iliyoharibika kutokana na kujengwa kwa kiwango duni pamoja na ununuzi wa madawati.

Mpaka kamati ya mfuko wa jimbo inafika shuleni hapo kukagua utekelezaji wa matumizi ya fedha zilizoombwa hakuna utekelezaji wa shughuli yoyote uliokuwa umefanyika jambo ambalo lilimlazimu m/kiti wa mfuko wa jimbo Mh. Wilfred Lwakatare (MB) kutumia “theory” yake ya usimamizi lazimishi kwa kumuagiza mhandisi wa Halmashauri kusimamia utekelezaji wa ukarabati wa vyumba hivyo vya madarasa haraka sana iwezekanavyo, na shughuli hiyo ilikamilika ndani ya siku kadhaa.

Pia m/kiti huyo wa kamati alishauri uongozi wa kata na shule kushilikiana kumtafuta mkandarasi aliyejenga vyumba hivyo vya madarasa katika kiwango kibovu ili kueleza kwa nini alijenga kwa kiwango duni.
1587972884733.png

Sakafu ambayo ilifanyiwa marekebisho na baadaye kupatwa na nyufa kutokana na tetemeko la ardhi.
1587972916819.png

Kama inavyoonekana kwa ndani na nje ya vyumba vya madarasa ambavyo paa zake zilifanyiwa ukarabati kwa kuweka mabati mapya ili kuzuia kuvuja wakati wa mvua

IV. KATA YA BUHEMBE


Kamati ya maendeleo ya kata ya Buhembe iliomba ufadhili wa kukamilishiwa ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya msingi Kashenge. Kutokana na uwepo waradi huu kama kiporo kwa muda mrefu na adhma ya serikali ya kuboresha miundombinu na mazingira bora ya kujifunzia.Baada yakupitia maombi haya kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo iliidhinisha kiasi cha Tsh. 2,200,000/= ambapo kiasi cha tsh. 2,000,000/= kilielekezwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa chumba cha darasa s/m Kashenge na kiasi cha Tsh. 200,000/= kwa ajili ya kununua madawati ikiwa ni mchango wa mh.Mbunge katika kuchangia ununuzi wa madawati katika shule zote zilizopo katika jimbo la Bukoba Mjini.
1587972943374.png

Wajumbe wa kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo wakiwasili Eneo la s/m Kashenge
1587972976761.png

Wajumbe wakielekea kukagua ukamilishaji wa vyumba vya madarasa s/m Kashenge
1587973005193.png

Wajumbe wa kamati wakikagua kazi zilizofanyika katika ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa s/m Kashenge10

VI. KATA YA HAMUGEMBE

Kamati ya maendeleo ya kata ya Hamugembe iliomba kuwezeshwa kukamilisha ujenzi wa chumba cha darasa katika shule ya Hamugembe sekondari.Kamati ya mfuko wa maendeleo ya jimbo iliidhinisha kiasi cha Tsh. 1,762,500/= ambapo kiasi cha tsh. 1,562,500/= kwa ajili ya ukamilishaji wa chumba cha darasa kwa kununua vifaa vya kuezekea na kiasi cha tsh. 200,000/= kwa ajili ya ununuzi wa madawati.
1587973166364.png

Mwonekano wa chumba cha darasa Hamugembe sekondari ambacho kabla ya kuezekwa kilikumbwa na adha ya tetemeko la ardhi na kupelekea kubomoka upande mmoja hivyo vifaa vya uezekaji bado vimetunzwa kwenye stoo ya shule

VII. KATA YA KASHAI


Kamati ya maendeleo ya kata ya Kashai iliiomba kupitishiwa mradi wa ufunguzi wa barabara ya kilimahewa – Mtakuja kwani barabara hiyo haipitiki hadi mtakuja na kuleta adha ya usafiri panapotokea dhalura hata usafirishaji wa vifaa vya ujenzi kwa wakazi wa Mtakuja inawalazimu kusomba kwa pikipiki au kubeba kwa kichwa.

Kamati iliiridhia na kupitisha kiasi cha Tsh. 5,690,000/= kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe.
1587973246267.png

Mh.Diwani wa kata ya Kashai akikagua matengenezo ya barabara ya Kilimahewa-Mtakuja

VIII. KATA YA NYANGA


Kamati ya maendeleo ya Nyanga iliomba kufadhiliwa mradi wa matengenezo ya madawati katika shule ya msingi Kyakailabwa, kutokana kuwa na upungufu mkubwa wa madawati. Kamati iliidhinisha kiasi cha Tsh 2,000,000/= kwa ajili ya matengenezo ya madawati 40.
1587973275546.png

Matengenezo ya madawati 40 kwa ajili ya shule ya msingi Kyakailabwa- kata ya Nyanga
1587973371303.png

Wajumbe wa kamati ya Mfuko wa jimbo wakikagua madawati yaliyotengenezwa kwa ajili ya s/m Kyakailabwa

MUHT. WA MIRADI ILIYOPANGIWA FEDHA NAKUTEKELEZWA KWA FEDHA ZA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO 2015/2016



NAJINA LA MRADIMAHALI ULIPO/
GHARAMA
KATA
1.Kuchangia ununuzi waKATA ZOTE 14
2,800,000.00
madawati kata zote 14 za
Manispaa
2.Ununuzi wa madawati 40 s/mNSHAMBYA
2,000,000.00
Nshambya

3.Ununuzi wa madawati 40 s/mNYANGA
2,000,000.00
Kyakailabwa Nyanga
4.Matengenezo ya barabara yaKAHORORO
1,000,000.00
Makongo – Ntoro
5.Matengenezo ya barabara yaKASHAI
5,690,000.00
Kilimahewa -Mtakuja
6.Matengenezo ya daraja kashaiKASHAI
500,000.00
- matopeni
7.Kununua vifaa vya shule kwaKASHAI
500,000.00
wanafunzi wanaolelewa na
kituo cha NUSURU YATIMA -
Kashai
8.Matengenezo ya barabara yaKAGONDO
800,000.00
mtaa wa Kagondo - Kyamzinga
9.Ukarabati wa vyumba vyaRWAMISHENYE
674,375.00
madarasa kwa kutengeneza
sakafu na paa linalovuja
10.Kulipia gharama za ufundiRWAMISHENYE
100,000.00
11.Ununuzi wa vifaa vya kufanyiaBAKOBA
400,000.00
usafi- Bukoba Tuinuane Saccos
(BUTUWOSA
14​

12.
Ununuzi waBAKOBA
587,000.00
nyundo,makoleo,mitalimbo,futi
kamba, tolori na tindo
13.
Matengenezo ya kifyatuliaBAKOBA
150,000.00
kalvati
14.
Ukamilishaji wa chumba chaIJUGANYONDO
1,000,000.00
darasa la chekchea kwa
kuweka vioo,kupaka rangi
ubao wa scatting
15.
Ukamilishaji wa chumbaBUHEMBE
2,000,000.00
kimoja cha darasa kwa kupaka
rangi na kurekebisha madirisha
katika shule ya msingi
Kashenge
16.
Gharama za ukaguzi wa miradiBMC HQ na Kata
4,550,125.00
na vikao vya kamatizote
JUMLA KUU:
30,294,000.00

https://www.jamiiforums.com/data/attachment-files/2020/04/2381314_bukoba.pdf
 

Attachments

Muda umeisha bwana, kuna siti yako taari uraiani
 
Back
Top Bottom