Ahsante Sana. Kuna mwongozo umeandaliwa na BASATA utazinduliwa hivi karibuni, ngoja tushirikiane nao kuutangaza Sana kisha kama kuna vitu vinapungua, maoni haya ya jamii yatakuwa muhimu sana kwenye kuja na revised version
BASATA ivuliwe mamlaka ya kudhibiti na kuwaongoza wasanii, wabaki kuwa wasajili na wasimamizi wa wasanii na kazi zao za Sanaa.
Wamethibitisha zaidi ya miaka 10 kwamba hawana meno ya kung’ata inapostahiki na pia wamechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili kwa kuendelea kufumbia macho maudhui ya kingono yaliyopo katika miziki karibu yote ya wasanii wa Tanzania.
Mambo ya maudhui katika nyimbo na Sanaa za wasanii yawe regulated na Wizara yako kwa maana ndio inasimamia Ustawi imara wa jamii na maadili yake.
BASATA is incompetent and Politically compromised.
Hawatoshi na Hawafai.
Serikali pia iangalie uwezekano wa Wizara ya Utamaduni kujitegemea ili kulinda Mila, Tamaduni na Desturi zetu watanzania kwa mujibu wa makabila yetu. Hii itasaidia kuokoa maadili yetu Kama taifa.
Wizara ya Sanaa na Michezo pia inastahili kujitegemea.
Ni ushirikiano wa hizi wizara ;
1) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi maalum.
2) Wizara ya Tamaduni, Mila na Desturi
3) Wizara ya Sanaa na Michezo
Ndio utasaidia kuongoza, kusimamia, kuimalisha na kulinda maadili ya Tanzania na watanzania.
Utandawazi na kukua kwa technology kunaweza kupoteza asili ya taifa lolote lisilo makini na ulinzi wa asili yake na watu wake.
Tamaduni zetu, Mila zetu, Desturi zetu ndizo alama na vitambulisho vyetu kwenye ardhi ya dunia hii na maadili ya jamii na taifa letu yanalindwa na vitu hivi.