Taarifa za Ikulu kwa lugha ya Kiingereza za nini wakati sisi ni Waswahili asilia?

Sisi ni wahitaji ndio maana atuishi kwenda kwao hivyo ni lazima tuchuchumae wakati mwingine!! Umewahi kuisikia huu usemi :' MUHITAJI HANITHI INGAWA NI LIJARI?"
Haina maana. US au beberu yeyote hawezi kusoma habari zenu feki feki. Habari za swrikali haziaminiki kabisa.

Mabeberu wakitaka kitu wanajua pa kukipata. Hawawezi kuamini habari zenu zilizofikia kiwango cha kwenda against common sense zinazodai mmeitokomeza korona kwa maombi.

Eti Mungu awasikilize wadhambi wanaomkejeli kila siku? Duh.
 
Haina maana. US au beberu yeyote hawezi kusoma habari zenu feki feki. Habari za swrikali haziaminiki kabisa
Sio Kweli! Serikali ya Marekani wizara ya Mambo ya nJe ina kitengo kinachoshuhurika na Afrika ikiwemo Tanzania hivyo ni jukumu lao kujua kila kitu kinachoendeleA ILI WAWEZE KUYAWEKA MAMBO YAO SAWA!!! Kwavile hao wamarekani wanakijua KISWAHILI huweza kusoma lugha zote mbili!!
 
Corona gani Tena jamani mbona watu tulishaanza hata kuisahau
 
Hakuna serikali duniani iliyo na mpango wowote na wanyonge.
Hapa kwetu wanaojua kiingereza sio wanyonge na hiyo ndio targeted group. Mnyonge taarifa za ikulu anazitakia nini? Kama ni teuzi hasimhusu.
Serikali iko kwa ajili ya middle na the well to do.
Hata ukienda Kenya wanyonge wanakaa sehemu Kama kibera kusiko kua na huduma za maji, barabara, umeme, usafiri, n.k
Angalia machinga wanavyofurushwa Zambia.
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeibuka na mfumo mpya wa kujulisha umma Serikali inayoyafanya kwa njia ya Kiingereza. Hii imeminya umma usiojua Kiingereza kutojua yanayoendelea nchini

Tabia kama hii naona ni bora Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Zuhura Yunus atambue kuwa kwa sasa hayupo Uingereza ni muhimu sana taarifa aziandike kwa Kiswahili kwani itasaidia umma wote kufahamu yanayoendelea nchini.

Zuhura tunaomba ufahamu sisi ni Watanzania na lugha yetu ni Kiswahili ; lugha unayotumia kutupasha habari za Ikulu ni mwiba kwa walio wengi hapa nchini

Tunaomba ubadilike na kama unaona ni muhimu kuandika lugha hiyo basi tuandikie na lugha yetu ya kiswahili.

View attachment 2120348
Dina kantri wanamasharti kama waganga wakienyeji
 
Lugha ngeni za nini nyumbani. Kwani tunayoyafanya lazima mabeberu kuwajulisha kuwa tumefanya haya.! Asilimia 99% ya watanzania wengi wao hiongea kiswahili kama lugha ya taifa, na umoja wa afrika wamepitisha lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano, tupende vyakwetu tusiwatukuze ngozi nyeupe kila kitu.
 
Samahani, wewe ni CHIZI
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeibuka na mfumo mpya wa kujulisha umma Serikali inayoyafanya kwa njia ya Kiingereza. Hii imeminya umma usiojua Kiingereza kutojua yanayoendelea nchini

Tabia kama hii naona ni bora Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Zuhura Yunus atambue kuwa kwa sasa hayupo Uingereza ni muhimu sana taarifa aziandike kwa Kiswahili kwani itasaidia umma wote kufahamu yanayoendelea nchini.

Zuhura tunaomba ufahamu sisi ni Watanzania na lugha yetu ni Kiswahili ; lugha unayotumia kutupasha habari za Ikulu ni mwiba kwa walio wengi hapa nchini

Tunaomba ubadilike na kama unaona ni muhimu kuandika lugha hiyo basi tuandikie na lugha yetu ya kiswahili.

View attachment 2120348

Tatizo langu mimi ni hilo tangazo utafikiri gazeti la mzalendo limefufuka?
 
Basi tufanye hivi;

Nasisi tusiojua kusoma tuwekewe audio.

Mtanzania mwingine alisikika akilalamika kutokea viti vya nyuma.
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeibuka na mfumo mpya wa kujulisha umma Serikali inayoyafanya kwa njia ya Kiingereza. Hii imeminya umma usiojua Kiingereza kutojua yanayoendelea nchini

Tabia kama hii naona ni bora Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Zuhura Yunus atambue kuwa kwa sasa hayupo Uingereza ni muhimu sana taarifa aziandike kwa Kiswahili kwani itasaidia umma wote kufahamu yanayoendelea nchini.

Zuhura tunaomba ufahamu sisi ni Watanzania na lugha yetu ni Kiswahili ; lugha unayotumia kutupasha habari za Ikulu ni mwiba kwa walio wengi hapa nchini

Tunaomba ubadilike na kama unaona ni muhimu kuandika lugha hiyo basi tuandikie na lugha yetu ya kiswahili.

View attachment 2120348
Wewe ni jinga kabisa.Kwani hujui kwamba Lugha rasmi za kazi Tzn ni Kiswahili na kingereza?

Ofisi za umma zinatumia lugha gani? Kuwa kwako msawahili ndio tumesema uwe mbumbumbu wa kingereza?

Mwanaume mzima unakuwa na nongwa,hapo katoa taarifa kwa lugha zote je ingekuwa kingereza tuu ungefanyaje? Hovyo kabisa wewe mtoa mada.
 
Back
Top Bottom