Taarifa za usajili wa dirisha dogo kwa timu za ligi kuu ya NBC

Naona picha ya Shiboub akiwa na uzi wa Simba. Sitaki kuamini kuwa viongozi na benchi la ufundi la Simba wamekosa weledi kiasi hicho kiasi cha kumrudisha Shiboub. Wakisema kama wamemleta tu kama mchezaji mwalikwa ili kuchangamsha timu kwenye Mapinduzi Cup nitawaelewa. Hivi huyu Shiboub ambaye alikuwa anakata upepo kuanzia dakika ya 40 jumlisha umri halafu wamrudishe tena Simba? Labda kama anakuja bure Simba na Simba hawana pesa ya usajili hapo itakuwa sawa.

Kuliko Simba imsajili Shiboub ni bora mara 100 wamsajili Moses Phiri au Emanuel Okwi lakini sio huyu jamaa. Na kila siku viongozi wa Simba wanaambiwa hapa jamvini toka dirisha kubwa la usajili kuwa shida ya Simba sio kiungo ni mshambuliaji namba tisa (9). Washambuliaji waliopo sasa wote walikuwa wanafichiwa madhaifu yao na Chama na Luis kwa kufunga magoli wao wenyewe na pia kuwapa washambuliaji pasi za mwisho za upendo. Lakini toka Chama na Luis wameondoka leo hii ligi ipo karibu nusu hakuna mshambualiaji hata mmoja mwenye goli tano (5) kati ya washambuliaji wote watatu wa Simba.
 

Wako 2 wamekuja kwenye Majaribio Wakimshawishi Mwalimu wanasajiriwa
 
Wako 2 wamekuja kwenye Majaribio Wakimshawishi Mwalimu wanasajiriwa
Kwenye dirisha hili la usajili ndio tutajua mambo mawili:
1. Kama kweli viongozi wa Simba wapo "seriou" na kuikuza Simba ili iende mbali zaidi ya ilipofika au wana mpango wa kuirudisha chini ilipotoka huko miaka mitatu/minne iliyopita.
2. Pia tutajua kama kweli MO bado yupo kuisadia Simba kama alivyosema wakati anaachia uenyekiti wa bodi au alikuwa anazuga. Maana kwenye usajili MO huwa hatanii linapokuja suala la mchezaji mzuri.

Yote hayo hapo juu yatajulikana kutokana na aina ya wachezaji watakaosajiliwa kabla ya tarehe 15 mwezi huu kufika
 
Kuanzia kiuchumi mpaka kwa wachezaji TP MAZEMBE hii sio TP ya miaka 5 years ago Quality yao imeshuka sana.
hebu tupe source ya hizo habari kwamba TP Mazembe imeshuka kiuchumi.

Kisoka, nitakubaliana na wewe kwamba kwasasa performance yao imedrop kdg, kama ilivyo kwa zamalek walivyorudi nyuma kimashindano.

Tofautisha kudrop kimashindano na kuanguka kiuchumi.

Pyramid ipo juu kiuwezo wa fedha lakn kwny mashindano inatapatapa tu.
 
Tp Mazembe ilianza kuyumba kiuchumi baada ya boss wao Moise Katumbi kuipata kesi za kisiasa huko Congo kisha akatimukia Ufaransa.

Kiwango chao kimeshuka baada ya kushindwa kusajili wachezaji wazuri kwa zaidi ya misimu minne.

Kwahiyo kwa kiasi fulani uchumi wa Mazembe hauko sawa na ulivyokuwa zamani.
 
Simba wala hawahitaji kusajili, kwa sasa wanatumia utaratibu wa kwenda viwanjani saa sita usiku kuset "mitambo".
Kaduguda anafafanua.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…