Kwa taarifa yako mimi Simba damu na nimetoa maoni kama mshabiki wa mpira na sio kama mshabiki wa klabu ya mpira.
Tatizo letu ndio hapo, kila kitu mnaweka ushabiki wa timu mbele kuliko muelekeo wa soka la Tanzania kwa ujumla. Ni ngumu kutoa maoni mazuri kama unaweka ushabiki wa timu mbele. Tunaweka chuki binafsi kwenye kila jambo; ndio maana juzi ukaona wale wanaomchukia Bashite wali omba timu ya Taaifa ifungwe wakati timu ya Taifa inawakilisha wa Tanzania wote na sio mtu mmoja (bashite).
Sasa swala la Mo kama nia kumpa timu, apewe timu ili aanze kutimiza malengo yake badala ya makundi kuanzisha migogoro ambayo inaweza kukwamisha maendeleo ya timu.