Ukitoa wanaofanya kazi kwenye kada zifuafazo
- Udaktari
- Ufundi kama tanesco
- Walimu wa vyuo vikuu na shule ya msingi
- Polisi
- Wanajeshi
Hawa wanatakiwa waendelee kuajiriwa kwa mfumo wa sasa kwa sababu umri unavyozidi kwenda ndo wanakua na utaalamu wa juu
Walioajiriwa kwenye kada zifuatazo wanatakiwa waajiriwe kwa mda wa miaka 10 baada ya hapo mkataba uishe waajiriwe wengine ni kama
- TRA
- TANROADS
- Walimu wa secondary
- Wafanyakazi wa wizara
- Wafanyakazi wa bot
- Mashirika ya Hifadhi za jamii
Tukienda kwenye careers mfano
- Wahasibu hawa wanatakiwa kuajiriwa kwa miaka 10
- Afisa manunuzi (procurement) hawa wanatakiwa kuajiriwa kwa miaka 10
- HR hawa wanatakiwa kuajiriwa kwa miaka 10
- Mwanauchumi hawa wanatakiwa kuajiriwa kwa miaka 10
Faida yake
- Kupunguza tatizo la ajira
- Kuongeza ufanisi
mkuu tatizo la ajira halitatuliwi kwa kupunguza muda wa kufanya kazi tatizo la ajira linatatuliwa kwa mikakati ya muda mrefu kwa kishirikiana na sekta binafsi
hebu tuangalie mikakati hii ambayo imetumiwa na mataifa makubwa na ya kafanikiwa kabisa
Ili kutatua upungufu wa ajira, serikali, sekta binafsi, na jamii kwa ujumla zinaweza kutumia njia mbalimbali, zikiwemo:
1.
Kukuza Ujasiriamali na Biashara Ndogo
hapa ni pamoja na kupunguza mnyororo wa kupata leseni, kupunguza kodi wa wafanyabiasha wenye mtaji wa hadi 25m
Kutoa mikopo nafuu na mitaji kwa wafanyabiashara wadogo na yenye masharti nafuu kabisa
Kuwezesha mafunzo ya ujasiriamali na usimamizi wa biashara pamoja na kutoa vifaa vya kuwawezesha mfano mtu anayetengeneza viatu vya kandambili anapewa mashine baada ya hapo ana kuwa na kiwanda kidogo ataajiri watu watano mtaji ukikua atapanua hii inatumiwa na china na india
Kutoa mazingira rafiki kwa biashara kwa kupunguza urasimu na kodi kubwa.
2.
Kuimarisha Sekta ya Kilimo na Viwanda
Kuwekeza katika kilimo cha kisasa na kuongeza thamani kwa mazao kupitia viwanda vya usindikaji.
hii inaendana na kujenga viwanda vya juice, kuhitadhi mazao ya kilimo na kuwatafutia soko wakulima
mfano singida kuna kuwa kiwanda kikubwa cha alizeti na mafuta haya yanauzwa mpaka nje ya nchi ukanda wa iringa ukanda wa kanda ya ziwa kuna kuwa na viwanda vya ngozi,maziwa
Kuboresha miundombinu ya kilimo, kama umwagiliaji na teknolojia bora.
Kutoa mafunzo ya kilimo cha biashara kwa vijana kwa vitendo hii endane na sera ya kupanda matunda kwa afya hii itasaidia wananchi kutumia matunda kwa wingi na kupata mazao ya matunda kwa urahisi
3. Kuhamasisha Ubunifu na Teknolojia
yeyote mwenye kufanya ubunifu aitwe na awezesho na alindwe hii itasaidia sambamba na hilo kutengeneza na kuibua vipaji maalumu Kuwekeza katika elimu ya sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati
Kuendeleza programu za kusaidia wabunifu na wataalamu wa teknolojia kuanzisha miradi yao mfano anayetengeneza gari aruhusiwe na apewe support ya kutokuwa na kodi ili aonyeshe ubora zaidi
4.
Kuboreshwa kwa Mfumo wa Elimu na Mafunzo ya Kazi
masomo yawe ya vitendo kabisa hii itasaidia zaidi kutengeneza mtu imara zaidi lakini afrika tumefanikiwa kufanya kazi tu ya dini mtoto anapewa zaidi elimu ya dini wakati watoto wadogo ulaya wanasoma kwa vitendo na si kushinda makanisani wakisoma madude yasiyo kuwa na faida tofauti na kutengenezewa mazingira ya kuchotwa hela tu na kuwa zezeta wa iman na kujengewa mazingira ya hofu tu
Kulinganisha mitaala ya elimu na mahitaji ya soko la ajira pamoja na kupanua mafunzo ya ufundi na ujuzi wa kazi kwa vitendo.
Kuweka ushirikiano kati ya vyuo na waajiri ili wanafunzi wapate uzoefu wa kazi mapema.
5. Kuongeza Uwekezaji wa Ndani na wa Nje
Kuweka sera rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa nje ili kuongeza fursa za ajiri pamojq na Kuboresha miundombinu (barabara, umeme, maji) ili kuvutia wawekezaji.
6. Kuimarisha Sekta ya Huduma na Utalii
Kukuza utalii wa ndani na nje kwa kutangaza vivutio vya asili na utamaduni pamoja Kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu huduma za hoteli, mwongozo wa watalii, na biashara ya sanaa.
7.
Serikali Kuajiri kwa Ufanisi na Kukuza Sera za Ajira
Kuanzisha miradi ya maendeleo inayotoa ajira kwa watu wengi, kama ujenzi wa miundombinu pamoja Kubuni sera zinazolinda wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi hii muhimu sana sekta binafsi ndio inaajiri watu wengi hivyo walindwe zaidi wakitaka kuporomoka wapewe support zaidi pamoja na Kutoa motisha kwa makampuni yanayoongeza ajira kwa vijana na wanawake.