Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Taasisi na Idara mbalimbali Mkoani Arusha zimeendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani humo katika kupambana na uhalifu ambapo Idara ya maji na Benki ya Crdb wametoa vifaa vya Tehama katika kituo kikuu cha Polisi Arusha.
Akiongea mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mkurungenzi wa mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Mkoa wa Arusha Mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji wa Jeshi la Polisi katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kwa upanda wake Meneja wa Benki ya Crdb tawi la Arusha Bi Mary Kimasa amesema kuwa ujio wao ni kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi huku akiweka kuwa vifaa hivyo anaamini vitakwenda kusaidia Jeshi hilo ambalo linategemewa na wananchi katika ulinzi wao na mali zao.
Nae Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Georgina Matagi amezishukuru taasisi hizo ambazo zimetoa vifaa hivyo huku akiwasihi wengine kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi wilayani humo katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Mwilikiwa Masawe ambaye ni Mjumbe wa bodi ya maji Salama Mkoa wa Arusha amesema waliamua kuleta vifaa vya Tehama wakitambua mchango na mapambano ya uhalifu yanayofanywa na Polisi Wilaya ya Arusha ili kuwasaidia katika mapambano hayo.