Kuna taasisi ya elimu ya juu imeruhusu umoja wa kusaidiana kwa misingi ya dini. Tafsiri yangu ni kwamba, kwa kuunda umoja huo, na kuhamasishwa na viongozi wa taasisi ni ishara ya kuwatenga watu wa dini zingine.
Nimeona ushahidi kupitia kumbukumbu ya malipo ya mishahara (salary slip) ya mmoja wa wanachama hao ikionesha michango ya umoja huo inakatwa moja kwa moja toka hazina ya serikali. Bado 'nabembeleza' kupata nakara ya malipo hayo, nitaileta hapa jamvini.
Ni vema kutoa tahadhari kwa viongozi hawa dhaifu wanaofikia hatua ya kuhamasisha umoja wa kusaidiana kwa misingi ya dini ndani ya ofisi za serikali. Mbaya zaidi ni taasisi ya elimu ya juu! Kwa maana nyingine hata elimu itatolewa kwa misingi ya kidini.