Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Mzee Butiku inapoteza hadhi yake!

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Hii Taasisi inakwenda kupoteza hadhi yake. Inaongozwa na chawa kachara.

Matamshi yake ya juzi yanaivua nguo taasisi acha yeye mwenyewe anakuwa "takataka"!

Kupoteza heshima yake kubwa aliyoijenga for decades!

Haongelei matatizo makubwa ya utawala wa Samia, mauaji ya watu on 29, na mengine mengi!

Eti rais wa watanzania na si wa ccm. Dunia nzima inasema hapakuwa na uchaguzi, wewe unasema Rais wetu!

Unatetea tumbo lako na wanaokuhusu!
 
Nchi hii hakuna taasisi iliyobaki salama kwenye nchi hii ya ma primitive!
 
Kwangu mimi imeshapoteza. Kwa kilichotokea tarehe 29 na matamko aliyotoa Butiku ni kama ameifuta kabisa hiyo taasisi. BTW kwa nini asiachie vijana wenye ujasiri, wenye maono na wakweli kama mwl Nyerere waongoze na yeye awe mshauri tu? Kuna jambo jingine: pengine Butiku alikuwa overrated na alikuwa anajificha kwenye kivuli cha Nyerere. Kuna ule msemo usemao kuwa kiongozi mzuri hujulikana wakati wa matatizo na taharuki. Hiki ndicho kipindi ambacho alitakiwa kuonyesha umuhimu wa hiyo taasisi.
 
Hakuna taasisi pale, walishafunga kitambo na chanzo ni yeye butiku kufanya MNF km taasisi ya familia, inaanzishwa sijui samia scholarship na kuwa na pesa nyingi wakati MNF hata kulipa wafanya usafi imeshindwa!
 
Kama unajua CV ya Batiku huhitaji kushangaa kwa yeye kuwa chawa kwa mamlaka kwa kuwa maisha yake yote ya kazi amekuwa Mbeba mikoba wa Mwalimu Nyerere.

Hajawahi kuwa na fursa ya kutoa maamuzi mazito ya kujitegemea.
Kwa nafasi yake pale Ikulu, uhuru aliokuwa nao pekee ni kuamua mkoba wa Mwalimu aubebe kwa mkono wa kulia au wa kushoto,basi.
 
๐Ÿ˜๐Ÿ˜…๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜ƒ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜€ You are very correct! Kumbe ni๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ
 
Nyerere alitukosea sana kuunganisha nchi kubwa kama Tanganyika na mkoa kama Zanzibar. Kwa anayoyafanya Butiku ni ushahidi tu kuwa aidha amezeeka akalee wajukuu au yeye na Nyerere hawakujua wanachokofanya hadi kutuingiza kwenye janga la aibu tulilofikia sasa hasa mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ