Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) Yagawa Mitungi ya Gesi 2,000 (Kg 30) kwa Wanawake Wajasiriamali Mkoa wa Kusini, Zanzibar
Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir tarehe 04 Julai, 2024 imegawa Mitungi ya Gesi 2,000 ( KG 30) kwa vikundi vya wanawake Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini, Zanzibar.
Hafla ya ugawaji wa Mitungi ya gesi ya kupikia ilifanyika katika ukumbi wa Kibeshi Unguja Ukuu ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati.
Wizara ya Nishati ya Tanzania imewakabidhi Taasisi ya MIF mitungi 2,000 (Kg 30) kutoka ORYX Energy Tanzania, MIF wamepewa dhamana ya kuwagawia vikundi vya wanawake Wajasiriamali vinavyosimamiwa na MIF kupitia mradi wa Upishi Salama.
Hayo yamefanyika ikiwa ni kuendeleza juhudi za Serikali za kupunguza matumizi ya mkaa na kujali afya ya wapishi haswa wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa, kuokoa na kutunza mazingira kwa kupunguza ukataji miti.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-07-05 at 00.14.36.jpeg134.5 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-07-05 at 00.15.18.jpeg156.3 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-07-05 at 00.15.18(1).jpeg107.3 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2024-07-05 at 00.15.18(2).jpeg114.7 KB · Views: 7 -
Screenshot 2024-07-05 at 11-28-11 Mwanamke Initiatives Foundation (@mwanamkeinitiativesfoundat...png822.1 KB · Views: 10 -
Screenshot 2024-07-05 at 11-27-50 Mwanamke Initiatives Foundation (@mwanamkeinitiativesfoundat...png878.5 KB · Views: 7 -
Screenshot 2024-07-05 at 11-27-57 Mwanamke Initiatives Foundation (@mwanamkeinitiativesfoundat...png808.2 KB · Views: 7