JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam inakabiliwa na uhitaji wa matiti bandia kwa ajili ya kusaidia akina mama wenye saratani ya matiti ambao wengi wao wamekuwa wakikatwa titi na hivyo kuhitaji titi bandia ili wawe na mwonekano mzuri.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa hafla ya Nyerere grand dance itakayofanyika Oktoba ambapo sehemu ya mapato yake itatumika kununua matiti bandia 100 kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wanaokatwa matiti kutokana na tatizo la saratani.
Kwa upande wake Muta Rwakatare, amesema harambee hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuanzishwa kwa taasisi ya Mama Getrude Rwakatare, ambapo kwa kuanzia harambee hiyo itafanyika Oktoba 8, 2022, mwezi wa saratani ambapo taasisi hiyo itatoa misaada pamoja na kufanikisha zoezi la upimaji wa saratani ya matiti.
Chanzo: EATV