Uchaguzi 2020 Taasisi za Kimataifa zatoa tafiti zao kuhusu Magufuli na uchaguzi wa 2020

Uchaguzi 2020 Taasisi za Kimataifa zatoa tafiti zao kuhusu Magufuli na uchaguzi wa 2020

Huitaji kuwa na PHD kujua hilo kwa upinzani upi uliopo sasa hadi 2020 wachukue nchi
Inatakiwa wajenge vyama na kujipanga kwa 2025
Lakini watatujaza ujinga na ukiisha uchaguzi watatuambia kuwa walishinda ila waliibiwa kura


Sent using Jamii Forums mobile app
join date 30 dec 2018 , umejiunga humu kuja kusema uongo ?
 
Habari za utafiti wa hivi karibuni toka shirika amaTaasisi ya kimataifa ya Intelijensia ya Kiuchumi/ Economist Intelligence Unit/EIU lenye makao yake makuu jijini London Uingereza, limetoa matokeo yake ya kitafiti kuhusu UCHAGUZI ujao wa 2020 wa Tanzania.
Taasisi hiyo ya kimataifa ambayo ndo think tank kuu ya mambo ya kimataifa katika Nyanja za KISIASA, KIUCHUMI n.k.imetoa utafiti wake.

Miongoni mwa kazi zake kuu ni kufanya Utafiti/Research na ANALYSIS/ UCHAMBUZI ili kupata MATOKEO/ PROJECTION za nchi mbali mbali kuhusu Siasa na Uchumi na hivyo kubashiri wakiwa wamelenga shabaha kabisa/ Accuracy katika ubashiri wao.

Kulingana na Tafiti na Chambuzi zake za hivi karibuni zinazohusu uchaguzi wa Tanzania wa mwaka ujao wa 2020,
Rais Magufuli anategemewa kuchaguliwa tena kwa kura nyingi sana kuliko uchaguzi uliopita wa mwaka 2015.

Tafiti zao zinaonyesha pia kuwa, chama cha CCM kitachukua viti vingi sana vya UBUNGE na hivyo kuvinyima vyama vya upinzani nafasi nyingi za UBUNGE.

Tafiti zinasema pamoja na kuwa vyama vya upinzani vimejaribu sana bado CCM itapata ushindi mkubwa sana na hivyo kuifanya Tanzania kubaki nchi iliyo na Stability/AMANI kwa miaka mingi ijayo.
Chanzo: IEU.
mmebakia kudanganya tu. Economists walewale waliomuita mpumbavu??
 
CCM huwa hawashindi kihalali.

Sababu zangu ni kwamba CCM hajawahi kushinda kihalali, sababu kubwa zaidi kuliko zote ni hii,mkurugenzi nimekuteua mimi,ninakulipa mshahara, unaishi kwenye nyumba ya serekali, unatembelea gari ya serekali halafu nikusikie umetangaza mpinzani kashinda, maneno hayo na marufuku hiyo siyo ya kwangu ni ya mwenye serekali yake.
Hiyo ni dhana tu.
Kama ingekuwa ni hivyo, basi tusingekuwa na Wabunge wa vyama vingine kando ya CCM.
 
Muongo wewe hii link yako inakupeleka kwenye home page ambayo hiyo ripoti haipo. Halafu siku nyingine ukitoa hoja kumbuka ni jukumu lako kuitetea kwa vielelezo na sio kuwaambia watu wakatafute vyanzo.
Umeangalia ukakuta hamna?
Pole ni bonge la taarifa inahitajii muda.
Ni zaidi ya home page. Tafuta mkuu
 
naweza kukuthibitishia kwamba nusu ya wabunge wa ccm hawakushinda uchaguzi ule , mfano halisi ni Mbunge wa Kyela Harrison Mwakyembe na mbunge wa Rungwe Saul Amon
Je hawa wabunge wa upinzani waliwekwa na CCM?
Naamini kuwa kuna demokrasia. Ila sisi wafrika hatukubali kushindwa.
Hata kama ni MPIRA bado mtu atasema refa alibana filimbi.
Hili ndo tatizo letu.
 
Ukiongelea uchaguzi wa Tanzania ni lazima uguse tume ya uchaguzi, vyombo vya dola, vyombo vya habari na magoli ya mikono...... kisha huo utafiti wauandike tena upya na kwa lugha ya kiswahili kisha ukausome.
Mkuu nina swali.Je hawa wabunge wa upinzani waliimgiaje bungeni.
Je ni CCM iliwaweka kama boya?
Ukinijibu hapo utakuwa umepata jibu kuwa dhana yako si ya kweli.
 
Back
Top Bottom