HOJA Taasisi za Vibali: Kuzuia au Kuwezesha Wajasiriamali?

HOJA Taasisi za Vibali: Kuzuia au Kuwezesha Wajasiriamali?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Taasisi Za Umma Nyingi Zinazohusika na Vibali (Regulatory Authorities) Kama BRELA TBS TMDA TCRA NEMC EWURA LATRA TRA OSHA GCLA n.k

Hebu Ifike Hatua Tufanye Kazi Kwa kuwezesha zaidi na si kuzuia Kwa Mfano mzuri Mjasiriamali Anapata Wazo La Kuanzisha Biashara Kama Crips tu Za Kawaida Anatafuta Mtaji Anaanza Kutengeneza Anatafuta soko labda Anatembelea Supermarket Baadhi Kuomba achukue Order kisha Anapeleka Mzigi Wake sokoni Pengine Amekopesha ndo Anaanza Wanakuja watu Wa TBS wanaona kuwa mtu huyu hana kibali cha ubora na cha kuweka Sokoni Bidhaa hii Wanabeba Bidhaa zake zote Zilizopo Supermarket Na bado Wanamfungia mtu huyu mpaka Atakapokamilisha kupata kibali,

Ni Sahihi Kudhibiti Viwango Vya Ubora je Hiyo ni Njia Sahihi Kwanini Nyiye Kama watu Wa Ofisi Baada ya Kugundua Hilo Msingeamua Kumtafuta Mtu huyo na Kumpa Elimu ikiwezekana mkahakiki Ubora Wa Kiwango Cha Bidhaa Kwenye Ofisi yake Mwenyewe kisha Mumpe Utaratibu kama yuko chini ya Kiwango au yuko sawa Hii Itamfanya huyo mtu asianze Upya pia Mtu huyu Atakuja Kuwa Na faida Kwa Taasisi nyingine Kama Brela, TRA, na nyingine kwasababu Lazima Atakua na itakuwa Kampuni ataajiri watu atalipa mapato Makubwa kwanini Tuwe Ofsini Kwaajili ya kuabudiwa Maboss Wote Kila idara Ya utoaji Wa vibali Kabla Hamjamfungia mtu jiulizeni Idara yako imemwezesha mtu huyo nini? Tuhame basi Huko Mbona Hivi Vitu Vimesemwa Sana.

Asante Mdau.
 
Back
Top Bottom