DOKEZO Taasisi zinazotoa mikopo zitunze faragha za wateja wao

DOKEZO Taasisi zinazotoa mikopo zitunze faragha za wateja wao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jamaludin

Member
Joined
Apr 26, 2024
Posts
48
Reaction score
40
Napenda kulalamikia makampuni ya mikopo madogomadogo na assasi zisizo za kiserikali, kurekebisha kauli zao na misimamo yao, Mtu anapoomba mkopo nikwamba anahitaji mkopo ule ajikimu na matatizo aliyonayo, lakini badala yake wao hu (upload users devices data) mfano Phonebooks na meseji kisha mteja wao akichelewesha kurejesha mkopo hata ndani ya 24 tu, wanamuongezea riba na kuwatumia meseji jamaa wa wateja wao (yaani nikama kumuaibisha mteja) ili ionekane anadaiwa, hili linafanyika kwenye Application nyingi za mikopo Mfano MR FINANCE(Ustawi Loan/Cash Pesa/Pesa Tree/Yes Pesa..etc)

Naiomba serikali kuwaangalia hawa waendeshaji wa mikpo na kujitahidi kutunza faragha za mteja wao.

Kwasababu Mteja anapoomba mkopo hamna mzamini ispokua kitambulisho chake cha uraia kwahiyo atatakiwa kuchukua responsibility na si kuwatumia meseji watu wake kwenye phone book.

Ahasanteni kwa kunielewa mlionielewa:

1000058742.jpg


Soma: Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yazionya Taasisi za mikopo zinazodhalilisha watu ikiwemo kutuma ujumbe kwa ndugu
 
Hawa jamaa siyo wastaarabu,hata deadline ya kuwalipa haijafika,wanataka ulipe yaani ni lazima,usipofanya hivyo,unatangazwa kuwa ni tapeli.
 
Muachage kwenda na nyie. Mambo mengine jikaze tu. Mikopo unatangazwa mji mzima na bado unaenda tu.
 
Back
Top Bottom