Tabaka la elimu Tanzania litatumaliza, Rais, Waziri wa Elimu tufanyeni jambo hili kwa kasi laweza saidia

Tabaka la elimu Tanzania litatumaliza, Rais, Waziri wa Elimu tufanyeni jambo hili kwa kasi laweza saidia

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
8,406
Reaction score
9,619
Ndugu wanaJF na Watanzania kwa ujumla amani ya Mungu na ikawe juu yenu kila mmoja KWa imani yake.

Husika na mada tajwa hapo juu, Matabaka ya elimu Tanzania limekua zimwi linaloendelea kututafuna Kama watanzania hasa kwa vijana wetu katika level tofauti za elimu nchini hasa huku chini kwenye elimu ya Msingi ambapo ndo basic haswa.

Leo zipo shule za msingi za serikali na watu binafsi (primary english Medium) ila vijana wetu wanaohitimu huko la Saba ni Mbingu na aridhi, kwamba ni kwepesi mkuta mtoto alie kidato Cha kwanza hajui soma Wala kuandika toka shule zetu za serikali ila ni ngumu Kukutana na mtoto wa namna hii kutoka shule binafsi , ukiachana hata uwezo wa kujitambulisha tu kwa kingereza.

Wazee wetu walisoma mpaka la nne , la Saba ila hata leo ukikutana nao wanaweza wasiliana KWa lugha ya kingereza bila shida , Sasa leo tunakwama wapi kuwatengenezea watoto wetu misingi bora na iliyosawa KWa watoto wapitao shule za Serikali kuendana na Kama Sio kufanana na watoto wapitao shule binafsi?

Ikumbukwe shule za Serikali watoto wanaopitia huko ni kutoka kwenye familia maskini na duni ,hutokuta mtoto wa yeyote yule mwenye uwezo watoto wake wapo kule, na Sio kwamba hawataki bali uchumi ndo shida.

Mh Rais na Waziri wa elimu Tz mnaweza kufanya Jambo Ili kuleta angalau usawa katika elimu yetu ya msingi ambayo ndo basic, maana Sio lazima kila mtanzania afike chuo kikuu Ili fanikiwa kimaisha, ila ukimtengeneza kijana / mtoto anzia msingi ataenda pia kidato Cha kwanza akiwa anajua anaenda fanya nini, lakini hata katika maisha yake ya utafutaji unakua umemrahisishia Mambo mengi kuanzia mawasiliano nk.

Mpaka Sasa tunaona matatizo tunayokumbana nayo Kama taifa kutoka na mfumo wetu wa shule za msingi hasa za serikali leo MSUKUMA (Mbunge) ndo anaanza jifunza lugha ya mawasiliano ya kingereza pamoja na kwamba ana pesa na ni Mbunge ,hii haikubaliki

NINI TUFANYE KAMA TAIFA CHINI YAKO MH RAIS,

Napendekeza Sasa ikikupendeza tufanye mahamuzi Magumu ya elimu katika Taifa letu hasa kwenye shule za msingi za Serikali tanzania nzima KWa kuzibadili kuwa shule za

PRIMARY ENGLISH MEDIUM SCHOOL .hii itasadia kumpunguza Matabaka ya elimu nchini na inawezekana Kama zilivyo kuzibadilisha na maboresho mengine kuendelea fanyika taratibu.

Kufikia hatua hii napendekeza serikali Sasa kuanza ajiri KWa Kasi walimu wa mfumo huu Sasa hasa wa
BABY CLASS,MIDDLE CLASS, PRE UNIT, na walimu waliopo kwenye shule hizi waanze kupewa MAFUNZO kupitia Kanda ili kuweza endana na mfumo huu

Napendekeza mfumo huu mwaka 2024 January huwanze kufanya kazi maana walimu wapo,shule zipo, ila swala hapa ni kuongeza .

Niwashukuruni
 
Shida ya Elimu yetu ipo kwenye mitahala yani kinacho fundishwa na kilichopo mtaani ni vitu viwili tofauti . Elimu yetu imejikita katika vyeti na idadi ya wanaofaulu tu wakati kwa wenzetu imejikita katika maarifa na msingi wa kujitambua

Walimu wengi nao wamekuwa bora liende unakuta mwalimu yupo kazin miaka 6 hajawaipata mafunzo/semina ya kumuendeleza na maarifa mapya lazma akili itaganda na atakuwa anafundisha kama wajibu tu na sio wito

Lugha unasoma kiswahili msingi ukifika secondary kingereza hatuna lugha rasmi ya kujifunzia na kibaya zaid sijui nimeona mimi tu yan alichojifunza mwanafunzi shule ya msingi anakuta kile kile kuanzia form 1 mpk 2 tofauti ni lugha tu ila vitu ni vile vile unajiuliza sasa haya marudio ya nn

Wasomi/maprofesa wamechanganya siasa na Elimu yan mtu anajua Elimu yetu inavurugwa hana habari yupo tu kazi kuabudu wanasiasa tu

NB: Mungu aliumba akili sio Elimu
Unaweza ukawa na Elimu kubwa ila sio akili
 
Kama mtunga sheria(Mbunge) anatakiwa ajue kusoma na kuandika kwa kiswahili.

Mitaala mibovu.

Mpaka leo mtu anafundishwa vita ya kwanza ya dunia huko ulaya badala ya kufundishwa kilimo,ujasiriamali na biashara
 
Uzuri talanta ya mtu haiamuliwi na umesoma serikalini au private.
Swala sio talanta, tunapoelekea kutafuta njia za talanta zitakua ngumu kama hawezi andaa vijana vizuri kuanzia shule za msingi hasa kwenye lugha ya mawasiliano Mkuu,

Shule za Serikali ndo watoto wa familia za chini wapo , hata mtoto akimaliza huko akaenda veta kweli anakua na ujuzi flani ila bado kwenye lugha za mawasiliano katika soko la ajira in E .frika inakua shida,

Kweli kujua kingereza sio kwamba mtu anaakili Sana ila Kama sehem ya mawasiliano inasaidia vuka vikwazo vingi katika utafutaji,

We huoni hata wasanii wetu waendapo nje wanavyopata shida, vipi Kama tukiweka msingi huu wa lugha kwenye shule zetu KWa vijana wanaokuja huoni watakua wamerahisishiwa Mambo mengi
 
Wachina , wakorea, warusi, kiingereza sifuri.
Sikatai watu kukijua kiingereza lakini kuna mambo ya msingi/maana zaidi linapokuja suala la kutoboa kimaisha: talanta binafsi, ubunifu, stadi za maisha (bidii, kujituma, kutambua fursa, matumizi bora ya pesa, n.k), ujuzi na maarifa. Kiingereza ni icing on the cake. Sisi tulio kitaa tunaona waziwazi, nenda pale Kariakoo uniambie ni mkinga gani pale anaongea kingereza vizuri? Kama ikibidi mtu akijue kiingereza kwa dunia hii ya sasa kuna njia nyingi sana za kukijua kiingereza kama mtu atahitaji kukijua.
 
Mkuu, haya mambo tusahau mark my words! Huwezi mpa fisi aamue mambo ha kondoo. Ningumu Sana kueleweka kwa lugha hii, Ujinga ni mtaju mkubwa Sana kwa Serikali yetu ndio maana hawashtuki kuona ubovu wa elimu na hakuna jipya wanalilileta.

Just imagine Karne ya ishirini na moja serikali yetu haikai chini kuwaza mtaala mzuri wa elimu kwa wanachi wake , Bali wanaahidi kuleta maji na umeme ambavyo vyote vimewashinda. Hatuwezi kuwa serious Kama nchi kuendelea kuamini Serikali ya Tanzania italeta mabadiliko katika Elimu yetu huku tukiwa na wabunge walioshindwa kuja na mikakati na kuishauri serikali namna Bora ya uendeshwaji wa Elimu.

Hatuwezi kutoboa katika Elimu Kama tutapangiwa matofali na Kuta kupakwa rangi nyeusi ili kuitwa ubao kwaajili ya watoto wetu na kupiga makofi kuwa serikali ni sikivu na inajenga Shule Bora at the same time mtoto wa mkuu wa wilaya hasomj hapo huu ni upuuzi

Serikali ijenge miundombinu Bora kwa Shule zetu, ikae na wataalaam na wadau mbali mbali katika Elimu waje na mapendekezo ya mtaala kwa Elimu yetu
 
Wachina , wakorea, warusi, kiingereza sifuri.
Sikatai watu kukijua kiingereza lakini kuna mambo ya msingi/maana zaidi linapokuja suala la kutoboa kimaisha: talanta binafsi, ubunifu, stadi za maisha (bidii, kujituma, kutambua fursa, matumizi bora ya pesa, n.k), ujuzi na maarifa. Kiingereza ni icing on the cake. Sisi tulio kitaa tunaona waziwazi, nenda pale Kariakoo uniambie ni mkinga gani pale anaongea kingereza vizuri? Kama ikibidi mtu akijue kiingereza kwa dunia hii ya sasa kuna njia nyingi sana za kukijua kiingereza kama mtu atahitaji kukijua.
Mkuu njia za kufanikiwa kwenye maisha zipo tofauti Sana ila pia elim ni njia mojawapo, katika ukanda huu WENDA tz ndo tuko nyuma kiushindani wa soko la ajira ndani ya E.Afrka na nje , KWa vijana wetu na shida sio kwamba hawawezi tatizo kubwa ni ni communication skill .

Hatuwezi ACHA wekeza kwenye elim bora na yenye kuleta ushindani kisa mtu au kabila flani kafanikiwa bila kutokua na elim

Hata hivyo ipo tofauti Sana Kati ya mfanyabiasha anaefanya akiwa na elim plus communication skill nzuri na wa upande mwingine,

Maono ya taifa nikuwa na wafanya biashara wakubwa wa kitaifa na kimataifa je tunafikaje huko Kama hatuwezi wekeza kwenye elim?

Tz tumechelewa Sana hasa kwenye shule za serikali ,za binafsi wako juu maana hata wanaoenda huko ni wale wenye kipato

Wote hatuwezi toboa KWa njia moja chamsingi kila mtu pitia njia tofauti wote mkutane pale mojawapo ikiwa elim,

Dunia ya leo na inayokuja bila kutokua na lugha inayoweza kukuunganisha kimataifa bado shida,

Nakubali njia za kujifunza kingereza zipo nyingi, ila kwanini, mtoto anaeanza leo shule ya Msingi asijue/kujifunza, kwamba tumsubilishe huko mbele kisa njia za kujifunza nyingi wakati Jambo linawezekana
 
Hata hivyo nikubaliane na wewe kwamba penye elimu bora hata communication skills itakaa sawa tu.
 
Elimu I Shaka I,hata kuandika tu humu mitandaoi ni shida,na imeenea..
 
Naunga Mkono hoja. Ni kweli changamoto nyingi sana zitakuwepo awali lakini mbeleni tutafaidika sana.

Kwanza shule binafsi zitapungua, wazazi wengi watawapeleka watoto wao shule za serikali, watafanya mpango wa masomo ya ziada. Si Kila Mzazi anaesomesha mtoto wake shule binafsi ana uwezo kiasi hicho ila anajibana amudu Kwa wofa wa kupeleka watoto shule za serikali.
 
Kweli mkuu ukienda Mbeya mfano zipo shule za Serikali za English medium nazifaham 2 Benjamin plus Azimio zinafanya vizuri japo hutoza ada Kama laki 5 KWa mwaka ila mpaka tunavyoongea nafasi kupata pale huwa ni kimbembe,

Sasa hii tunataka watoto wetu ata alioko huko ndani apate fulsa , inawezekana mkuu
 
Watu watakubeza na kukukejeli lakini hii ni hatua ya awali kabisa kurekebisha mfumo wa elimu yetu.

Mengine yatafuatia baadae
 
Uzuri talanta ya mtu haiamuliwi na umesoma serikalini au private.

Mkuu sijui dhima ya maini yako ni nini lakini kwa maelezo ya JK mwanafunzi aliyemaliza la 7 shule ya serikali na mwenzake wa binafsi walio na talanta zinazofanana, yupi itakuwa imeonekana mapema??

Sidhani unaieleza talanta katika kizania ya elimu. Umechanganya talanta na elimu. Uendeshaji ndege ni elimu, kuwa mwanariadha ni talanta. Alichosema JK ni elimu - talanta si muhimu kuliko elimu!
 
Kuendesha ndege ni elimu lakini kuvumbua ndege ni talanta. Utaamua mwenyewe kipi cha muhimu kati ya elimu na talanta. Na kuna njia nyingi za kupata elimu kuliko ile anayozungumzia JK, ikiwemo kupata elimu katika mfumo usio rasmi. Katika zama hizi za karne ya 21 watu wanapata maarifa kwa njia nyingi sana nje ya mifumo rasmi -- na itabidi ujiulize kwa nini wengi wa waliomo bungeni siyo wale walio na elimu saaaana lakini bado wamefanikiwa kufika bungeni. Ningeweza kwenda zaidi na kukuuliza kwanini tajiri namba moja Tanzania siyo profesa au PhD. Ukweli wa mambo ni kwamba mimi silengi kupuuza umuhimu wa kukijua kiingereza ila nina uhakika kwamba talanta ya mtu haiwezi kukwamishwa na kutokijua kiingereza. Yapo ya kukwamisha talanta ya mtu lakini siyo kiingereza.
 
Mkuu sijui dhima ya maini yako ni nini lakini kwa maelezo ya JK mwanafunzi aliyemaliza la 7 shule ya serikali na mwenzake wa binafsi walio na talanta zinazofanana, yupi itakuwa imeonekana mapema??
Unataka kusema mwanafunzi aliyemaliza darasa la saba akapata ufaulu unaofanana na yule wa private (assuming ufaulu ni kielelezo cha uwezo) basi huyu wa serikali uwezo wake hautaweza kuonekana kulinganisha na yule wa binafsi?
 
Uwezo utaonekana tu ila mbele ya safari katika kukimbizana na fulsa utofauti utakua mkubwa tu
 
Back
Top Bottom