Mgombea ubunge wa jimbo la Sengerema alivyokuwa kwenye mkutano katika kijiji cha Mchangani kasema changamoto zingine atazimaliza kwa pesa yake mwenyewe, kwa kuanzia atatoa mifuko 200 ya saruji kumalizia ujenzi wa sekondari ili januari watoto waanze kusoma.
Kasema kwa sasa katingwa na kampeni ila baada ya uchaguzi pia atawajengea shule ya msingi kwa pesa ya mfukoni kwake. Mgombea ambaye ni tajiri na mfanyabiashara maarufu wa Sengerema amekuwa anakerwa na umasikini wa wana Sengerema.
Kawaomba wananchi wasimchanganyie madiwani wakamkwamisha kwenye madhumuni yake, alivyokuwa katika kijiji cha Ibisabageni aliwalaumu wanakijiji kumharibia mbunge aliyepita bwana William Ngereja kwani walimwekea gunzi kwenye tochi, akashindwa kuona mbele na maendeleo yakakwama.