Uchaguzi 2020 Tabasamu kutumia nusu ya utajiri wake kuwahudumia wana Sengerema

Uchaguzi 2020 Tabasamu kutumia nusu ya utajiri wake kuwahudumia wana Sengerema

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Posts
16,054
Reaction score
11,568
Mgombea ubunge wa jimbo la Sengerema alivyokuwa kwenye mkutano katika kijiji cha Mchangani kasema changamoto zingine atazimaliza kwa pesa yake mwenyewe, kwa kuanzia atatoa mifuko 200 ya saruji kumalizia ujenzi wa sekondari ili januari watoto waanze kusoma.

Kasema kwa sasa katingwa na kampeni ila baada ya uchaguzi pia atawajengea shule ya msingi kwa pesa ya mfukoni kwake. Mgombea ambaye ni tajiri na mfanyabiashara maarufu wa Sengerema amekuwa anakerwa na umasikini wa wana Sengerema.

Kawaomba wananchi wasimchanganyie madiwani wakamkwamisha kwenye madhumuni yake, alivyokuwa katika kijiji cha Ibisabageni aliwalaumu wanakijiji kumharibia mbunge aliyepita bwana William Ngereja kwani walimwekea gunzi kwenye tochi, akashindwa kuona mbele na maendeleo yakakwama.
 
Tabasamu ataleta maendeleo asibadilike tu. Sio kama Ngereja hovyoo.
 
Kama kweli anakerwa na umaskini wa wanajimbo lake, asingoje hadi wamchague ndio ajenge hizo shule. Hiyo ni rushwa hata Takukuru wanajua hivyo.

Jamaa ana pesa nyingi tu, laiti angeyafanya hayo hapo awali angekuwa na wasaa mzuri kwa sasa. Ila nampongeza kwa jinsi alivyoweza kupenya lile jopo la Wajumbe. Hongera sana Bwana Tabasamu.
 
Kafanya mengi sana hata kabla ya kupewa hiyo ridhaa ya kugombea Ndio maana haikua shida kwake kupambana na ngeleja
 
Back
Top Bottom