Tabasamu la Rais Samia, Tabasamu mbele ya Tundu Lissu, Kiongozi wa Chama Cha Upinzani Nchini (CHADEMA)

Maryam Malya

Senior Member
Joined
Nov 29, 2021
Posts
116
Reaction score
260
bde8c343-145a-4702-820d-6c665f142ddc.jpg
Mama anazidi kuonesha jinsi alivyo na moyo wenye hekima, utu na upendo.

Tazama, amesafiri kutoka Ufaransa kwenda Ubelgiji akiendelea na ziara yake barani Ulaya. Kufika Brussels, Ubelgiji anapokea maombi ya Lissu akiomba waonane.

Kwa moyo wenye upendo alionao Mama Samia unadhani angekataa? Akatae vipi wakati yeye ni Mama wa kila Mtanzania aliyepo ndani na nje ya Nchi yetu?

Akatae vipi wakati yeye habagui? Kwake kila mmoja ni sawa, uwe CCM, ACT au Chadema mbele ya Rais Samia kila mmoja ni sawa.

Wameongea Nini? Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema ni mambo yanayohusu ustawi wa Nchi yetu. Wooow just woow.

Hongera Rais Samia, Hongera Mama yetu, Tuko salama kwenye mikono yako.

Kazi zako, Mipango yako, Upendo wako tuufananishe na nini? Jibu ni hakuna. Wewe ni Samia, Rais wetu na Mama yetu.
 
Ni sawa na Ni kweli kabisa. Lakini Rais ni Taasisi na nchi ni Mifumo. Kwa tabasamu hilo ni ishara nzuri ila kwa Taasisi na Mifumo iliyo Nyuma yake napata mashaka kila nikitazama picha hiyo.
 
Hongera Rais wetu mama Salmia Suluhu Hassan kwa kukutana na mpinzani wako wa kisiasa!!! Umeleta somo kubwa siyo tu kwa Watanzania bali dunia nzima.Mungu akubariki mama yetu kwa hatua uliyoichukua.Umeliunganisha Taifa letu.Na umekubalika zaidi.
 
Maryam Malya hivi Kaaya, Malya na Urio ni watu wa eneo moja? Nimeuliza tu. Kwenye jibu lako mtoe John Mallya.
 
Mhe. Tundu Lissu amefurahi sana na inaonekane amefarijila sana sana.
ila anatakiwa ajifunze kitu kimoja tu nacho ni;
1. Unapo heshimiwa au unapo onyeshwa uungwana nawe uwe hivyo hivyo.

Rudi nyumbani tuijenge nchi yetu.
 
Team roho mbaya Mama amewafumba midomo.
 
Mhe. Tundu Lissu amefurahi sana na inaonekane amefarijila sana sana.
ila anatakiwa ajifunze kitu kimoja tu nacho ni;
1. Unapo heshimiwa au unapo onyeshwa uungwana nawe uwe hivyo hivyo.

Rudi nyumbani tuijenge nchi yetu.
Kwani Lisu aliacha lini kuwa muungwana? Tatizo lenu ni kujibu hoja kwa bunduki, kuteka na kubambikia kesi. Mkijirekebisha kwenye hayo maeneo hii nchi itakua tamu sana hapa duniani.
 
View attachment 2121712
Mama anazidi kuonesha jinsi alivyo na moyo wenye hekima, utu na upendo.

Tazama, amesafiri kutoka Ufaransa kwenda Ubelgiji akiendelea na ziara yake barani Ulaya. Kufika Brussels, Ubelgiji anapokea maombi ya Lissu akiomba waonane.

Kwa moyo wenye upendo alionao Mama Samia unadhani angekataa? Akatae vipi wakati yeye ni Mama wa kila Mtanzania aliyepo ndani na nje ya Nchi yetu?

Akatae vipi wakati yeye habagui? Kwake kila mmoja ni sawa, uwe CCM, ACT au Chadema mbele ya Rais Samia kila mmoja ni sawa.

Wameongea Nini? Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema ni mambo yanayohusu ustawi wa Nchi yetu. Wooow just woow.

Hongera Rais Samia, Hongera Mama yetu, Tuko salama kwenye mikono yako.

Kazi zako, Mipango yako, Upendo wako tuufananishe na nini? Jibu ni hakuna. Wewe ni Samia, Rais wetu na Mama yetu.
Hilo Magafuri hata ungempa miaka 30 ya uraisi asingelifanya kwa Roho mbaya yake yule shatani mkubwa.
 
Back
Top Bottom