matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Moja kwa moja tuokoe muda maana zamani hizi watu wako bize sana na breaking nyuzzz.
1: Wanadhani utajiri ni kunyenyekewa na kila mtu.
Hawa utakuta bila kupiga Magoti Ndugu, kanisa, msikiti, masikini hapewi msaada.
2: Hofu ya kupoteza ni kubwa kuliko hamasa ya kupata zaidi.
Hii ilimkuta msanii Jack Chein alipoingia Hollywood. Wenzake wakitumia nguo hawazirudii zinachukuliwa kwa ajili ya kusaidia watu. Yeye alikuwa anatunza hadi Nguo za ndani. Kumbuka alitokea China ambako hali ilikuwa mbovu kwa Sera mbovu za babu Yao Mao.
3: Wengi hawawezi kudumu katika hali ya utajiri. Watapambana kutumia hovyo hadi warudi katika umasikini bila kujua. Kumbuka Tyson alikuwa na msafara wa Magari na anasa za kila Aina. Ila ndani ya muda mfupi tu akawa masikini wa kutupwa, madeni anadaiwa kuliko mama wa uswahilini ambaye anadaiwa upatu na vikoba hadi anauziwa madera na wenzake.
4: wanaulimbukeni ambao haujali updates. Gari kwa sababu alinunua Benzi enzi zile nchi nzima wakiwa Wawili tu wenye benzi, basi hata leo ambapo kuna latest version ya Benzi atakomaa tu wakati watu wanamshangaa. Hii tabia alikuwa nayo Prof mmoja UDSM. Anaipenda pijoti yake balaa hadi foronya za siti zimeisha lakini haambiliki.
Kama alinunua suti milioni moja mwaka 90, hadi Leo atakomaa nayo tu hata kama ni bwaga kama zile suruali za ngongoti.
5: Wanaamini utajiri ni wake na sio yeye na familia. Utamkuta anazunguka kwenye mahoteli makubwa anakula vyakula vya thamani, wakati mkewe na watoto huko ni ugali mchicha. Nimewahi kwenda kwa bosi mmoja Mkubwa sana wakati wa msosi tunakula ugali sembe na dagaa zimechanganywa na mchicha. Hakuna matunda, juice wala jamaa halijali balanced diet. Tulikula wote yeye, mkewe, watoto na mfanyakazi. Ila jamaa lilikuwa linazuga tu, huko kazini limeshapakia mavitu ya maana .
6: Huwa ni malimbukeni. Kama alikuwa anasali/swali ataacha, kama alikuwa anapenda kusalimia washkaji anawapiga chini wote. Muda wote wanahisi kulogwalogwa tu.
7: hawana skills za kutafuta watu ambao watakuwa msaada siku wakiishiwa. Wanakuwa wamezungukwa na watu ambao wao wanadhani wanawandesha. Au wanawategemea. Ndio wale ambao wakifulia kila mtu anawakimbia. Anabaki na wale ambao hata akiomba 500 ya kununua dagaa Gengeni hawana. Watu wa maana huwa na connection na watu wa kila kada . hata wakiishiwa bado kuna watu wanaweza kumpa Mawazo,mtaji, njia ili asidhalilike.
Ni hayo tu.
Nimekaa sehemu nimetafakari nikasema ngoja nisikae na haya Maneno Kichwani niwatupie watu wanaofikiri nao wachakate