Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Ile ya mama kusema amuka ule na mjomba hii imekaaje kila ukinunua msosi

Mimi nilipitiliza kabisa huko nilikokua naenda,maana yule dogo kila saa maza ake anamwambia hutaki nyonyo nitampa anko anyonyee,nimesubiria weee mwishowe nikamwambia kama unanipa nipe ninyonye nimechoka aiseee.
 
Kukaa na mtu anakulakula hovyo, yani yeye mayai ya kuchemsha, karanga, mahindi ya kuchemsha mara ya kuchoma, yeye kila anachoona lazima kipite mdomoni. Mwisho anaanza kubeua na kujamba hovyo.

Sipendi hiyo tabia!
 
Nikae siti ya nyuma ya dereva, ili nione barabara vizuri...tena kwenye basi unakuwa juu dereva anakua chini hivi. Safari inakuwa safi kabisa, uwe umekaa na mdada mrembo pembeni, story mbili tatu basi safari itakuwa nzuri.
 
Hapa tupo pamoja
 
Hii seat hata mimi huwa naipenda mno ila bahati mbaya huwa siipati.
 
Nikikaajirani na anaerudisha chenji huwa naboweka sana
 
Napenda kukaa siti za mbele,macho muda wote natazama nje kuona milima na mabonde...huku nikiimba wimbo wa tazama ramani kimya kimya
 
Sipendi kula kula njiani, ila najikuta naiga abiria wenzangu tu!
 
Unakakomesha kwa kula na mayai mawili ya kuchemsha halafu unakaambia upepo unakuumiza kifua ndipo unapoachia kitu kinaitwa organic gas from Uvinza
 
Kukaa na mtu anakulakula hovyo, yani yeye mayai ya kuchemsha, karanga, mahindi ya kuchemsha mara ya kuchoma, yeye kila anachoona lazima kipite mdomoni. Mwisho anaanza kubeua na kujamba hovyo.

Sipendi hiyo tabia!
🤣🤣🤣 Hiyo inakera endapo akianza kufanya vitu kama hivyo 🤔
 
Nikae siti ya nyuma ya dereva, ili nione barabara vizuri...tena kwenye basi unakuwa juu dereva anakua chini hivi. Safari inakuwa safi kabisa, uwe umekaa na mdada mrembo pembeni, story mbili tatu basi safari itakuwa nzuri.
Hatari sana Bata zote za safarini unazipitia
 
Unakakomesha kwa kula na mayai mawili ya kuchemsha halafu unakaambia upepo unakuumiza kifua ndipo unapoachia kitu kinaitwa organic gas from Uvinza
🤣🤣🤣 Noma sana
 
Kukaa na mtu anauliza uliza maswali sijui tumefika wapi, bado masaa mangapi.

Nimewahi kukaa na mdada huyo anaongea sana asee hadi ikabidi nivunge nimesinzia ila kila nikiamka analianzisha. Nilikereka sana, safari niliona chungu.

NB: Mimi sio mtu wa stori na kujuana juana.
 
Mi napenda sana kuropoka dereva tumwage.... afu hapo nipo nyuma
Basi utaskia wamama " kuna vijana bangi sana nchi hii"
Mimi ndo naona raha hapo
Unautani na akina mama wewe.
 
Dah kama ni binti wa saizi ungetongoza ili akae kimya
 
Punguza wivu
 
Mimi napenda kukaa na wakaka afu awe mchangamfu kidogo tupige japo stories kidogo safari iwe fupi,kuna safari nilikaa na mkaka tukasalimiana nimekaa gari inaondoka tu nilijiskia vibaya homa hivi, Aisee yule kaka Mungu ambariki. Alinisaidia dawa za maumivu alikua nazo na kila kituo tukishuka alihakikisha ananisubiri niingie kwenye bus nisije kuachwa.nilimuona ni gentleman nikamshukuru.

Sipendi kukaa na wanaoringa sijui, ndiyo introverts kuna dada nilikaa naye picha linaanza mimi nimepandia Ubungo seat ya dirishani, kufika mbele dada kapanda tena hata salamu hamna eti anataka nitoke hiyo ni seat yake, nikamwambia hii ni seat yangu bana, akaanza kusema kaweka booking sijui, konda akaja kumaliza utata, dada akaambiwa hiyo seat no ni seat hiyo nyingine si dirishani akanunaa akakaa , jamani hatujaongeleshana hadi tunafika Mbeya😜 na vile sijazoea nilikoma😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…