Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Mara kadhaa nadhani nimesafiri safari ya zaidi masaa 13 bila kuongea neno.

Uwa sili njiani zaidi ya maji niliochanganya k vant.
 
Kuna kamoja kalinitapikia Kuanzia mbezi hadi mutukula.
Yaani kanatapika alafu kanaagiza tena mavitu barabarani.

kakilala kakiamka " Baba tumeshafika Bukoba?' wakati tuko mdaula
Qmmk unaeza kumuomba konda ukae kwenye godoro mbele
 
Mtu anganganie kukuuliza maswali kama huko unapoenda unafikia wapi etc ..
 
Je, ni Tabia Gani hupendi au unapenda ukiwa safarini

Binafsi Napenda kukaa na binti nikiwa safarini ila asiwe na Smartphone kubwa kunizidi,
Utakuta wewe una Tecno pop2 F harafu yeye ana iPhone 13.
Yaani unakuwa unaona aibu hata kuitoa.

Unakuta kabinti kanajikuta kako busy na Simu kameweka earphone hakatoi ukikakaribisha mhindi unaona kanatoa earphone sikio moja harafu kanajibu "Ahsante stumiagi mimi" na wakati kanaelekea Usukumani


Binafsi hiyo tabia sipendi
[emoji23]safari ni kula
 
Sipendi tabia ya baadhi ya watu kupayuka hovyo kwenye gari utadhani wapo wapi sijui.

Unakuta wamekaa siti tofauti ila wanapiga kelele yaani ni kero mno.
Kuna wale wanaongelea kwa sauti mambo ya nyumbani kwao kwenye bus, wanakera sana

Unakuta mama anamwambia binti wa kazi tunakuja tupo njiani, hakikisha umepika hiki na hiki, halafu mjaze maji kwenye jaba eeh

Jana usiku mlikula nini? Hamjanimiss na wanacheka cheka sana

Mara Baba yenu yupo hapo mumpe simu nimsalimie Mume wangu???

Yaani mambo ya nyumbani kwao wanaongea kwa sauti kama vile yanatuhusu na sisi.

K E R O K U B W A
 
Kwanza nikae kwa dirisha,halafu awepo slay Queen pembeni.Hapo hata awe matawi ya safu za milima Everest Nepal huko,atanikubali tu hizo swagg zangu.Picha linaanza kwanza namlia tinted hamna cha salam wala nini.Ni earpods tu zipo kwa sikio nakula ngoma,pipi classic mojamoja natumia na maji kwa mbaali.Mida ya chai nakunywa,narudi na apples matunda.
Nasema mpaka atanisemesha tu.
Huku nacheza video kwa simu huku nachat,lazima atashangaa tu.Mara niingie Google map nione nipo wapi na jinsi gari ina move.

Atanisemesha tu.
Muda wa lunch ni chips kuku,na Ceres tropical napanda nayo,na redbull na maji kubwa.Hivi navitumia kwa akili sn kidogo kidogo ili visifanye nikojoe kojoe.Atanisemesha tu.

Mara simu yake charg inaisha,anaazima USB achaji anakuta ni ya kitofautiiiii,atanielewa tu.

Saa moja usiku atakuwa hoii,ataanza kunilalia,uchovu hamu ya kiwa holded itamuingia.Hapo ndo namwambia tukifika nikutafutie maji ya moto uoge et ee? Upate na chai nzuri sawa? Hapo ni sawaaaa!

Itaendelea.....
We unakunywa Ceres tropical hii yenye sumu? Huwezi nibabaisha sana sana ntakuona mshamba tu[emoji16][emoji16][emoji38]. Joke mkuu
 
Unanikumbusha siku naenda zangu Iringa nikapanda basi fulani hivi ile kuingia kwa seat yangu tu nikakutana na mdada amejazia kalio la uhakika ila sura ya kawaida
Nikamsalimia then nikalopoka "aise afadhari hata nimekukuta wewe walau safari yangu itakuwa nzuri"
Akatabasamu na kuniuliza kama vile hajanisikia eti umesema..!??
Nikarudia maneno yale yale
Akacheka na kuniuliza kwanini unadhani safari yako itakuwa nzuri?
Nikamjibu nimekaa karibu na dada mzuri [emoji3]
Unajua kiliendelea nini?
Nilijilia vyangu mpaka kesho yake ndo tukaachana
Yaaan alikupa maku just kwa kumsifia?[emoji849][emoji849][emoji849] Huyo demu msengeee
 
Abiria jirani kutaka kunijua saaana na kuomba namba,, keroo mnatakiwa kujua si mara zote mtu Yuko safari kwa matembezi manake hizi ndo zenye raha, wengine safari ni za majonzi, mahangaiko nk kuuliza uliza habari za mtu Ni kumuongezea mahangaiko na makasiriko
Au dereva yaan ni anakuanza ubungo kuomba namba au kukuzoea[emoji849]
 
Back
Top Bottom