Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Tabia gani hupendi au unapenda ukiwa safarini?

Napenda kusikiliza mziki huku nikicheza game kwa simu.
Sipendi kula kula hovyo. Sana sana huwa ni biskuti na maji + muhindi wa kuchoma.
 
1. Kama naendesha gari basi huwa sipendi kutembea mwendo mdogo, kufunga vioo

2. Kama ni usafiri wa basi, treni, boti, meli, ndege huwa sipendi kukaa siti moja na mtu yuko na smell weird, anakula kula hovyo, anauliza uliza maswali au kuongea sana...
 
Sitasahau siku niliyokata tiket siti ya katikati nyuma kabisa usawa wa korido nilikua wa mwisho kuingia ndan ya bus, nilikuta wamama wa 4 wamebanana hatari. asee niliishia kucheka tu, Siti za watu 5 wamekaa watu 4
🤣🤣🤣 unatamani hata kurudishiwa nauli.
 
Kila nikipanda gari lazima nikae na mwanaume mwenzangu na akiwa mwanamke lazima awe mmama au mzee. Nakereka😅

Sipendi shobo wala stori na mtu nikiwa kwenye safari kila mtu ajue yake
Siku moja moja omba wakuweke na watu tofauti na hao.
 
Abiria jirani kutaka kunijua saaana na kuomba namba,, keroo mnatakiwa kujua si mara zote mtu Yuko safari kwa matembezi manake hizi ndo zenye raha, wengine safari ni za majonzi, mahangaiko nk kuuliza uliza habari za mtu Ni kumuongezea mahangaiko na makasiriko
Kuna wengine hua wanabahatika wakiwa kwenye usafiri hivyo ni kutest tu Huenda bahati ni yako siku hiyo.
 
Huwa napenda kukaa siti ya dirishani, napenda sanaaaa. Yani ikotokea siku nimepanda kwenye basi alafu sijakaa dirishani kwa kweli huwa makosa amani kbs, sioni Raha ya safari.
Huu ugonjwa ni asilimia kubwa ya abiria wa kwanza Mimi
 
Udhaifu huo.
Binti akija akute nimekaa akae kimya kimya wala sina habari hata kama tutasafiri masaa 20 i don't care wala simuongeleshi

Aje akae namimi yuko bize na simu yake wala sina habari namuona msukule tu

Tabia inayonikela ni mtu kutaka kunijua nafanya shughuli gani, yaan kutaka kunijua kiundani ni jambo ambalo silipendi kabisa tena kwa mtu tuliyekutana kwa mara ya kwanza.

Nishawahi kudate na mwanamke almost mwaka na tukaachana mpaka leo hajawahi kujua nafanya shughuli gani
Hii imekaa vizuri kuepuka kujulikana.
 
Napenda kusikiliza mziki huku nikicheza game kwa simu.
Sipendi kula kula hovyo. Sana sana huwa ni biskuti na maji + muhindi wa kuchoma.
Kweli hata mimi kura kwenye Safari sijajaliwa kabisa
 
1. Kama naendesha gari basi huwa sipendi kutembea mwendo mdogo, kufunga vioo

2. Kama ni usafiri wa basi, treni, boti, meli, ndege huwa sipendi kukaa siti moja na mtu yuko na smell weird, anakula kula hovyo, anauliza uliza maswali au kuongea sana...
Imekaa vyema sana hiyo
 
Back
Top Bottom