Mimi napenda kukaa na wakaka afu awe mchangamfu kidogo tupige japo stories kidogo safari iwe fupi,kuna safari nilikaa na mkaka tukasalimiana nimekaa gari inaondoka tu nilijiskia vibaya homa hivi, Aisee yule kaka Mungu ambariki. Alinisaidia dawa za maumivu alikua nazo na kila kituo tukishuka alihakikisha ananisubiri niingie kwenye bus nisije kuachwa.nilimuona ni gentleman nikamshukuru.
Sipendi kukaa na wanaoringa sijui, ndiyo introverts kuna dada nilikaa naye picha linaanza mimi nimepandia Ubungo seat ya dirishani, kufika mbele dada kapanda tena hata salamu hamna eti anataka nitoke hiyo ni seat yake, nikamwambia hii ni seat yangu bana, akaanza kusema kaweka booking sijui, konda akaja kumaliza utata, dada akaambiwa hiyo seat no ni seat hiyo nyingine si dirishani akanunaa akakaa , jamani hatujaongeleshana hadi tunafika Mbeya😜 na vile sijazoea nilikoma😂