vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Habarini,
Kuna tabia imejengeka kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya (hospitali, zahanati, vituo vya afya) ambapo mteja baada ya kumaliza kuhudumiwa, analazimika kuacha karatasi ambayo ina taarifa za msingi kuhusu mgonjwa husika.
Karatasi hiyo inakuwa na taarifa za aina ya vipimo na majibu ya vipimo lakini unalazimishwa kuacha wanakwambia ni mali yao. Ukiandikiwa dawa basi hospitali zingine wanakulazimisha ununue hapo hapo dawa, hawakupi karatasi ya dawa ili ukanunue kwengine.
Hili jambo ni kumnyima haki mgonjwa kwasababu yeye ana haki ya kununua dawa popote pale anapoona pana unafuu kwake. Msifikirie kibiashara tu bali angalie na utu kwa mgonjwa.
Kwa upande wa karatasi yenye vipimo na majibu ya vipimo pia ni haki ya mgonjwa kupewa kwasababu ataitumia siku nyingine kama reference pindi akienda hospitali nyingine kupata matibabu kuwa kuna huduma ilishawahi kufanyika. Na pia ni muhimu kwa mgonjwa kuweka kumbu kumbu.