Mkuu Jacobus, kwanza pole kwa hayo yaliyotokea.
Kwa sisi tunaomjua Ufoo Sara, ni mwanadada wa shoka kweli kweli na yuko poa sana!.
Kwa hayo uliyoelese, naomba nikuombe samahani kabla kwa sababu siamini kama ni kweli kilichotokea ni hiki ulichoeleza.
Haiwezekani mtu aje na kujichomolea tuu tv, kuna jambo behind ambalo wewe ama ulilisikia na hukulieleza kwa makusudi ama hukulijua kuwa lilitokea kabla na hali lazima ilikuwa hivi
- Lazima huyo dada aliwaona wahusika kabla na kuomba idhini ya kucharge laptop yake!.
- Alielekezwa hapo ilipo tv ndio the only swich socket inayofanya kazi na kuruhusiwa kwenda kuchomoa TV.
- Kwa vile lengo lilikuwa kuwahisha story kwa kuripoti live kwenye habari, due to pressure, alighafilika na kusahau kuwaomba radhi nyinyi mliokuwepo, kughafilika ni ubinaadamu pia!.
- Huyu ndie mwandishi aliyezunguka nchi nzima ndani ya helcopter ya Mbowe ile 2010 wakati mwenzake Makunga alizunguka na CCM! nadhali malipo ya Ufoo Saro baada ya kuwafanyia Chadema very positive reporting unayajua!. na ya Makunga pia unayajua!.
- Nakubaliana na wewe, wako watangazaji wa TV wanaojisikia sana na kujiona wao ni ma celeb, lakini wako watangazaji wengine tuu tena ni wazuri ila hawajisikii kabisa na kujihesabu wao ni watumishi wa watu!. Ofoo Saro, yuu mmoja wa Watangazaji hao!.
Pasco.