Ntiyakama
Member
- Sep 19, 2021
- 32
- 37
Kuvimba miguu au mikono (peripheral edema)
Edema ni uvimbe unaoonekana kwa macho unaotokana na mkusanyiko wa vimiminika ndani ya tishu za mwili.
Uvimbe huu hutokea mara nyingi kwenye nyayo, ankle, miguuni na mikononi ambao huitwa “peripheral edema.”
Uvimbe huu ni zao la kujikusanya kwa majimaji ya ziada chini ya ngozi kwenye nafasi zilizomo kwenye tishu za mwili.
Majimaji mengi ya mwili yanayopatikana nje ya seli hutunzwa ndani ya maeneo ya aina mbili; mishipa ya damu kama “serum” na kwenye nyufa zilizo nje ya seli “third spaces”.
Sababubu za kuvimba kwa miguu zinaweza kuwa rahisi tu kama kukaa au kusimama kwa muda mrefu na kutofanya mazoezi (being inactive). Baadhi ya magonjwa pia husababisha tatizo hili.
SABABU ZA KUVIMBA MIGUU
‘Edema’ hutokea pale mishipa midogo ya damu iitwayo kapilari inapovujisha majimaji. Majimaji hayo hujikusanya kwenye tishu za karibu na kusababisha uvimbe.
Sababu za muda mfupi (temporary causes).
a) Kusimama au kukaa pahala pamoja kwa muda mrefu.
b) Kula chakula chenye chumvi nyingi.
c) Kuumia (kuvunjika, kuteguka n.k).
d) Alegi (kung’atwa na wadudu au wanyama, kuchomwa na miiba au vyuma).
e) Kuvuaa nguo zinazo ban asana (eg. Nguo za ndani).
f) Unene uliopitiliza (Obesity).
g) Kuwa karibu na kupata hedhi (kwa wanawake).
h) Ujauzito (kwa wanawake)
Sababu zisizo eleweka (Idiopathic cause).
Edema huweza kuwa ni matokeo ya kutumia baadhi ya dawa, kama:
• Dawa za pressure
• Dawa zinazozuia kufyonzwa kwa Ca (Calicium channel blockers)
• Steroids
• Mineralcorticoid (eg. fludrocortisones)
• Madawa ya homoni
• Baadhi ya dawa za kisukari (eg. thiazolidinediones)
Kwa kuvimba miguu kunakosababishwa na matumizi ya dawa; wasiliana na mtaalamu wa afya aliyekushauri kutumia dawa husika juu ya tatizo hilo.
Mara nyingine, edema huwa ni ishara ya magonjwa mengine ya hatari. Baadhi ya magonjwa hayo ni:
• Magonjwa ya Moyo,
• Magonjwa ya Ini (Cirrhosis)
• Magonjwa wa Figo.
• Udhaifu au uharibifu wa veni za miguuni.
• Tatizo katika mfumo wa limfu (Lymph system)
• Upungufu mkubwa na wa muda mrefu wa protini.
Uvimbe Unaobonyea – Pitting Edema.
Uvimbe unaobonyea (pitting edema) hugundilika kwa kubonyeza eneo la mwili lililovimba kwa kidole.
Endapo eneo hili liltaacha kijishimo kinachodumu kwa muda baada ya kidole kuondolewa, edema hii huitwa pitting edema.
Mgandamizo wa aina yo yote, hata unaotokana na kuvaa socks, unaweza kusababisha kubonyea endapo mtu ana pitting edema.
MATIBABU YA KUVIMBA MIGUU
Matababu yasiyo husisha dawa (Non pharmacological)
Matibabu ya hali hii hutegemea sababu haswa ya uvimbe wenyewe. Kwa uvimbe ambao ni matokeo ya ugonjwa, matibabu ya ugonjwa husika yatasaidia kuondoa uvimbe.
Kwa uvimbe uliosababishwa na mitindo ya maisha au sababu za muda mfupi, zipo njia nyingi zinanazoweza kuleta nafuu/kupona;
a) Inua miguu yako juu usawa wa moyo; unaweza kulala ukiwa umeweka mto chini ya miguu yako ili kuifanya miguu iinuke juu kidogo ya usawa wa moyo wako.
b) Fanya mazoezi
c) Inapokulazimu kukaa au kisimama kwa muda mrefu; pata vipindi vya kujipumzishwa kwa kutembea tembea kidogo
d) Punguza kiwango cha matumizi ya chumvi
e) Sugua taratibu (massage) mguu uliovimba kuelekea ulipo moyo (kutoka chini kwa kupanda juu)
f) Punguza uzito kama, una uzito uliopitiliza
Zingatia;
Ongezeko la kiwango cha Sodium (Na) mwilini, hupelekea ongezeko la mlundikano wa maji katika tishu za mwili; chumvi (NaCl) hukadiliwa kuundwa na 40% ya Sodium.
Kiwango cha Sodium kinachoshauriwa kiafya kwa siku ni 2,300mg wastani wa “kijiko 1 cha chai”.
Inakadiliwa kuwa 75% ya chumvi itumikayo, hutoka katika “vyakula vya viwandani” na 25% tu ndio ipatikanayo asilia katika vyakula au wakati wa kuunga chakula kinapo andaliwa.
Kupunguza matumizi ya chumvi ni sambamba na kupunguza kiwango cha Sodium kinachoweza kubakia mwilini.
Ni vyema kuhakikisha unavitambua na unaepuka kutumia au kutumia kwa uangalifu vyakula vyenye chumvi kwa kiasi kingi;
Vifuatavyo ni miongoni mwa vyakula vyenye kiasi kingi cha Sodium; nyama au samaki zilizobanikwa, nyama za kwenye makopo, nyama choma, biscut, mikate, ngozi ya nguruwe, vyakula vilivyogandishwa, tomato sauce, mboga zamajani za kwenye makopo, pizza, sosegi, jibini (chees)
Fika Hospitalini kwa msaada zaidi pale ambapo;
Unapo dalili zingine zinazo ambatana na kuvimba miguu, kama vile; maumivu ya miguu (kuhisi miguu kama inawaka moto, kuona ngozi ya eneo lililovimba likiwa ang’avu na lenye wekundu huku likiongezeka joto zaidi), tumbo, kifua na kichwa
Pia unapohisi kuwashwa, kushindwa kupumua vizuri, kizunguzungu, kushindwa kuona vizuri, kuhisi ganzi miguuni na kuhisi kuchanganyikiwa.
Afya yako ipo mikonono mwako. Chukua hatua.

Upvote
1