KERO Tabia ya Gari za Abiria Barabara ya Mbeya - Kyela (Kilometa 120+) kubeba Abiria kuliko uwezo ni hatari kwa usalama

KERO Tabia ya Gari za Abiria Barabara ya Mbeya - Kyela (Kilometa 120+) kubeba Abiria kuliko uwezo ni hatari kwa usalama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Magari ya abiria ya Barabara ya Mbeya kwenda Kyela, hapo namaanisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine yanajaza sana abiria tofauti na uwezo wake.

Gari hizo zimekuwa na utaratibu wa kutoa Viti vya katikati kisha wanasimamisha abiria, fikiria umbali wa zaidi ya Kilometa 120 Watu wanasimama ndani ya gari.

Uwezo wa gari hizo ni kubeba abiria 29 lakini maajabu yake gari hizo zinabeba zaidi ya Abiria 40.

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani siyo kwamba hawaoni bali wao wanakunja buku mbili kisha wanaruhusu gari iendelee na safari.

Inawezekana ikaonekana ni kitu cha kawaida kwa kuwa hakuna tatizo lililotokea lakini siku ikitokea inakuwa sio salama zaidi kwa vyombo na wahusika wenyewe waliopo ndani ya gari.
DSC_0593.JPG
DSC_0596.JPG

 
Magari ya abiria ya Barabara ya Mbeya kwenda Kyela yanajaza sana abiria tofauti na uwezo wake

Gari hizo zimekuwa na utaratibu wa kutoa Viti vya katikati kisha wanasimamisha abiria .

Uwezo wa gari hizo ni kubeba abiria 29 lakini maajabu yake gari hizo zinabeba zaidi ya Abiria 40.

Askari wa kikosi Cha usalama Barabarani siyo kwamba hawaoni bali wao wanakunja buku mbili kisha wanaruhusu gari iendelee na safari.
Mbona ni kama wananchi wanapenda na wanataka kuwai 😅
 
Back
Top Bottom