A
Anonymous
Guest
Mimi ni mchimbaji mdogo katika moja ya Vijiji katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya, kero yangu ni kuwa kumekuwepo na tabia ya mazoea ya kuchoma dhahabu mbichi kwa moto wa mkaa katika hizi buying center nyingi za huku Chunya, jambo ambalo ni hatarishi kwa afya za wachimbaji.
Mvuke wa zebaki (Mercury) kutoka kwenye dhahabu inayochomwa ni sumu hatari sana kwa watu wote wanaokuwa eneo la vituo vya kununulia dhahabu.
Kisheria Tume ya Madini inakataza uchomaji dhahabu kiholela (Open-air burning), kila kituo cha ununuzi kinatakiwa kutumia kifaa kinachoitwa Retort.
Hali hii ni hatarishi na kwa kuwa jamii nyingi ya wachimbaji hawana hii elimu wako katika hatari kubwa sana ya kiafya.
Madhara ya hii mercury vapor:
1. Kutetemeka kwa mikono na mwili (Tremors)
2. Matatizo ya uzazi
3. Kichwa kuuma
4. Kifua kubana na kukohoa kwa kila wakati