Tabia ya kukodolea macho simu za watu

Tabia ya kukodolea macho simu za watu

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
602
Reaction score
969
Hii tabia huwa inanikwaza sana halafu ni ya wengi sana! Upo kwenye daladala unatoa simu ujibu meseji au kuanglia kama kuna jipya, sasa jirani yako bila aibu anakodolea macho kwenye simu utadhani inamuhusu!

Unaandika meseji yeye anafuatilia na kusoma unachoandika!

Tuweni wastaarabu jamani
 
Nunua starlet yako bwana tusipangiane matumizi ya macho yetu.

[emoji23][emoji23][emoji23] mwenyewe hako katabia nilishawahi kukafanya sana. Kuna siku niliona kajamaa akanamtext mke wa mtu, nilijua kuwa anachati na mke wa mtu pale alipomtumia text ya kusema nakuona umeingia na mumeo.

Alipotuma text ikaingia kwa mdada yupo siti ya nyuma simu yake ikaitika ikiinyesha kuna notifications...!

Naomba niishie hapo ila Kikubwa tu watu wawe wanaficha hizo simu zao mie macho yangu huwezi nipangia wapi niangalie kipi nisiangalie[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuza maandishi ya simu, type bonge la tusi kumtukana anaechungulia simu yako... iwe kama draft tu..kila ukiona anakutolea macho unamuwekea hilo tusi.
 
Kuza maandishi ya simu, type bonge la tusi kumtukana anaechungulia simu yako... iwe kama draft tu..kila ukiona anakutolea macho unamuwekea hilo tusi.

We kuza maandishi ujuavyo ila bado nitakodolea macho simu yako kama wewe unaziweka weka wazi chat [emoji189] zako.
 
[emoji38] [emoji38] wewe unasema hiyo, mimi niliishaporwa simu na dada mmoja kisa nimescroll post fulani instagram ikimuonyesha mobeto, aisee nilishangaa ujasiri wa yule dada.

basi vile ni mambo ya wadada kuangalia celebrities nikamkaushia.
 
Kuna siku ilishawahi nitikea hii nikiwa kweny Daladala. Naandika sms tena kwa Group naona mtu amekodolea tuu ninachoandika nilivyomaliza kuandika nikaandika sms nyingine akiwa anaiangalia nikaandika ivii


KUNA ABIRIA NIMEKAA NAYE ANAFUATILIA SMS BILA HATA AIBU, VP NIMCHUKULIE HATUA GANI?

Daaah mjinga yule aliona aibu balaaa
 
Kuna siku ilishawahi nitikea hii nikiwa kweny Daladala. Naandika sms tena kwa Group naona mtu amekodolea tuu ninachoandika nilivyomaliza kuandika nikaandika sms nyingine akiwa anaiangalia nikaandika ivii


KUNA ABIRIA NIMEKAA NAYE ANAFUATILIA SMS BILA HATA AIBU, VP NIMCHUKULIE HATUA GANI?

Daaah mjinga yule aliona aibu balaaa
Mimi nitaandika "kuna ngedere hapa anasoma msg zangu"
 
Ndio ipoje hiyo mkuu ??

[emoji419]Ni km protector zile za glass ila yenyew imetengenezwa kwnye mfumo kwmba utaweza kuona kinachofanyika kwnye simu only if uko usawa wa 90° kutoka usawa uliowekwa simu, pia utweza kuona kama uko umbali wa 30CM plus hzo nyuzi 90°kutoka kwnye usawa ulioshika simu.

[emoji419]So ukiwa umesimama na mwana amekaa utakua umezidi 30cm hvyo hutoweza kuona mtu anaandika nn ama anafanya nn kwnye simu yake.

Zipo za aina mbili (i)BLACK//TINTED

(ii) COLORLESS/PLAIN

[emoji419] Hiyo inamaana kwamba hata abiria mwenzako kwnye seat HATOWEZA kuona unachokifanya zaidi ya kuona giza tuu, kwasababu atakua ameshazidi nyuzi 90° kutoka usawa uliowekwa simu.

[emoji1630]Kwenu nawasilisha [emoji1630]
 
Hii tabia huwa inanikwaza saana halafu ni ya wengi saana! Upo kwenye daladala unatoa simu ujibu meseji au kuanglia kama kuna jipya, sasa jirani yako bila aibu anakodolea macho kwenye simu utadhani inamuhusu! Unaandika meseji yeye anafuatilia na kusoma unachoandika!

Tuweni wastaarabu jamani
Huyo wa kuangalia kioo cha simu yako ana nafuu.

Je yule anayekukodolea macho kukufuatilia ama kukushangaa unapokuwa unasorolea maumbile yanayotamanisha ya mwanamke apitaye mbele yaako!

Yaani umevutiwa na uzuri wa mwanamke, unaona ustarehe kwa kumwangalia, halafu unashitukia pembeni kunajitu linakuchora jinsi unavyoumia na kudhalilika kwa tamaa mzee mzima!

Hiyo tabia ni ya kishenzi afadhali hata mtu anaye chabo sms zangu isee!
 
Back
Top Bottom