Tabia ya Watanzania kupenda michango

Tabia ya Watanzania kupenda michango

Hii ni legacy ya Nyerere na sera zake za ujamaa

If we could go back in time ningetamani Kambona afanikiwe kupindua serikali ya Nyerere na kuintroduce capitalism from the 60s. Hii mentality ya kuombaonba hovyo kila ukiwa na shida isingekwepo.

Kila mtu aishi kwa uwezo wake, kila mbuzi ashibe kwa urefu wa kamba yake.
For sure mkuu ni mentality mbaya sana ...Ila kwa wazembe hawawez kuelewa
 
NILISHAWAHI KUTEMBEA NA HELA YA MCHANGO WALIYOTOA WATU
NILIJIPATIA NAULI NKATAMBA,NYUMA NLIWACHIAA VILIOOOO

OVA
 
Siku hizi mpaka makanisani watu wanapangiwa kiasi cha kutoa na utoaji wako ukiwa hauridhishi utajua kwa nini Yesu ni Bwana!.
Ha ha ha ha [emoji23][emoji38]
 
Kama una mgonjwa anayehitaji fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ntachangia,kama umekwama ada ntakuchangia,kama umepata msiba wa karibu ntakueezesha kidogo,ila kama ni harusi,kipaimara,graduation,birthday party,au sherehe nyingine yoyote ya anasa sitakuchangia!! Sitoi hata mia!
🤣
 
Kama una mgonjwa anayehitaji fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ntachangia,kama umekwama ada ntakuchangia,kama umepata msiba wa karibu ntakueezesha kidogo,ila kama ni harusi,kipaimara,graduation,birthday party,au sherehe nyingine yoyote ya anasa sitakuchangia!! Sitoi hata mia!
Ulichoandika ndicho nami nakifanya, nachangia sana matatizo kama misiba au ugonjwa ila sherehe sijawahi kuchangia kabisa. Uko sahihi mkuu na najifeel good kuona tupo wengi kumbe.
 
Hii ndiyo dawa. Na siku hizi wanawake wa uswazi wanajifanya kuwa wazungu kuliko hata wazungu wenyewe. Wengi hawajaenda shule hivyo wanakuwa rahisi sana kuingia kwenye mkumbo. Kitu kama birthday uswahilini imekuwa kama ni lazima. Kuna mama mmoja darasa la saba ukimsikia anavyozitamka sasa. Utasikia ''nilikuwa kwenye basi-dei ya jirani yangu''. Wamejua mpaka baby shower wewe unafikiria mchezo. Kweli ukitaka kujua gharama za ujinga nenda uswahilini huko uone kina mama wanavyoshindana na sherehe.
Naked truth, umesema kitu cha ukweli kabisa mkuu. Pata like yako
 
Mfano hii michango ya harusi imeshachosha sana.

Waoaji au waonaji wapya, badilikeni kidogo. Andaa shughuli ndogo kabisa gharamia, usafiri wako, mavazi yenu, gharama za ukumbi mdogo, then alikeni watu waje kuwapongeza kwa zawadi mbali mbali, huo ndiyo uungwana. Watu wa karibu tu.

Ikitokea zawadi ni nyingi na zenye thamani kuliko gharama mlizotumia kuandaa shughuli basi tutasema shughuli yenu ilikuwa na mafanikio makubwa.

Maisha yamekaba punguzeni hizi mambo za michango isiyo ya lazima, tubadilike sasa!!
 
Setting ikoje hiyo nami nifanye? Yani juzi kuna mtu nimempa namba kesho yake tayariii nipo group sijui jumuiya ya mtakatifu gani tayari anaomba michango nikabaki...,😳
Angalia kwrnye setting yako nenda privacy
 
Juzi kulikuwa na harusi ya mtangazaji fulani
Basi hiyo michango ilikuwa balaaa

Sasa ukiangalia mpaka sahv mshafanya harusi mmetumia mamilion,what's next?

Ova
 
ila kweli kule kwenye kitochi hufuatwi hovyohovyo
Saana wanaunganishana kwenye wasapu na kukumbushan kwenye wasap pia. So ukiwa na kitochi unateleza tu mpaka mtu akukumbuke sio leo wala kesho
 
Habari wadau,

Leo nimepata muda kujiuliza hivi hii tabia ya Watanzania (walio wengi) au jamii yetu kupenda sana tabia ya kuanzisha michango na kuchangia tumeipata wapi? Au ni ile toka enzi za siasa za ujamaa na kujitegemea?

Sipingi kuchangia mambo muhimu, ni jambo jema sana kuchangia mambo muhimu ya maendeleo.

Lakini hivi sasa tabia hii imezidi kwa kweli. Najua kuchangia si lazima ni hiari Lakini imekuwa too much!

Kila group la whatsup likianzishwa, wiki ya kwanza ya pili mchango. Wanasiasa kitu kidogo, wananchi tunaomba mchangie kidogo. Tabia hii mpka serikali kupitia viongozi wake, wanahamasisha michango, huku wakizitafuna kodi bila kujali.

Leo mtu anafungua kesi mahakamani ambayo haina gharama zozote zaidi anahamasisha umma umchangie.

Nina magroup ya whatsup takribani Matano baada ya kuyapunguza sana, lakini bado nikimaliza mchango huu, group lile linaleta michango miwili au zaidi. Matatizo ni yale yale.

Tupunguze haya mambo jamani.
Weka setting wasap ambayo mtu hawez kukuunga tuu na grp kiholela..tangu nmelijua hilo lawama zimekua nying..et oooh mbona hatuwez kukuunga kwenye grp kiongoz.nawambia aisee hata mim sjui kwann...hahahahah
 
Weka setting wasap ambayo mtu hawez kukuunga tuu na grp kiholela..tangu nmelijua hilo lawama zimekua nying..et oooh mbona hatuwez kukuunga kwenye grp kiongoz.nawambia aisee hata mim sjui kwann...hahahahah
Ndio utuelekeze vizuri tuweze kujua mkuu....ukisema juu juu sio kila mtu anajua.
 
Niliacha kutumia smartphone sababu ya haya ma group ya michango.
 
Mimi ukiniunga group naleft hapo hapo. Kuna siku nashtukia nimeungwa kwenye group la niliomaliza nao sec nilileft within a second.
Hehehe kwenye setting kiboko yao hakuna kuungwa hovyo
 
Back
Top Bottom