Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Tuseme masikini anapenda ngono kuliko tajiri. Mawazo yake yote ni ngono na sio uchumi. Bara la Afrika masikini wapo wengi sana ndio maana ongezeko la watu ni kubwa.
Afrika hakuna watu kama Asia,Amerika na Ulaya.Afrika watu ni wachache sana na mapori ni mengi ambayo watu wanastahili kuishi ila idadi ya watu ni tatizo.
 
Waarabu hapa hapa Tanzania wanazaana mpaka 40 na baba mmoja ila sio masikini.
Laumuni vichwa vyenu.
Wana visima vya mafuta! Wana viwanda,Wazungu wame invest kule,wana mipango mizuri ya maendeleo!
Vipi kwetu?
 
Kwa mwendo huu hakuna Rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote?

Unakuta bodaboda ana watoto 6? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasababu watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dkt. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Halafu tutailaumu serikali wakati tunaona kabisa kwenye jamii watu wanazaliana Kama simbilisi

Hata kuambiana ukweli tu mtaani hatutaki…. Lakini tutakuja kulaumu serikali
 
Kwa mwendo huu hakuna Rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote?

Unakuta bodaboda ana watoto 6? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasababu watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dkt. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Kwani,mara ya mwisho hatukuambiwa tufyatue watoto tu serikali itatufanyia wepesi?Au kauli ilifutwa?
 
Wana visima vya mafuta! Wana viwanda,Wazungu wa invest kule,wana mipango mizuri ya maendeleo!
Vipi kwetu?
Ndio nasema kaka sisi tuzilaumu akili zetu.
Ila kuzaa sio chanzo cha umasikini,mbona kuna waswahili hapahapa Tanzania wamejipata na wana watoto 7 mpaka 12 huko!??
Tulaumu akili zetu,sisi pia tuna madini ya kutosha,gesi asilia ya kutosha ya kutumika karne nzima,rasilimali misitu,rasilimali wanyama.
Hivi vyote kama tungeweza kuvitumia vizuri kama wanavyotumia waarabu tusingelalamika umasikini.
 
Kwa hilo hata ukisimama juu ya mlima Kilimanjaro sidhani kama watakusikiliza!
Pamoja na jitihada zote za serikali kuelimisha katika Mpango wa Uzazi,bado hawa maadui watatu wanaliandama Taifa letu-Ujinga,Umasikini na Maradhi.
 
Sisi wenye uwezo wacha tuzalishe tu maana mashoga wanaongezeka kwa kasi ya ajabu tukileta uzungu wa kuzaa watoto wawili tumekwisha.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan had muhusishe mashoga ndo roho zenu kwatuuu.
Woiiiiih, muwe mnawapa matunzo na malezi sahihi, isijekua ndo mnaongeza wingi wa mashoga.
 
Na mimi nashangaa, mtu hana kipato cha kueleweka ila chini kulivyo active!! Utasema tumempa tenda ya kuongeza watanzania [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimeshangaa huyu makamu wa rais aliyefariki juzi hapo nchi jirani ana watoto wawili yule mjeshi hapo kwa uhuru aliyepotelea kwenye ukungu naye aliacha watoto wawili.

Mamndenyi nina watoto wanne naona nilifeli sana ningezaa hata nane.

Watu wazae watoto wengi
 
Unamaanisha watu milioni 2 ndio wanalipa kodi, umesahau hata ukinunua tu maji ya kunywa kuna kodi unalipa moja kwa moja?
 
Back
Top Bottom