Tabia ya watu kuniomba pesa kuwaacha wenye pesa inatokana na nini?

Una nyota ya umama huruma

Wala hufanani na jambo hilo , una mambo wewe
 
Nina mpango wa kuwa mchoyo sasa
Hiyo ndio dawa, wakishona unawabania wanaacha wenyewe. Mimi nilizoea kutoatoa baadae nikashtuka baada ya kupiga mahesabu, nikaona sehemu kubwa tu ya kipato changu cha mwezi naishia kuwapa watu.
Nikasitisha rasmi, labda mtu awe yuko hospitali anahitaji hela ya dawa, kinyume na hapo sina hela.
 
Habari za majukumu wadau wenzangu.

Nimekuwa nikiombwa hela na watu tofautitofauti tangu nikiwa Mdogo kabisa. Nilipokuwa nasoma shule, nikirudi likizo watu huniuliza una buku hapo?

Hadi leo nahangaika na maisha yangu bado mizinga ni mingi. Mfano kuombwa Shililingi 200, 500, 1000, 5000, 10000 na wengine wakizidi hapo watajifanya wanakopa na hawanirudishii.

Kuna watu mtaani na hata ndugu zangu wenye uwezo kuliko mimi lakini siwaoni wakiombwa hela na watu. Nimewahi kuwauliza wakasema hakuna anayethubutu kuwaomba hela.

Hapa Kuna mtu ananisumbua tangu jana anaomba elf tano tu. Mwezi wa pili nilimpa elf 12 bure kabisa. Sasa karudi tena. Hali hii inatokana na nini? Napatwa na wasiwasi.
Yaani wewe mjomba upo kama mimi inanitokea mimi hivyo mara nyingi,juzi bro mmoja anamiliki gari kali na mjengo wa maana alikuwa na binti yake akanipga mzinga yupo dogo ninunulie bia basi na sina mazoea naye na mbele kidogo nikakutana na mama wa heshima kabisa akasema naomba elfu mbili ukimuangalia unakataa kwamba hivi kweli au yaani inanikuta mara kibao
 
Mkuu unanitia moyo wakati Mimi imefikia hatua nawafokea!
Hapana,japo ukiona kuna anayekuzoeA sana teach him how to fish and he will never come back but he will start up a restaurant to provides food to others
 
Hiyo ndio dawa, wakishona unawabania wanaacha wenyewe. Mimi nilizoea kutoatoa baadae nikashtuka baada ya kupiga mahesabu, nikaona sehemu kubwa tu ya kipato changu cha mwezi naishia kuwapa watu.
Nikasitisha rasmi, labda mtu awe yuko hospitali anahitaji hela ya dawa, kinyume na hapo sina hela.
Umejitahidi kuondoka ktk hali Kama hii. Cha ajabu waombao usitarajie kupata chochote kutoka kwao
 
Habari za majukumu wadau wenzangu.

Nimekuwa nikiombwa hela na watu tofautitofauti tangu nikiwa Mdogo kabisa. Nilipokuwa nasoma shule, nikirudi likizo watu huniuliza una buku hapo?

Hadi leo nahangaika na maisha yangu bado mizinga ni mingi. Mfano kuombwa Shililingi 200, 500, 1000, 5000, 10000 na wengine wakizidi hapo watajifanya wanakopa na hawanirudishii.

Kuna watu mtaani na hata ndugu zangu wenye uwezo kuliko mimi lakini siwaoni wakiombwa hela na watu. Nimewahi kuwauliza wakasema hakuna anayethubutu kuwaomba hela.

Hapa Kuna mtu ananisumbua tangu jana anaomba elf tano tu. Mwezi wa pili nilimpa elf 12 bure kabisa. Sasa karudi tena. Hali hii inatokana na nini? Napatwa na wasiwasi.
wewe Kama unayo toa, habari za kujifananisha na wengine temana nazo huna, mwambie huna siyo kosa kusema hivyo.

Na kumbuka kutoa siyo utajiri Bali ni moyo, hivyo umebarikiwa na moyo wa kutoa Jambo zuri kwa kiwango chake, Huku duniani hatufugi pesa twendenazo huko kwenye maisha mengine baada ya kumaliza safari hapa duniani.

Toa kwa kadri ya uwezo wako, pima shida ya mtu ukijiridhisha fanya maamuzi, wema ni adhina mbele ya safari kwako binafsi au kizazi chako Kama utakuwa umetoweka duniani. Hivyo sioni umuhimu wa ww kutaka kutafuta sababu kuwa kwanini iko hivi au vile.
 
Nilipitia hali kama yako mkuu. Mwanzoni nilikuwa mtoaji sana tu. Ilifikia kipindi nikitoka nyumbani mpaka kufika mfano dukani umbali wa kama mita 500 nakuwa nimeombwa na watu wawili au watatu. Mpaka wazee wenye nyumba zao za kupangisha waliniomba nauli ya kwenda mjini. Nikajiuliza, hawa wanaambiana? Nikaamua kuwa nawajibu sina. Ilinichukua takriban miezi mitatu kueleweka. Kwa sasa naishi kwa amani. Sio kwamba wameisha ila wamepungua sana. Wakati mwingine utoaji ni mzuri, ila isiwe mtu akikuona tu anawaza kupewa hela. Toa unapoweza na penye ulazima. Vinginevyo utakuwa unafanyia kazi watu..
 
Sawa nimekuelewa
 
Leo Mungu akikwambia uchague kuwa unaombwa au Wewe uwe unaomba,utachagua nini
 
Sawa nimekuelewa
dah, kacomment kako kamekaa kiunyonge unyonge sana na ndo hivyo hivyo kwenye maisha yako watu wanakuona we mnyonge na una huruma sana ndo mana hawaachi kukuomba.
mtu mwenye roho kama yako huwa anajiskia vibaya sana asiposaidia watu na watu wanaokuzunguka wanalijua hilo.

hata ukisema ubadili namba ya simu na uhame makazi, huko kwenyewe unakoenda utajifichafichaaa upole wako ila ipo siku tu utaonesha upole wako na hapo ndo watu watajua kuwa wewe ni mtoaji by nature.
ni sawa na kuficha kitobo cha chupi kwa kuvaa suruali ila ipo siku utaianika hio chupi nje na watu ndo watakapojua kumbe siku zoote hizo unavaa chupi yenye kitobo.

lakini pia hata uso wako na uongeaji wako inatosha kumuonyesha mtu kuwa wewe una huruma.
 
Mkuu umenigusa sana,nina siku ya tatu tu makazi mapya,lakini yale yale!
 
Wanaona una hali nzuri kuliko wao na una moyo wa kutoa.Ushauri wangu kwako;Usiwakimbie wala kuwachukia bali saidia unapoweza.
 
Back
Top Bottom