Tabia ya Wazazi/Walezi kuwarekodi Watoto video zinazotwezwa Utu wao na kusambaza Mitandaoni

Tabia ya Wazazi/Walezi kuwarekodi Watoto video zinazotwezwa Utu wao na kusambaza Mitandaoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ulinzi na usalama wa mtoto mtandaoni haumaanishi kudhibiti mambo mtoto anayoyaona mtandaoni au watu anaoongea nao pekee, lakini ni pamoja na vitendo vyote vinavyomuhusu mtoto vinavyofanyika mtandaoni kumdhalilisha au kuutweza utu wake.

Kushea, kupakia na kudaunlodi picha au video zenye maudhui ya udhalilishaji / ukatili kwa mtoto ni kosa ambalo mzazi / mlezi unapaswa kujiepusha nalo.

Hivi karibuni kumekuwa na tabia ya watu kuwarekodi watoto katika mazingira yanayotweza utu wao pasipo idhini yao na kisha kutumia video hizo kwenye mtandao. Wanaofanya vitendo hivi mara nyingi ni wazazi au walezi. Inafikirisha!

Inawezekana kusudi lako mzazi / mlezi kufanya hivi si baya. Walau mfikirie mtoto wako miaka 10 toka sasa na kwamba video / picha uloipakia inaweza kutumika kumdhalilisha kwa rafiki zake, 'adui' zake, na 'dunia.'

Mtoto ambaye hawezi kusoma akichekwa, mtoto akipigwa, mtoto akiongea maneno ambayo hayalingani na umri wake, watoto wakipigana n.k ni baadhi ya video zinazosambaa mtandaoni kwa sasa. Matukio haya yanaweza kurekebishwa / kukaripiwa bila kupakiwa kwenye mitandao.

Mlinde mtoto wako na mtoto wa mwenzio ukiona maudhui yoyote ya udhalilishaji wa mtoto katika mitandao ya kijamii kwa kuwaelimisha au kwa kutoa taarifa kwa kupiga simu namba 116 Huduma kwa Mtoto. Huduma hii haina malipo na inapatikana mitandao yote Tanzania.

Chanzo: Sema Tanzania
 
Wazazi wengine useless kabisa hatufundishani malezi lakn mara nyingi sampling za aina hii huwa zinatamani akikua mwanae afanane na yeye mara nyingi huwa hivo maji hufuata mkondo
 
Dunia ya kidijiti inawazuzua wazazi wengi siku hizi, na ndio maana suala la malezi kwa kipindi hiki ni changamoto
 
Bora hilo kuna wajinga kutwa kupost video za watoto wao
 
Privacy ni moja ya haki muhimu za watoto.

Utandawazi unawafanya watu wanakuwa wajinga wakati mwingine..
 
Ni kama paula na kajala.
Imagine mpaka imefikia hatua unampa mtoto jina la mama eti Paula Kajala inasikitisha sana.

Huwq najiuliza kama huyu Kajala ana wazazi? Atleast kama walimshindwa yeye basi wangemuokoa huyo mjukuu wao asipotee kama mama yao, lakini ndio mtoto ameshaharibika tayari.
 
Back
Top Bottom