Tabia ya Wazungu ya Kutopenda Umri Mkubwa

Tabia ya Wazungu ya Kutopenda Umri Mkubwa

8691jakigili

Senior Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
178
Reaction score
67
Wanawake maajuza walioishi katika "apartment building" moja walifika mahakamani wakishitakiana kwa mambo mbalimbali yaliyojiri katika pango hilo. Kelele zilizidi ndani ya chumba cha mahakama hata kumfanya Jaji kuwanyamazisha na kusema, "Kila mmoja atazungumza zamu kwa zamu na kwa utaratibu, hamwezi kuzungumza wote kwa wakati mmoja, kwani siwezi kuwasikiliza wote mkizungumza kwa pamoja. Nitaanza kumsikiliza mwenye umri mkubwa kuliko wote na atafuata anayemfuatia kiumri, vivyo hivyo hadi mwisho." Kesi iliishia papo hapo, kwani hakuna ajuza aliyetaka kuonekana ni mkubwa kuliko wote! Wote walikaa kimya hadi mahakamani inafungwa!!
 
Back
Top Bottom