Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

mie nimesema dini gani mkuu? labda ni iyo 95% iliyo baki
 
Nilikuelewa vema ulicholenga japo hukutaja waziwazi.
hapana mkuu sema ulijenga picha ambayo siyo naona umetaja hadi watu wasiohusika hadi kuitaja sudani

ila kwangu watu wa dini ile (sijui ni ipi) hawajawahi kuwa rafiki na mahusiano mazuri kwa kazini
 
Mkuu kwanza pole sana maana uchungu wake naujua vizuri maana na mimi ni muhanga.
Na mimi nipo na tabia kama yako na kila nikijitahidi nashindwa umbea kweli ni kipaji.
Hata mimi niko na misimamo yaani muda wa kujikomba sina,na kingine hata kama ni mkurugenzi usitake nikuogope ukinifokea tunafokeana.
Ukinipa kazi nitaifanya kwa ufanisi wa hali juu na kwa haraka ila usinipelekeshe.
Msimamo wako usiuache endelea nao ila hakikisha mambo yafuatayo.
1.Hakikisha unaiset vizuri CV yako iwe ya kimataifa au iwe very impressive yaani mkipeleka CV mahali watu 100 basi yako wewe ionekane the best na impressive.
Mimi nimefanikiwa kwa hili muda mwingine huwa natafutwa bila hata kuomba kazi.
2.Hakikisha ukipata kazi pesa unayoipata usitumie vibaya bali uwe unaitumia kuweka vitegauchumi vitakavyokusaidia kipindi hauna kazi,usidharau hata biashara ndogondogo za mitaani kama saluni na bodaboda watu zinawaweka mjini.

3.Hakikisha una networks/connections nyingi za watu especially Linkedin ndio mtandao unaunganisha professionals wengi duniani kisha jieleze kwenye profile na timeline kuwa unatafuta kazi utafanikiwa.
Ukishaweza kuyafanya hayo niliyokwambia basi hautababaikia kazi ya mtu.
Mimi mwenyewe hiyo hali ilinitesa sana mwanzoni nilikuwa nafanya kazi miaka 2 natenguliwa nakaa nyumbani mwaka 1 napata tena hadi sasa hivi nimeshazoea yaani hata nikikaa nyumbani mwaka mzima maisha yanaenda tu sina presha.
 
Nipo kwenye kihunzi hiki sijui ntavua watu eanajuana na boss balaa
 
Duu Mimi ya menikuta kwa went nyumba Kuna mzee nilipanga kwake deily anakaa sebleni ninavyo enda chumbani kwangu nakatisha kwenye korido namuona kwa mlango Sasa Mimi zangu ndani nikitoza hamna Cha salami nikiopoa demu hivyo hivyo saivi ameniondoa eti sisalimii Napo hapa nilipo nae ameanza eti rafiki zako wa kinge wanavaa nguo fupi alafu hawasalimii Sasa ni mademu zangu wengine niende Gest wakati Nina chumba
 
Aisee nipo mkoa wa Mara na nimekuwepo kwenye kampuni flani hivi ambayo Boss Ni mjomba angu haya mambo yamenipa shida Sana maana nisipomuona mjomba hata Mara moja kwa wiki hata kumpelekea umbeya wowote siku ya kwenda kumuona anisaidie ananiambia simsaidii kazi na pia hajui hata kazi ninayoifanya kwa hiyo hatanisaidia nilichomuomba nilivyosikia hizi habari niliacha kabisa kumwona na badaye nikaacha kazi.
 
Duh yaani wewe kufutwa kazi kampuni ikafa? Kwamba ni coincidence au ulikuwa na umuhimu kuliko members wote wa hio kampuni?
Mkuu inatokeaga tu mfano mimi nilisingiziwa napeleka habari makao makuu yanayoendelea pale wakati simjui mtu yoyote huko makao makuu mana nilikuwa intern na ni mikoa tofauti nikaona niache kazi mwezi haukuisha yule mzee pamoja na walionisingizia wakatumbuliwa.
 
Wengine wivu/vijicho vinawasumbua wenzenu kuwa mabosi
 
Kumbe tuko wengi mkuu,,,, Tabia hii ya kutopenda kujipendekeza, umbea, unafiki, uongo na uzandiki, ulinifanya nionekana nalinga tangu niko masomo, mpaka siku za hivi karibu ndio naona wameanza kunielewa,,,

Endelea na msimamo wako, mradi haumuonei mtu wala hauna nia ovu nyuma yake, iko Siku watakuelewa na kutambua dhamira yako njema!
 
Hapa kwetu kupo hivyo hivyo lakini Mimi siwezi na nimeshindwa, MD anaweza kuja site na simsalimii kabisa maana anapenda maneno maneno sana Mara fulani vipi, hivyo hata Salary sijaongezwa na nipo tuu nafanya kazi zangu,
Kikubwa zaidi ukifanya kazi kwa kutegemea mdomo basi ipo siku utakwama sehemu zingine
 
Tena huku private company tunapitia mengi sana, Boss anaweza kuja site huku kanuna anafoka kinoma, sisi hata kama umegombana na mkeo asubuhi huna budi kufanya kazi kwa ufanisi
 

Mimi naipokea hoja yako kwa namna mbili. Kwanza ninakubali, tabia hii ipo sana Afrika, Tanzania ikiwemo. Na si kwamba tumelogwa, bali ni utamaduni. Sisi hatujaweza kutofautisha mtu na ujuzi. Aidha, sisi mfumo wetu ni ule ambao mwenye nguvu(iwe uchumi, cheo, au hata nguvu ya mwili au vyovyote) ndiye mfanya maamuzi. Sheria zetu zipo vichwani, si zile ziliondikwa kwenye karatasi. Kwa hiyo, kuwa karibu na bosi ni muhimu ili nawe ufaidike maana bosi ni kila kitu.

Pili, kidogo ninatilia shaka staili yako ya maisha. Wakati hapo juu tumekubaliana kuwepo kwa udhaifu huu kwenye taasisi zetu, lakini, pia itategemea sana wewe pia unaishi vip na wanajamii ama wafanyakazi wenzako. Wengi tunakutana a changamoto za namna hii lakini unapokuwa na ushirikiano mzuri a wafanyakazi wenzako, Mungu pia anakulinda. Sasa picha ninayoiona,japo hujaweka bayana, ni kama vile wewe ni wale watu hawana time na mtu ofisini.Kama upo hivi, basi utapata changamoto hizi maisha yako yote. Si ajabu ukashindwa hata kuendesha kampuni yako mwenyewe.

Ni mtazamo tu
 
Mungu yupi sasa na wewe huamini katika huko kusikoonekana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…