Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Yaan kama unanisemelea Mimi

Hiki ndo kipo ofisin kwetu, usipojipendekeza unapigwa chini
Sio ofisin kwenu, ofisi karibia zote za kibongo ziko hivyo maboss wenyewe wanapenda kunyenyekewa na kupelekewa umbeya

Kuna ofisi moja mke wa bosi anafanya kazi sehemu nyingine, lakin anajua maisha binafsi ya karibia wafanyakazi wote
 
Unajua nimekaa hapa natafakari ya mtoa mada, kwamba kutokujipendekeza kunaweza kuwa sababu ya mtu kukosa kazi, naona kama haliingii akilini, labda kama kuna lingine ambalo mtoa mada anatuficha.

Hakuna anaepinga ya kuwa makazini kuna fitina, ila hakuna watu wanao kubalika makazini kama watu wanao jikubali, wachapa kazi na wasio na tabia ya kuwalamba miguu wakubwa, hili mimi nina ushahidi nalo na mpaka leo kutokana na kujiamini kwangu linanipa ugali, sambamba na kupiga kazi, yaani kazi ya fani yangu ukinipa naipiga mpaka una unafurahi.

Hayo mengine anayo yasema mtoa mada ni sahihi, lakini hili la kujipendekeza kidogo napingana nalo kwa mtindo huo.

Kwa ufupi ajira ni ngumu na upatikanaji wake ni mgumu pia.
 
Kujipendekeza kipaji Cha kipekee Sana..nilishashindwa na sitakuja kuweza kujipendekeza..never.
 

hata mm inakuta sana hiyo mpaka siku hizia nashangaa nakosa training za sana sina muda wa kujipendekeza kwa boss kabisa ndio nilivyo
 
Nakujuaga dada angu hutakagi makuu, ila sometimes uchangamke utakosa fursa, [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nifundishe kuchangamka mdogo wangu..maana napoelekea ni huko huko kwenye kukosa fursaa😂😂😂
 
Hali mbaya kwenye makampun binafsi ambapo hatima ya kazi yako anayo boss wako nmegundua ni bora kujiajir kuliko kuishi na mastress kwa kujikomba na kuwalamba miguu miungu watu (boss)
 

Inategemea unatafsiri vipi kusabahi.
 
Ni kweli maboss wengi wanapenda umbea

Mimi sehem nayopiga kazi wamenipga majungu weeeeee mpaka wamechoka Ila nachojua ni mungu na pia cheti nilichonacho boss imebidi awe mpole tu ananimind kimya kimya Ila Hana la kufanya
 
Ndio mkuu ila daah sijazoea[emoji16]
Mimi kuna kasehem nlikuwa nimejishkiza miez 3 tu wamenichongea baada ya kuwakarbisha geto walitaka kufaham nnapokaa nkaona haina shaka, wakakuta chupa kazaa za spirit kwenye cabin "ooh jamaa mlevi, jamaa anapenda madem ana boksi la ndom, jamaa atakuwa mpiga dili, jamaa kazini anapendeza zaid ya boss" nkapigwa chini unemployed and broke

Yan ntanunua Bastola 1day...
 
Iko hivi bosi anakua anapelekewa habari zako mbaya, ili upige counter attack inabidi nawewe uwe unajipendekeza kwa boss ndo wengi wanavyofanya hivyo
 
hata mimi mkuu niko kama wewe.
Watu wa aina hii hat akama wakisota il andio huwa wanadumu.
Usikubali kubadili tabia kaza utatoboa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…