Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Tabia yangu ya kutojipendekeza, kusujudia maboss na kutokuwa mfitini inanisotesha mtaani

Yaan kama unanisemelea Mimi

Hiki ndo kipo ofisin kwetu, usipojipendekeza unapigwa chini
Sio ofisin kwenu, ofisi karibia zote za kibongo ziko hivyo maboss wenyewe wanapenda kunyenyekewa na kupelekewa umbeya

Kuna ofisi moja mke wa bosi anafanya kazi sehemu nyingine, lakin anajua maisha binafsi ya karibia wafanyakazi wote
 
Unajua nimekaa hapa natafakari ya mtoa mada, kwamba kutokujipendekeza kunaweza kuwa sababu ya mtu kukosa kazi, naona kama haliingii akilini, labda kama kuna lingine ambalo mtoa mada anatuficha.

Hakuna anaepinga ya kuwa makazini kuna fitina, ila hakuna watu wanao kubalika makazini kama watu wanao jikubali, wachapa kazi na wasio na tabia ya kuwalamba miguu wakubwa, hili mimi nina ushahidi nalo na mpaka leo kutokana na kujiamini kwangu linanipa ugali, sambamba na kupiga kazi, yaani kazi ya fani yangu ukinipa naipiga mpaka una unafurahi.

Hayo mengine anayo yasema mtoa mada ni sahihi, lakini hili la kujipendekeza kidogo napingana nalo kwa mtindo huo.

Kwa ufupi ajira ni ngumu na upatikanaji wake ni mgumu pia.
 
Kujipendekeza kipaji Cha kipekee Sana..nilishashindwa na sitakuja kuweza kujipendekeza..never.
 
Kama kawaida baada ya kumaliza chuo nikaingia mtaani kusota na maisha bahati nzuri nikapata intern kwenye moja ya taasisi za serikali zinazolipa vizuri.​

Changamoto ikawa kumbe kwenye taasisi hizi za serikali inatakiwa ufanye kazi kwa bidii bila kusahau kujipendekeza kwa boss.​
Kwa jinsi nilivyo tabia yangu ya kutopenda kujipendekeza wala kufitini wafanyakazi wenzagu mm nikawa natimiza Majukumu kama kawaida.​

Kumbe ilitakiwa niwe naenda hata kumuona boss personly angalau mara moja kwa wiki kumsalimia tu ambavyo wengine hufanya sasa mm nawaza nikamuone manager nimweleze nini Cha zaidi wakati meeting za Kila wiki tunakutana na kila mtu anawasilisha ripoti yake?.​

Basi bwana boss akaanza kulalamika ooh sina msaada kwenye office ikabidi nifuatilie kujua ninakwama wapi bassi wadau wakanitonya jipendekeze nenda hata mara moja peleka umbea wowote ule atakukubali tu.​

Asikwambie mtu hakuna kazi ngumu Kama kuwa mmbeya eneo la kazi Kama hauna tabia hiyo.​

Mm nikasema potelea mbali ilimradi natimiza Majukumu yangu na nipo qualified siwezi kujipendekeza kwenye ofsi hii nitapata kazi hata kwingine.​

Mkataba wa intern ukaisha boss Kama kawaida akaaniambia nitafute kazi sehemu nyingine.​

Mwamba nikaona siyo kesi nikaingia mtaani nikapata kazi kampuni nyingine ya kibongo aisee kule ndo ikawa balaa bila kuwa mbeya humalizi mwezi unatimuliwa boss anataka kila siku mpishane na wafanyakazi ili apate taarifa mara huyu kapeleka fulani mwizi kaiba mafuta, kifusi.​

Daah nikaona pia isiwe kesi nikaacha kazi.​
Sasa Nina mwaka nasota mtaani nimezunguka kinoma hamna kazi kila Kona patupu wadau wanashauri tafuta hata viongozi wa kisiasa ujipendekeze kazi siku hizi kujuana mm naona wananisumbua tu.​

Natafuta kazi nikiamini qualifications zangu zitanibeba lakini patupu nimeapply sehemu nyingi hata kuitwa hakuna.​

Nikatafuta mpaka sehemu za vibarua patupu. Sasa nawaza hii tabia ya kutojipendekeza nitaachaa vipi maana kubadili tabia ni ngumu kama kubadili ngozi.​

hata mm inakuta sana hiyo mpaka siku hizia nashangaa nakosa training za sana sina muda wa kujipendekeza kwa boss kabisa ndio nilivyo
 
Nakujuaga dada angu hutakagi makuu, ila sometimes uchangamke utakosa fursa, [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nifundishe kuchangamka mdogo wangu..maana napoelekea ni huko huko kwenye kukosa fursaa😂😂😂
 
Hali mbaya kwenye makampun binafsi ambapo hatima ya kazi yako anayo boss wako nmegundua ni bora kujiajir kuliko kuishi na mastress kwa kujikomba na kuwalamba miguu miungu watu (boss)
 
Mkuu ukifika kazini fanya kilichokupeleka, habari za kusabahi ni nje huko baada ya muda wa kazi. Mambo ya kusabahi watu ofisini ndio kujipendekeza kwenyewe. Unashindwa kutulia sehemu yako ya kazi unazunguka kusalimia watu, kama sio kujipendekeza ni nini?

Inategemea unatafsiri vipi kusabahi.
 
Ni kweli maboss wengi wanapenda umbea

Mimi sehem nayopiga kazi wamenipga majungu weeeeee mpaka wamechoka Ila nachojua ni mungu na pia cheti nilichonacho boss imebidi awe mpole tu ananimind kimya kimya Ila Hana la kufanya
 
Ndio mkuu ila daah sijazoea[emoji16]
Mimi kuna kasehem nlikuwa nimejishkiza miez 3 tu wamenichongea baada ya kuwakarbisha geto walitaka kufaham nnapokaa nkaona haina shaka, wakakuta chupa kazaa za spirit kwenye cabin "ooh jamaa mlevi, jamaa anapenda madem ana boksi la ndom, jamaa atakuwa mpiga dili, jamaa kazini anapendeza zaid ya boss" nkapigwa chini unemployed and broke

Yan ntanunua Bastola 1day...
 
Unajua nimekaa hapa natafakari ya mtoa mada, kwamba kutokujipendekeza kunaweza kuwa sababu ya mtu kukosa kazi, naona kama haliingii akilini, labda kama kuna lingine ambalo mtoa mada anatuficha.

Hakuna anaepinga ya kuwa makazini kuna fitina, ila hakuna watu wanao kubalika makazini kama watu wanao jikubali, wachapa kazi na wasio na tabia ya kuwalamba miguu wakubwa, hili mimi nina ushahidi nalo na mpaka leo kutokana na kujiamini kwangu linanipa ugali, sambamba na kupiga kazi, yaani kazi ya fani yangu ukinipa naipiga mpaka una unafurahi.

Hayo mengine anayo yasema mtoa mada ni sahihi, lakini hili la kujipendekeza kidogo napingana nalo kwa mtindo huo.

Kwa ufupi ajira ni ngumu na upatikanaji wake ni mgumu pia.
Iko hivi bosi anakua anapelekewa habari zako mbaya, ili upige counter attack inabidi nawewe uwe unajipendekeza kwa boss ndo wengi wanavyofanya hivyo
 
hata mimi mkuu niko kama wewe.
Watu wa aina hii hat akama wakisota il andio huwa wanadumu.
Usikubali kubadili tabia kaza utatoboa tu
 
Back
Top Bottom